Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

ASANTE kitabu cha JUMA na ROZA !

>> Friday, June 08, 2012

Baada ya kucheki jinsi Mwanasiasa agombeaye Urais Mexico aitwaye Enrique Pena Nieto akishindwa kukumbuka vitabu vitatu ambavyo vimemsaidia KUTUTUMUA  kuna akili zake a.k.a   vimemuifluensi kunako mtazamo wake,...

.... ghafla nikajistukia kuwa MARA kedekede huwa nasahau kukiri kuwa kuna vitabu huwa naviruka ingawa ndivyo vilivyonipa mwanzo wa kuhusudu vitabu kama sio kusaidia kujenga nijuayo.

Swali:
  • SI umestukia kuwa kirahisi kunatusahau mchango wa shule ya chekechea kisa tu tuna madigrii ya mavyuo?
  • Si kuna tukimbiliao kutaja vitabu tufikiriavyo ni vikubwa kama Biblia na Kuruani ...na kusahau mchango wa vitabu vilivyotufunza A,B,C zituwezeshazo hata kuweza kusoma hayo matabu yaaminikao ni ya KIPROFESA tujivuniayo?

Ndio,...
.... nawaza tu kwa SAUTI!


Hebu Lágbájá aingilie kati kwa - Bling Bling Panda

 Au tu Lágbájá azime tena kwa - Sobolation

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 10:32 am  

Juma na Roza yaaani mtakatifu umenikumbusha mbali kwelikweli. Juma anasema kimbia ngómbe kimbia upesi...Ahsante nitakitafuta hiki kitabu. Ijumaa njema:-)

o'Wambura Ng'wanambiti! 8:51 am  

Kuna hata wadhanio kuwa mupenzi wa sasa ni bomba kuliko yule alomtoa Bikira :-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP