KUMBUKA TU kuwa wakati kazi ya GYNECOLOGIST na ANDROLOGIST zote hufanya MTU achungulie za watu NYUCHI,....
>> Thursday, November 11, 2010
.... LABDA kiangaliwacho na DAKTARI WA UCHI  bado si  UCHI katika MTAZAMO kama wa  mwanafunzi aliyeanza KUBALEHE katika majaribio ya kumchungulia mwalimu wa kike MWENYE CHUPI NYEKUNDU aliyekaa vibaya DARASANI.:-(
Ndio,....
 .... kuangalia kitu mara kibao hutegemea UNATAFSIRI nini  katika uangaliacho ,....
...au unalenga kuona nini kwa jinsi ya uangaliavyo KITU,....
.... kitu ambacho kinaweza kukusaidia kuelewa ni kwanini SI KILA SIKU uwaangaliapo OMBAOMBA uonacho ni matatizo ya umasikini hasa kama  KWA JINSI uwaangaliavyo  ulengacho  kitafsiri ni BUGHUDHA wakupazo kwa kukuombaomba tu MIPESA YAKO  au tu ni KAMASI tu  na ukurutu kama tu UKOMA   ambavyo wewe KIBISHORORO  ni ambavyo vikutiavyo KINYAA!:-(
Swali:
- Kwani unafikiri WENYE PESA ZAO BONGO wale WAZEE wa GETI kali na watoto wao wa GETI KALI unafikiri ni kila siku waonacho nje ya mageti yao yalindwayo na maaskari ili MASIKINI wasiingie huwa ni kuna UMASIKINI Tanzania wakati wenyewe na magari yao baab kubwa hawaujui huo UMASIKINI?
- Unafikiri mtu kama Rais Kikwete akiangalia ombaomba huwa anawaona kama wewe uwaonavyo ambaye unapigana nao vikumbo mitaani?
Ndio ,....
.... kama wewe hupendi pombe za KIENYEJI,....
....uonacho wakati unaangalia MATAPUTAPU chaweza kuwa ni tofauti na MPENZI wa pombe za kienyeji aonacho ingawa mbele ya macho KITU  ni kile kile,........kama tu ilivyokuwa kwa wapenzi wapya waonavyo kwenye uchunguzi wa zao NYUCHI mpya walizoanza kugawiana HIVI KARIBUNI utofautianavyo waonavyo MUME na MKE wa miaka LUKUKI waliozoea kugawiana embedodo za KIKUBWA.:-(
Swali:
- AU?
- SI unajua ukiizoea njia ndivyo jinsi upungukiwavyo na utaalamu wa kustukia mengi katika hiyo njia kwa kisingizio unadhani unajua kila kitu kilichokuwepo katika hiyo RODI?
- SI unakumbuka kila siku siowote uliowaelekezea sura na macho ni kweli umewaona?
Ndio,....
.... mtu apendaye MATITI,...
...anaweza kuwa kila siku hastukii una bonge la MATEGE kwa kuwa  kila akikuona KIMWANA aonacho ni HOTELI TU ZA MTOTO ,...
NI WAZO tu HILI MHESHIMIWA!
Kamusi kidogo:
Gynaecology ni SAYANSI na TAALUMA ya KIDUDE cha kike. Na GYNECOLOGIST ni mtaalamu ambaye akienda kazini anachungulia kitaalamu hicho kidude cha kike.
ANDROLOGY ni sayansi na taaluma ya kidude cha kiume.
NIMEACHA!
Hebu tu NINA SIMONE abadili na kurudisha ustaarabu hapa kijiweni kwa bonge la jabali-To be YOUNG, gifted and BLACK
Au tu TRACY CHAPMAN na LUCIANO Pavarotti wajaribu kistaarabu kulainisha kwa -Baby can I hold U
 
  
 Posts
Posts
 
 




1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Haya Mheshimiwa na mtakatifu...
Ulikuwa unawaza nini leo :-)
Post a Comment