Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

RIDHIKA uendelee kuwa MALAYA au USIRIDHIKE ili uendelee kuwa malaya!:-(

>> Friday, November 26, 2010

Swali:

  • Si unajua KURIDHIKA na KUTORIDHIKA vyote vinaweza kuendeleza TATIZO lilelile?


Ndio,...
....kwa kuridhika,...
MJINGA anaweza kuendelea kuwa MJINGA,...
...MASIKINI akaendelea kuwa MASIKINI,....
...kama mwerevu awezavyo kuanza kugeuka MJINGA.:-(

Ndio,...
....na kwa KUTOKURIDHIKA,...
...tajiri ni MASIKINI,...
..... mwenye SURA NZURI anaweza kujiona anasura mbaya kama kinyeo cha KUKU mwenye mdondo,...
...ingawa MJINGA kwa kutoridhika na kuwa mjinga labda ndio mwanzo wake  wa UEREVU.:-(

NI wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(

Hebu  Jean-Claude Naimro wa  Kassav arudie-Ave'w Doudou


Au tu Jocelyne BĂ©roard wa Kassav ashindilie na-Siwo


Au tu SIMPLY RED wabadili kabisa mchezo wa kujipikilisha kwa-Holding Back The Years

9 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 1:27 pm  

kaazi kwelikweli hapa!!!

emu-three 2:50 pm  

Ni kweli ni bora kuridhika kwa ulichajaliwa nacho, hata kama kina viraka hadi kwenye nanihii, ili uendelee kuwa masikini, kuliko kuota ndoto za alinacha, ili mwisho wa siku uwe tajiri wa umasikini!
Ni waso tu katika wazo lako mkuu!

Koero Mkundi 5:21 pm  

dada Yasinta sio kazi tu bali ni shughuli...LOL

Kaka nakutafuta nyuma ya pazia...LOL

chib 6:18 pm  

Bado nakuna kidevu, maana kichwa kimewaka moto kwa kukuna katika tafakuri ya ujumbe huu wa hapa

SIMON KITURURU 8:26 pm  

@Da Yasinta: DUH!
@M3: Mkuu unauhakika?:-(
@Da Koero: Ndio nimetoka bafuni na na taulo tu kiunoni , njoo TU nyuma ya pazia!:-(


@Mkuu CHIB:Asante kwa kuwa sijui kwa nini nahisi wewe ni miongoni wa mnipatao wakati nashusha UjingaBUSARA kwa kuwa kuna baadhi nahisi wakistukiacho hapa KIJIWENI KWANGU ni UJINGA na matusi tu!:-(

@Wote: Kwa mara nyingine WIKIENDI NJEMA wajameni!

Mzee wa Changamoto 10:57 pm  

Nami nawaza kuwa AWAZAYE si HUWAZA KUWAZA? Hakuna asiyewaza hata kama anachowaza ni kutowaza. Yes!! Thinking about thinking or thinking about NOTHING....

NDIO!!!
....naamini hakuna siyeridhika japo RIDHIKO laweza kutomridhisha ama kukatishwa
Narudia tena kuwa HAKUNA ASIYERIDHIKA, kwa kuwa anayeamini kuwa hajaridhika, anakimbia ukweli kuwa hajamaliza harakati za kusaka ridhiko lake.

KWA HIYO!!!!
...anayesema HAJARIDHIKA ni yule aliyeridhika kutoendelea kusaka ridhiko alipendalo. Na ndio maana kuna RIDHIKO MOJA TU KWA ALISAKAYE na kisha kuna wale waamuao kuridhika kutolikamilisha na kusingizia HAWAJARIDHIKA.
Anayesaka MAENDELEO anatambua kuwa MAENDELEO HAYANA MWISHO. Kwa hiyo hakuna kuridhika mpaka siku unapokufa kwani kila hatua upigayo ni changamoto ya hatua ijayo, na kama nia ni kusaka maendeleo, ina maana hatua upigayo ni "msingi" wa ijayo hivyo SONGA MBELE KUSAKA RIDHIKO.

Naaaa!!!
.....anayedhani ni mzuri ajue kuwa UPEO WAKE JUU YA UZURI ndio ridhiko lakini si maana halisi ya UZURI kwani kila uchao jicho la mtaka-TIFU linaona "kinyemi" kinachomfanya afikirie mara kadhaa juu ya yule wa jana (japo yawezekana nusu nyama, nusu plastiki).

Kwa maana nyingine
...... hakuna asiyeridhika, bali watu hawa huridhika kuacha kusaka ridhiko na kujitafutia njia m'badala kuhusu ridhiko lao.

Labda
....kichwa cha habari hapa kingekuwa "RIDHIKA uendelee kuwa MALAYA au RIDHIKA KUTOUKIMBIA UMALAYA ili uendelee kuwa malaya"(

NAWAZA KWA SAUTI TUUUUUUUU!!!!!

TUONANE "NEXT IJAYO"

SIMON KITURURU 12:41 am  

@Mzee wa CHANGAMOTO:

Nanukuu``Hakuna asiyewaza hata kama anachowaza ni kutowaza. ......NDIO!!!
....naamini hakuna siyeridhika japo RIDHIKO laweza kutomridhisha ama kukatishwa
Narudia tena kuwa HAKUNA ASIYERIDHIKA,....´´


Naendelea kuwaza unachoniwazisha!:-(

Unauhakika lakini na unachowaza?

emu-three 9:56 am  

@Da Yasinta: DUH!
@M3: Mkuu unauhakika?:-(
@Da Koero: Ndio nimetoka bafuni na taulo...!
Mambo hayo mkuu, umeniuliza nina uhakika?
Nilikuwa nawaza tu, ni ukiwaza, unaweza ukawaza hata kuwa `Kiwete, acha Kikwete, Obama, huyo huyo Obama, na ukajenga serikali yako akilini tu!
Kwahiyo usishituke mkuu, nawaza na niwazalo, huenda ukawa hujaliwaza, na ukiliwaza, huenda ninawaza tofauti na nililowaza awali, hata ukiniuliza nitakupinga! Au? Mkuu usijali na wasemayo wapita njia! Toa vitu tukune kuchwa au tugunwe, na kutoka kapa kama mtihani wa kemia wakti wewe umesomea masomo ya biashara!

SIMON KITURURU 10:07 am  

@M3:

``....nawaza na niwazalo, huenda ukawa hujaliwaza, na ukiliwaza, huenda ninawaza tofauti na nililowaza awali, hata ukiniuliza nitakupinga!``

DUH!Unanikunisha kichwa kweli MKUU!


Nje ya TOPIKI:

Mkuu asante sana kwa kutonitenga hapa kijiweni Mkuu!

Pamoja sana tu!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP