Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Baada ya mafunzo ya KIMWANA katika KITCHEN PARTY akufanyiayo KIMWANA yanaweza kuwa sio mapenzi tena!:-(

>> Monday, November 01, 2010

MTU yeyote yule,...
... BAADA ya kufunzwa jinsi ya kuonyesha PENZI,....

.... kama ni mwanafunzi mzuri  ataweza kuonyesha PENZI VYEMA TU hata kama amuonyeshaye mahaba wala HAPENDWI  zaidi tu ya pochi lake, KUTIMIZA WAJIBU kwa kuwa mpenzi kachaguliwa na mama, au tu kutimiza hamu yakupewa mimba ndani ya ndoa ili mitoto yake ikishatotolewa isionekane HARAMU.:-(

Swali:
  • Kwani unafikiri MABAAMEIDI kwenye mabaa  wote wamchekeaye MTEJA baada ya kujifunza kuwa wakilichekea teja litakuja tena huwa kweli wanalipenda hilo limteja LEVI au huwa hata wanafurahia hiyo kazi ya kujichanganya na MILEVI?Ndio,...
....kuna maswala watu HUJIFUNZA,...
.... na wakikubuhu hata katika kukuonyesha jinsi upendavyo kuona ndio kuwa ni DALILI unapendwa,...
.....unaweza KUDHANI NI KWELI unapendwa ndio maana asiyekupenda akujuliaye anaweza kukuchuna buzi na SWALA zima la kustukia yote ni maigizo ni pale  umeshachunwa.:-(

Swali:
  • Unabisha?
  • Kwani baada ya MKEO kupata DIGIRII  ya KITCHEN PARTY unafikiri afanyacho ni MAPENZI KWELI  au tu ni kukupagawisha kwa kupatia kukukuna KIPELE bila ya hata PENZI kwa kufuata moja mbili tatu alizojifunza za jinsi ya kukupagawisha?Ndio,...
.....KUPENDA mtu ,...
.... na kujulia jinsi ya kumuonyesha mtu umpendavyo ni TOFAUTI,....

..... ndio maana waweza kuwa unampenda sana mme wako lakini MMEO ASISTUKIE HILO na   akanogewa  ZAIDI na malaya  ambaye ni shoga wako KWA KUFIKIRI HUYO NDIYE ANAYEMPENDA ZAIDI kwa kuwa HALALAMI  kama wewe na SI MCHOYO KIUTU UZIMA kikipengele ,...

...kwa jinsi TU shoga yako ajuliavyo shughuli  katika  KUMPAKULIA PENZI BWANA WAKO kihuduma KWA KUIBIA kimpekecho wa dhati za mpaka  hata  kumkanda kwa maji ya karafuu  azipendazo SHOGA YAKO alizojifunza  Tanga  , huduma zile ambazo WAHAYA ni mabingwa na hata zile za KIZENJ za chapchap  kwa siri wakati wewe  hauko.:-(


NI WAZO TU HILI MHESHIMIWA Bi MKORA wala usikonde!:-(

Hebu tupate ESTEBAN Y LA BANDA mix - Pale Vu FranceAu tu King Yellowman arudie kudinya- Still Be A Lady

1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

emu-three 9:48 am  

Hapa twaweza kusema lipo penzi la kujifunza na penzi halisi ambalo lipo moyoni.
Umenikumbusha juzi nilihudhuria kitchen party ya mwanaume...Oh,inaitwaje vile..`boy party' au nini vile? mmmmmh,
Katika muda wa masaa mawili au matatu watu wanatoa hoja jinsi gani ya kumlea mke, nikajikuna kichwa kuwa kumbe haya yana shule.
Lakini shule ya masaa inataraji matokea ya miaka kenda au zaidi na je kuna uelewi wa darasa hili kama pendo halipo? je huko kwa akina mama wamemfunda nini mwali ili yaoane na haya mume mtarajiwa.
Isieje ikawa kule anafundwa mafiga matatu na huku anafundwa kuwa `mume' asitawaliwe na mke, na kwahiyo yeye sio mafigo tu bali ni jiko la gesi, au la mkaa au la umeme..`movable' leo kwa huyu kesho kwa yule...

Mhh, mkuu sijui nipo sawa au nimeenda nje ya mada...mmmmh, najua utaguna kwa waza au kwa hadithi njoo, utamu njoo, ....kwaheri!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP