Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

MHESHIMIWA kiheshima umefanikiwa KUDANGANYA MTU leo?

>> Friday, November 05, 2010

 Ndio,...
.... inasemekana KILA MTU ndani ya KILA SIKU ,...
.....kuna kitu adanganyacho hata kama ni kwa KUJIPODOA ili watu WADANGANYIKE kuwa  KIGOLI  ana SURA  yenye ngozi NZURI kiunyororo.:-(

Nafikiri tumeelewana;

  • Sasa vipi MKUU  leo nini unafikiri umedanganya au UTADANGANYA?
  • Si yasemekana KUDANGANYA ni silaha nzuri ya kutongozea kama  tu KUTISHIA WATU JEHANAMU  kulivyokuwa SILAHA NZURI TU kwa  baadhi ya wahubiri wa DINI fulani fulani hapa DUNIANI?


Na LABDA ni kweli,...
... DANGANYA nyingi wadanganyao hawastukii wanadanganya MTU,...
... ingawa  KUDANGANYA kwingi kuna maandalizi  hata kama MLENGWA bado hajulikani au hajajiingiza tu KICHWAKICHWA.:-(




NI wazo tu hili na nakutakia IJUMAA na WIKIENDI NJEMA BINGWA!:-(
Tuko PAMOJA!


Hebu Monique SEKA abadili  na kuanzisha siku  na wikiendi kwa ndude-Okaman



Au tu Monique SEKA aendelee na -Missounwa


Au tu tena Tshala Muana aingilie kati na -Kalume wee kama NYANI




Au tu Tshala Muana aongeze tu-Tshibola

5 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

emu-three 3:31 pm  

Tupo pamoja mkuu, naona akili zetu leo zilikuwa sambamba, na mimi niliandika kwangu kwa kichwa cha `ahadi ni deni'
Kudanganya ni dalili za mnafiki!

SIMON KITURURU 3:49 pm  

@M# : Si utani ! Nahisi nahisi kulikuwa na usambamba fulani Muu!:-)

Pamoja Sana tu Mkuu!

Candy1 6:45 am  

Nimedanganya kuwa nimelala ila nilikuwa nasoma na kuangalia videos kwa St. Simon usiku kucha...hapo je?

By the way napenda kusikia nyimbo ambazo zimetoka either mimi nilikuwa mtoto mchanga au sijazaliwa kabisa...sijui huwa nazikumbuka vipi hehe!

Upepo Mwanana 2:56 pm  

Candy 1, pole kwa kukosa usingizi ati waangalia movie na kusikiliza nyimbo.
Wanasema maisha huwa hayapotei, ati mtu akidedi, anaibuka kivingine kwa mfumo wa jinsia tofauti na ya awali au kama mnyama aghalabu paka, dogi nk.
Kama unazikumbuka nyimbo ambazo hujawahi kuzisikia, du, jaribu kukumbuka ulizisikia wapi, basi inawezekana uliishi kwa mtindo fulani mahali hapo kabla hujaachia ngazi na kuzaliwa tena!!!!

SIMON KITURURU 6:05 am  

@Candy1: Nahisi kuhusu miziki una tabia kama yangu.Nami napenda kusikia nyimbo zilizotoka wakati mtoto au sijazaliwa kabisa.:-(

@Mtoto mzuri Upepo Mwanana: Mmmmmh!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP