Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Ukijisahau na yako SASA HIVI,....

>> Tuesday, November 09, 2010

... unaweza KUMJAJI mtu VIBAYA akidai  kwake cha muhimu kuliko vyote DUNIANI sasa hivi ni CHIPSI MAYAI!:-(


Swali:
  • SI unakumbuka kutokana na KIBANO cha MAISHA si kila mtu sasa hvi CHA MUHIMU KWAKE ni shule KAMA WEWE, mavazi kama SHOGA YAKO,  nyumba kama  MDAU wako, gari kama HAWALA yako hasa ukizingatia kama umewahi kuumwa na njaa kisawasawa wakati huo akili yako ikipacho kipaumbele ni MSOSI kitu kiwezacho kufanya ukapigia kura FISADI kwa ahadi ya UBWABWA?


Ndio,...
.... KILA MTU akikuambia ni nini kwake ni MUHIMU SANA sasa hivi,....
......unaweza kushangazwa kukuta MCHUNGAJI  WA KILOKOLE cha muhimu sasa hivi ni kutofumaniwa na kipenzi chake AMBAYE ni mke wa JIRANI yake,....
... na wala sio BIBLIA awafundishayo watu sasa HIVI.:-(

Swali zaidi pembeni kidogo ya tundu:
  • Kwani  unauhakika cha muhimu kwako hakijawahi kuwa ni KITU KIDOGO tu kama hamu tu ya KUCHEKEWA na LIMTU fulani ?

NI wazo tu hili MTAALAMU na wala  usikonde!

Hebu Boyz II Men warudie-Tracks of my Tears


Au tu Boyz II Men waachie tu na-Water runs Dry

Au tu Boyz II Men wamalizie tu na - On Bended Knee

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

emu-three 10:14 am  

Cha muhimu kwa mtu ni wakati uliopo, na wakati ujao ni matumaini! Ukiwa na njaa cha muhimu ni kula, ukiwa na nanihii, cha muhimu ni kutafuta nanihino,
Mkuu mimi hapa cha muhimu ni kupata pesa, kama unazo nirushie...lol!

SIMON KITURURU 1:30 pm  

@M3: Hapo umenena Mkuu! Emu-three umejaribu ufisadi katika kusaka pesa?

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP