Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kwa kuwa kuna mwanafunzi wa PENZI anogewaye na SWALI LAKE kuliko JIBU LA WENGINE ikiwa ni hata lile LA MWALIMU wa chuma mboga!:-(

>> Wednesday, November 24, 2010

 [Angalizo: Wazo limepinda kwa hiyo cheza NALO kwa stepu usijemkanyaga mwenzio katika  kulielewa!:-(]


Ndio,....
....kunawaulizao swali AMBAO hawasikilizi wajibiwayo MAJIBU hata katika kitendo cha mapenzi,....
....kitu KWA BAHATI MBAYA kifanyacho kitendo kizima kigeuke PUNYETO.:-(

Swali:

  • Kwani maishani hujawahi kukutana na AKUULIZAYE swali halafu wakati unamjibu ukastukia hasikilizi jibu LAKO?

Ukiuliza,....
....jaribu angalau kusikiliza jibu kwa kuwa tukiachana na mambo mengine,...
...HIYO ni TABIA nzuri!:-(Na kama unajua jibu,.....
.....na bado unauliza ili kustukia UJINGA wa atakaye kujibu au tu kutaka POINTI ZAKO fulani TUZIELEWE,...
.... bado angalau sikiliza majibu  hata KAMA  ni ya kijinga kwa kuwa labda UTAFIKISHA ujumbe vizuri uliotaka kuufikisha kwa kuchokoza swali ,UTAJIFUNZA USICHOTEGEMEA au angalau uwaulizao UTAWAELEWA hata mambo mengine AMBAYO HAYAKULENGWA NA SWALI  kama ya jinsi ya kuwaibia  VIZURI.:-(


Swali:
  • Kwani ulikuwa hujui kuna wanogewao na SWALI LAO kuliko jibu LAKO sahihi?

Katika kuiongezea tako hoja kiwanzabanga :


Moja ya kisababishacho watu kunogewa na SWALI LAO kuliko JIBU la wengine,....
...hutokana  na HATARI ILIYOENEA KATIKA JAMII ambayo ni ,...
...WATU kuchagua WATAKACHO kujua  kitu kifanyacho katika stori nzima ya TITI ZIMA wanaamua kujifunza na kusikiliza kipengele kimoja tu ambacho chaweza kuwa ni cha CHUCHU tu.:-(


Na katika TITI aliyeweka kipaumbele kujua mishemishe ya CHUCHU TU,....
....aulizapo kuhusu ya TITI kwa kawaida MITA BENDI ZATE zinatyuni kwenye ya CHUCHU TU na ukianza kuongelea  maeneo mengine ya uzuri wa TITI kwenye jibu lako anaanza kusahau kuwa unamjibu  SWALI LAKE na hata kuanza kufikiri hujui jibu la swali lake,...
... kitu ambacho mwisho wa siku husababisha ANOGEWAYE na swali lake na sio JIBU lako ndio anayelosti kujua mfukuto mzima wa MITA BENDI za mpaka ni nini kitekenyacho CHUCHU.:-(

Swali:
  •  Si unajua kwa kuchagua utakachokujua , maana yake umeweka mipaka ya KUJUA kwako kwa hiari kitu ambacho chaweza kudhoofisha UJUAJI WAKO?
  • Si kunauwezekano kwa kuchagua utakacho kujua katika TITI ni CHUCHU tu maana yake unaruka ulimwengu mzima wa elimu ya TITI zima ambalo bila hilo labda chuchu yako UIPENDAYO SANA  isingekuwa na geto la kuishi kama vile achaguaye kutafiti kinyeo na KURUKA utafiti wa TAKO zima?

Ndio,...

.....kuna wanogewao na MASWALI YAO au mpaka sauti zao wenyewe,...
....na kwa kunogewa huko HAWASIKILIZI JIBU lako au hata la Prof. Mbele la ni kwanini ni muhimu KUSOMA VITABU kitu ambacho  labda wapungukiwao  kitu-   tukirusha shilingi ,...
....labda sio wale waliojibu JIBU LISILO SIKILIZWA!:-(


NI wazo tu hili MKUU na RUKSA kutolielewa katika kigezo cha kuwa sikila mtu lazima aelewe BEBERU anatafutanini katika kulamba mkojo wa MBUZI.:-(

Hebu OutKAST wabadili na kuleta ustaarabu kwa kitu-So Fresh, So Clean
Au tu India Arie arudie kitu-VIDEO

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

emu-three 3:02 pm  

Ndio mkuu unaweza ukauliza swali ukiwa unataraji jibu, ambalo una mwanga kidogo na jibu lake, lakini mjibuji akakupa jibu ambalo ni giza kwako.
Nataka nanihii, ukaomba, jamaa akakujibu kamwombe nanihii wako...kumbe hukuwa na maana ya nanihii, yeye kakuelewa vinginevyo...wakati anakujibu utakuwa unatafakari hivi ananijibuu kituu gani...humsikilizi yeye unawaza...mmmh, mkuu sijui nimechemsha, manake leo, ....leo....leo!

SIMON KITURURU 11:05 am  

@M3: Hujachemsha Mkuu cha zaidi umeniongezea kitu kwenye mtazamo ambacho sikukifikiria!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP