Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Wakati inadaiwa KUNA ya WAKUBWA na kuna ya KUKUA!:-(

>> Thursday, November 25, 2010

Kuna ya KUKUA  yachanganyikayo na mahomoni kufanya MTOTO adhaniye ya WAKUBWA anajua,...

....na kuna ya WAKUBWA ambayo wakubwa wameyapitia maishani na  KUYAJUA.:-(

Swali:
  • Si umeshawahi kukutana na MTOTO ambaye anajiamini kabisa YA WAKUBWA anayajua?

Tatizo ni kwamba,....
..... katika KUKUA,....
... si kila mtu hupitia yote kwa hiyo kwa kuwa NI MKUBWA basi ni kweli yakikubwa yote anayajua.:-(

Swali:
  • Unadhani MTOTO wa mitaani aliyekulia mtaani wa MIAKA TISA ana umri sawa na mtoto wa Rais  KIKWETE mwenye miaka TISA?
  • Si unajua kuna kitu labda toto ndilo LINALOJUA?


Naendelea KUWAZA.....
....ALHAMISI NJEMA  MKULU!


Moja kwa moja twende ARUSHA kupata jiwe la YUZZO liitwalo -DON'T GIVE UP


Tusiondoke ARUSHA kwa..AU tuendelee kuweka kikao hapahapa  ARUSHA nakupata kutoka kwa JCB na Arusha allstars  nyundo-ARUSHA

1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

emu-three 11:21 am  

Ndio mkuu kuna kukua kwa mwili na kukua kwa akili, na hata kama kakulia kwenye capeti la kijani kama wenzetu hawa walisimikwa ulaji karibuni, bado tu atakuwa sawa katika kukua kwake sawa sawa na yule aliyekulia kwenye jamvi. Kwani hata hivyo ukubwa wa pua sio wingi wa makamasi, na nywele nyingi sio akili ingawaje walisema,
Akili ni nywele kila mtu ana zake!
Mhhh mkuu ngoja nisichonge, kwani ukichonga sana, utabakia na bubusu!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP