Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Maana ya KITU!

>> Monday, June 04, 2012

Tatizo ni kuwa labda YAONEKANAYO ni ya MAANA,....
.... yametafutiwa UMAANA na BINADAMU kibinadamu tu,....
.... kitu kifanyacho LABDA ya MAANA mengi  kwa BINADAMU MMOJA  wala hayana MAANA kwa wengine.

Swali:
  • Kwani kuna la MAANA kwa BINADAMU lisilosingiziwa UMAANA kwa udhaifu wa KIBINADAMU tu?

Ila labda la MAANA,....
.... ni la MAANA kwako tu,....
...... na usipoangalia labda ufanyacho ni kuambukiza tu wengine MTAZAMO ili kwako la MAANA liwe  pia na MAANA kiumaana na kwa WENGINE!:-(

Swali:
  • AU?

Ndio,...
.... labda MITAZAMO tu ijengwayo katika JAMII inachangia TAFSIRI zifanyacho kuna yasiyo na MAANA binadamu kuyaona ya MAANA sana,....
... na wala hapa siongelei tu NGUO, ulabu, au hata DINI hata zisizo  za WACHAWI ambao kwao WALIONAZO  na jamii yao ya wachawi ,....
.... KWAO hata uchawi huleta MAANA!:-(

Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!:-(
Nakutakia JUMATATU NJEMA!:-)


Hebu Asathecomic aingilie na kubadili kwa kuongelea-Women HATE When Guys...
Tuendelee kusikiliza ya -Black men hate single women/mothers because........
Au tu NINA SIMONE aingilie kati kwa - My baby just cares for me

 Nina Simone aongezee - Ain't Got No...I've Got LifeAu tu azime kwa her live recording of her Civil Rights Anthem -To be Young Gifted and Black

1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 1:37 pm  

Pia kuna watu wanaona mtu fulani ni wamaana sana kwake lakini sio lazima wote waone hilo....Kwa mfano mimi naweza nikasema "Kadoda ni mtu wa maana sana kwangu " huu ni mtazamo wangu...

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP