Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Nasikia mpaka LEO HII hakuna mtu aliyewahi kukutana na MALAYA ajuaye kila kitu katika UMALAYA ndani ya dunia hii.:-(

>> Thursday, November 04, 2010Ndio,....
.... katika DUNIA HII ambayo unaweza kukuta PAPA BENEDICT ajulikanaye kwa kutofanya ngono ndio MSHAURI MKUU kwa WAKATOLIKI katika maswala ya KONDOMU,....

.... ni rahisi  kuchanganyikiwa na kusahau kuwa hapa DUNIANI hakuna mtu ajuaye kila KITU.:-(

Swali:
  • Unabisha?


Ndio,....
.... ukikutana na MTU ajifanyaye kuwa anajua kila kitu,....
..... kuwa muangalifu sana kwa kuwa kuna uwezekano anachanganya pointi za BICHIKOMA na zile za PEKOSI  wakati aongeleacho ni chupi.:-(
NI hilo TU Mheshimiwa NA NI WAZO TU HILI Bingwa!

Hebu tubadili kwa kumdeku Victor WOOTEN akichezea tena  gitaa la bezi....katika-Slow GrooveAu tu BOOTSY COLLINS naye achezee hili gitaa la BEZI...


Au turudi tu tena KAMERUNI ili KOOL BASS naye acheze na gitaa hili la bezi katika nyundo-NDOME

6 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

emu-three 11:47 am  

Wapo wanaojua kila kitu hukuwaona majukwani wakimwaga sera zao. Hawo wanajua hata umasikini ulikuwa utajiri...watu eeeeh, mpe huyo mpe huyo.
Sasa jana tu umeme umeanza kufanya vituu vyake, giza totoroo...wanajua hawa, watakuambia mmmh, bwawa limeanza kukauka...lakini majukwani wameshau walichosema!
Wanajifanya wanajua kila kitu, kumbe kujifanya wengine huita matusi!
Ni hayo tu mkuu

EDNA 12:20 pm  

Hehehee,mie bora nikutakie siku njema tuuuu Mtakatifu.

chib 5:02 pm  

!!!!

Adela Dally Kavishe 5:23 pm  

duuuh aisee hahahaha sijui nisemeje ila inawezekana

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) 12:45 am  

"Ndio,....
.... katika DUNIA HII ambayo unaweza kukuta PAPA BENEDICT ajulikanaye kwa kutofanya ngono ndio MSHAURI MKUU kwa WAKATOLIKI katika maswala ya KONDOMU,..."

Vipi tena Mtakatifu "unamzodoa" Mtakatifu mwenzio? Tuna uhakika kwamba hafanyi ngono?

Kwa vile hatujui tukijuacho kuhusu kile tukijuacho - hata iwe tumekisomea kwa miaka nenda miaka rudi mpaka tukafikia hata kuitwa mabingwa - mimi nadhani hakuna tujualo.

Hebu leo tufanye shindano la kumtafuta mtu anayejua kuiba kuliko wote tuone itakavyokuwa. Utagundua kwamba hata yale majambazi ya kimataifa yataogopa kushiriki. Hata mafisadi wanaovuma kila kona watanywea! Kula je? Ni nani anajua kula???

Wapo wanaoamini kwamba ni kutokana na upungufu wetu huu hata tulifikia hatua ya kugundua "Mtakatifu" Ajuaye kila kitu - bingwa wa mipango aliyepanga kila kitu hata kabla hatujawa!

Kama kawaida fikra nzuri!

SIMON KITURURU 4:51 am  

@M3: DUH!
@Edna: Haya mwaya nahisi kunakitu ulitaka kusema ila ukakimezea.Asante kwa kunitakia siku kibonge lakini!

@CHIB: Mmmh!
@Adela:Kwa sentensi yako NDIO ushasema Dada yangu!:-(
@Mkuu Matondo: ``Tuna uhakika kuwa hafanyi ngono?´´ -Swali gumu hilo YAKHE kwa kuwa jinsi Mapadre na Maaskofu wa KIKATOLIKI wadakwavyo siku hizi kwa kutafuta uroda mpaka kwa watoto, labd ni MUNGU mwenyewe anajua hilo kwa kuwa Vatican si atleast masista wapo?

Na hapa ;``Hebu leo tufanye shindano la kumtafuta mtu anayejua kuiba kuliko wote tuone itakavyokuwa. Utagundua kwamba hata yale majambazi ya kimataifa yataogopa kushiriki. Hata mafisadi wanaovuma kila kona watanywea! Kula je? Ni nani anajua kula???´´- umenikata kabisaa cha kuongezea.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP