Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Jana - Perdido. AU?

>> Wednesday, January 31, 2007


Sasa ngoja niachie picha kwanza....




Mhhhhh!!..



Kenya, Tanzania ,Kenya




Heidi na Mimi






Mimi na Erick






Wax na mimi






Au ngoja Billy Taylor, Duke Ellington na Willie the lion waseme hivi....

Tuendelee....




China na Tanzania



Mernard na mimi





T.I na mimi







Rasta na sio rasta






Lakini unawakumbuka Musical Youth?!.....




Raymond aka Mkuu waKikao na T.I




Chriss(T.I)na RaPPEr(Ghana)




Kenya na Tanzania






Du lakini lini Tanzania tutakuwa na waziri kama huyu Gilberto Gil






Tanzania na Somalia






Wasanii Babu K-Mernad na Aliko




Heidi








HUYU NANI?.....






























Samahani, ngojea nikuache na King Sunny Ade akudondoshee Synchro System

Read more...

Mungu Awalaze mahali pema peponi!

>> Monday, January 29, 2007



Hivi kwanini walazwe? Hivi peponi si sehemu ambayo mambo mengine yanaweza kufanyika?

Read more...

WACHAWI WA TANZANIA MKO WAPI?

>> Saturday, January 27, 2007


Hivi hakuna kanjia kakuuweka uchawi wenu ukawa unatusaidia wote
katika dunia ya sasa?

Je, haiwezekani kuwaloga wamagharibi wakatuletea teknolojia , halafu wakasahau tukaacha kuwalipa?

Mvua je?Wakati wa ukame mbona hamzileti?


Ningependa uchawi utusaidie kusafirisha vyakula nchini kuwafikia wenye njaa kwa kutumia Air Ungo. Ningependa mngesaidia kusafirisha Watanzania kwenda kwenye shule na vyuo babu kubwa vyote, halafu wasome bure bila kuonekana.
Ningependa mgundue kondomu zisizo onekana. Wavalishwe wote wenye mdudu.
Watembee wamezivaa bila kujua.

Mambo yenu ya kutishana nayaona ni nishai!
Mambo yenu ya kurudishana nyuma nayaona ni nishai!
SASA HIVI, NYIE WASHIKAJI MNAFIKIRIA NINI?

HIVI HIYO SAYANSI YENU NI LAZIMA IBAKIE HIVYOHIVYO KARNE ZOTE?

Nauliza tu!
Msiniloge!



Hebu nimwache Jimi Hendrix aachie VOODOO CHILD

Read more...

Kipenda Roho!


Juisi ya ukwaju

kwa uji wa ulezi

Macho gololi

Mashavu maandazi

Wanichoma kibiongo

kwa maungo ya ufukweni

Najilamba kwa auheni

busara uvunguni

Nyama ya mchicha

firigisi kiwanja mshikeni

Dirisha la burudani

Ubongo ndotoni

Mahaba kijiweni

Sina nguvu!
27/01/07




Au Tracy Chapman anasemaje?

Read more...

Masikini Jichoni mwako!


Hivi wewe kama Muafrika , unamuonea nani zaidi huruma?
Maskini wa kizungu au Wakiafrika?
Ukiwa na shilingi moja utampa nani?

Usitishike, najua wewe si mbaguzi!

Vipi unafikiria nini ukiona maskini hawa wa Marekani? Je, ni maskini kwako?

Read more...

Hivi Mambo ni YaleYale tu! Unaweza kujinasua kutoka katika mduara?

>> Friday, January 26, 2007


Nimesikia watu wengi wakisema kuwa kiini cha matatizo mengi kuendelea kuwepo ni kwasababu watu hawajifunzi kutoka kwenye historia.Ninakubaliana na hilo. Ukianzia kwenye umaskini, matatizo ya rushwa, uongozi ovyo, na mengineyo ,yanajirudiarudia tu kila kukicha kutokana na kutojifunza.Ukichora umbo la mrudiano utapata mduara. Lakini pamoja na wengi kuamini hivyo, hii haina maana kuwa haiwezekani kuvunja mduara wa kurudiarudia makosa. Ila katika swala la kuvunja mduara huu kunatakiwa fikira safi, dhamira na wadau kujua wanafanya nini na tatizo liko wapi.

Nilipingana na baadhi ya watu waliokuwa wanadai CCM sasa ishavunja wapinzani na hivyo hakuna litakalo badilika.Walidai kuwa mduara wa uzembe ushaanza kuingia katika mzunguko wa pili chini ya CCM.Na walidai kuwa mzunguko huu hautakwisha , kamwe. Nilipinga wazo hilo kwa sababu kubwa moja. Naamini kila siku hutoa nafasi mpya ya kubadili mwelekeo. Kila siku hutoa shule kwa wakereketwa , kwa watu wengine ambao wanaweza kubadili mambo. Naamini kila siku inatoa mwanya wa wapinzani kujijenga tena.
Kuna kipindi nilikuwa nafananisha utawala wa CCM na utawala wa kifalme wa Uingereza. Ingawa ni vigumu kufananisha historia ya nchi mbili hizi, bado nilipata mwanya wa kustukia ni jinsi gani hata mzunguko wa siasa za Uingereza uliweza kubadilishwa kutoka katika ule wa mfalme kuwa na nguvu zote mpaka wa leo ambao mfalme/malkia yuko kama simbo tu.Na baada ya Waingereza kuvunja mduara haujarudia tena.Hivyo naamini CCM pamoja na mabavu sasa , hainamaana kuwa haita banwa.Na CCM kuwapo na nguvu sana katika nchi kuliko vyama vingine ni mapungufu na sio jambo bora kwa Taifa.

Kwa Uingereza walitokea akina Oliver Cromwell ambao kwa kasheshe zao waliweza kuisababisha Uingereza kuwa republic kwa kujaza zaidi nguvu kwa watu na kuzitoa kwa mfalme. Na naamini kama CCM itafikia kujisahau kwa sababu ya kukosa upinzani wa maana , watatokea akina Oliver Cromwell wa Tanzania ambao watasitisha Utawala utawaliwao na CCM na kuleta uwezo kwa watu na bunge ambalo lina uhai na nguvu ya kupinga, kusawazisha na kuelekeza taifa la Tanzania wananchi watakako.


Swali:

Tunapozungumzia kuwa huu mduara(vicious circle) hauvunjiki tunamaanisha nini?

Wengi wetu tukiwa tunaongelea mduara wa mapungufu , tunatumia mifano kama;masikini huzaa maskini , na kupata vitukuuu maskini na kuendelea.Afrika inazalisha viongozi hovyo ambao hurisisha wengine ovyo na mpaka karne ijayo itakuwa ovyo.Tunasema hivyo kwa kuamini kuwa hakuna kitakacho badilika. Tunasema hivyo kwa sababu tumekata tamaa.

Swali:
Je, tunasahau ni mambo mangapi tumeyabadili Afrika ambayo hayawezi kurudia?

Je, tunasahau kuwa ni mambo mengi tu hata katika udongo /ardhi tuikanyagayo tushayatendea mambo ambayo haiwezekani kurudisha katika hali iliyo kuwepo zamani?

Tukijaribu kujikumbusha mambo madogo madogo, naweza kusema siamini kama uchifu utarudia hali yake ya zamani Tanzania. Naamini hata ukabila hauwezi kurudia hali yake ya zamani.Na mambo mengine mengi tu. Sasa kama imewezekana kwa Watanzania kuvunja kwa kiasi kikubwa baadhi ya mambo na ni vigumu kuona kuwa yatarudia tena, naamini mambo mengine mengi zaidi yanaweza kuvunjwa yasirudie.Kama Tanzania tumeweza kuifanya kiswahili lugha ya taifa basi tunaweza kuondoa rushwa kama tabia ya taifa.

Tatizo ambalo ni la kibinadamu niliogopalo nikusahau yaliyopita . Desmond Tutu amelisema kuwa waafrika kusini sasa hivi wanapoteza mwelekeo. Wanapoteza njia ya wapi wanakwenda.Ukifikiria jinsi walivyokuwa wanapigania kujitawala juzi juzi , nivigumu kuamini wanaweza kujisahau mapema namna hii.

Lakini utashangaa ikiwa baada ya karne kadhaa Watanzania nao wakawa wamesahau mpaka kiswahili? Inaweza kuonekana kama ni hoja ya ajabu isiyowezekana, ila bila mikakati kupoteza mwelekeo kupo. Na hili ni jambo ambalo ningependa Watanzania tuwetunahakikisha hatulisahau.DUh !Nimemkumbuka huyu Askofu Tutu. Ngojea nimuachie Miles Davis anisaidie kumenzi hapa kwa kibao TUTU


Tukiongelea rushwa. Naamini kabisa rushwa tuliyokuwa nayo leo hii ni ya kiasi ambacho hakijawahi kuwepo katika historia ya Watanzania. Hivyo sioni haja ya kuacha kuipiga vita kwa kisingizio kuwa itajirudia tu. Pia naamini kila tatizo laweza kutafutiwa dawa yake ya kienyeji. Kila tatizo ni changamoto ya jawabu. Tatizo la Tanzania linaweza likapatiwa dawa ya Kitanzania.Si lazima kila wakati tutumie dawa kutoka nje.



Swali:
Lakini kwanini ni rahisi kujikuta uko ndani ya mduara bila njia ya kutokea?.

Je , ukizaliwa masikini maana yake utafariki masikini pamoja na vizazi vyako vyote?


Jibu ni ;sio ukweli.

Sasa inakuwaje kuwa walio wengi tuliotokea katika familia masikini tunaendelea kuwa masikini?

Nafikiri jibu liko kwenye ukweli kuwa binadamu pamoja na janja yake anahitaji msaada. Anahitaji mfumo wa kumsaidia ilikuweza kupiga baadhi ya hatua.Binadamu ni kiumbe ambaye daima huhitaji msaada. Mfumo unaoweka dunia katika hali iliyopo sasa hivi husaidia wenyenavyo kuongezewa na wasionavyo kuporwa hata walivyo navyo wasipo angalia. Ingawaje inasemekana hili ni jambo lililozungumziwa hata kwenye biblia, mimi siamini hivyo. Mimi naamini kuwa kila hatua au msingi mtu aupigao ni msingi umuwezeshao kupiga ile hatua moja zaidi(extra step/mile) ambayo haionekani kirahisi. Kwa matajiri ni rahisi kupiga hatua ile moja zaidi kutokana na mfumo uwalindao. Kwa maskini hata kama unawazo fulani huanzii kwenye mstari mmoja na matajiri. Ukienda benki, wewe ni rahisi kukosa mkopo wakati tajiri ambaye haitaji mkopo ndio akapewa mkopo. Ukienda kuomba kazi ni hivyo hivyo. Lakini mimi navyojua ni kwamba, matajiri hujisahau, na pia hufikia wakati ambapo wanakosa moyo wa kuendelea kujiimarisha. . Maskini kwa kujijenga taratibu hufika. Hatua kwa hatua tutafika kama tunakumbuka tunako toka. Msingi utazidi kuimarika kama tunajua kuwa huu ni msingi utuwezeshao kuhimili na kutusaidia kujijengea mfumo ambao utatusaidia kukata mduara dhaifu na kuendelea mbele.
Tusaidiane kufanya vizuri tuwezavyo, au kama FEMI KUTI akwambiavyo, DO UR BEST

Read more...

Lakini Unakumbuka?

>> Thursday, January 25, 2007


Namuachia Bunny Wailer.
Msikilize....

Read more...

Duh!

Unajua unachokifikiria sasa hivi, inawezekana baada ya dakika tano ukawa umekisahau?
Halafu unajua inaweza ikawa ndio ilikuwa jibu la maswali yako, matatizo yako?

Usiniamini!


Niko mawazoni tu!



Lakini...!!

Read more...

Kung'ong'a!


kukenua meno!......
Kukenua mdomo!.....
Kununa.....
Kuonyesha chuki!...
kujidai unanionesha chuki!

Kunizalilisha...!
Nikuzalilishavyo!...

Kwanini?
Kwanini unipigi?
Nikupige eeeh!
............

Hivi nitafaidika au utafaidika?
Au ?
....!!!!!
?????


Unanichukia?

Read more...

Ashki


Kutaka...
Kutakwa.....
kuwania....
Kupewa....
kumpa...-.
Kumfurahisha.....
kujifurahisha...
kumwania...
kuwaniwa...
kutafunwa ....
kumtafuna....
Yote yanaweza kutokana na ashki!........mdadi.....genye....!

Inawezekana ni ashki imeniponza!...
Inawezekana imekuponza!....
inawezekana ....

Ashki!
MmmmHhhhh!

Read more...

Kama ningerudisha muda nyuma....

>> Wednesday, January 24, 2007


Je, ningeanza upya?

Ningekuwa mtu wa namna gani?

WEWE JE?

Bahati mbaya au nzuri, ndio imetoka hiyo!

Read more...

Nyama Ya Bata ni Tamu, lakini......

>> Tuesday, January 23, 2007



Watu husema kuwa ukifuatilia nyendo za bata ,ni vigumu kula nyama yake. Vilevile inasemekana ukijua nyuki anatumia viungo gani kukamilisha utamu wa asali, unaweza kuona kinyaa kujilamba.

Swali:
Lakini hivi unafikiria ni kwanini huoanishi mbogamboga zilizo mea wakati ziko pale jikoni na uozo wa mbolea, mboga hizo zilipofyoza rutuba?

Sawa labda wewe unatumia mbolea za chumvichuvi na makemikali mengine ya stawishayo mboga.

Je, mbona huoanishi makemikali na kinyaa au sumu ziwezazo kukuathiri wakati unapata shibe?

Binadamu ni mtu ambaye anaweza kubadilishwa mawazo. Binadamu kwa bahati mbaya anaweza akapandikizwa imani na mawazo hata yeye bila kujijua.Kikubwa pia ni kwamba binadamu tunaunganisha mambo kipicha. Na mara nyingi si ukweli yale mambo tufikiayo hatima ya akili ya common sense, kutokana na picha tuziungazo kutokana na fikira tu zisizo na uthibitisho. Siamini kwamba kula nyama ya bata ni uchafu kwa sababu tu imeaminika kuwa anakula uchafu. Siamini asali ni chafu kwa sababu sijui nyuki alitoa wapi siri ya asali utamu kunoga.

Nachojua ni kwamba kama sisi tumeumbwa kutoka kwenye udongo na tukifa tunarudi kwenye udongo, basi tulapo mimea inayofyonza udongo kwenye kupata shibe, maana yake sisi ni wala watu.Au?

Dondoo:
Ushasikia jinsi Nguruwe apigwavyo vita?Je, ushasikia jinsi ng'ombe apigwavyo vita?Je , unakumbuka kuwa konokono asemekana safi sana na popo kunasehemu wanawala bila kuwapika?Nachojaribu kusema ni kuwa kila jamii si lazima isimzimie samaki nchanga.


Kumtengenezea picha nzuri binadamu katika mawazo ni moja ya siri na kazi makampuni karibu yote duniani yanafanya. Utakuta huyu atakwambia haya maji ya chupa ni Perrier, hii chupi ni Gucchi iliakutengenezee katika mawazo kuwa ni ya thamani zaidi kuliko nyingine. Lakini mwingine atakudaka kwa kukustua kua achana na gucchi na malebo mengine hayana thamani yoyote zaidi nunua yangu ya bei chini isiyo na lebo. Huyu atangazae kutokuwa na lebo na atangazaye lebo wote wanacheza mchezo mmoja wa kukudaka . Wote wako katika mchezo wa kuuza na hawawezi kuuza kama hawajakudaka.Cha muhimu ni kwamba je, wanacheza mcho wa kihalali katika kukujenga kimawazo?Wamarekani wanaimba tokea utoto nchi yao ndio bora kuliko zote. Wauza madoli na mpaka sigara ilikuwa kawaida kabisa , kama sio kawaida kabisa kulenga watu tokea watoto. Kuwaanda kimawazo kujua nini wazinguke nacho.

Sasa nini:

Mimi kama Mtanzania ningependa Tanzania kama nyama ya bata ijulikane kuwa ni tamu.

Sasa kwanini Tanzania haijulikani?

Tanzania tutake tusitake haijulikani kama inavyo stahili.Tanzania ni nchi yenye mambo mengi.Ni nchi inayopendeza. Lakini bado watu wanafikiri mlima Kilimanjaro uko Kenya.Halafu jiulize tu kama kitu kilichowazi kama mlima Kilimanjaro hakijulikani kiko Tanzania ni nini kinajulikana basi. Nasikitika kwamba ukiwauliza watu wengi duniani, cha kwanza watakachosema ni magonjwa au njaa.

Kwa nini Kenya inajulikana kuliko Tanzania?

Naweza sema ni kutokana na kuwa katika mfumo wa kibepari muda mrefu ukihusisha mbinu za kisoko za kibepari tokea zamani.Mbinu hizo ikiwa ni kujitangaza kwa namna ya kulenga pato. Mbinu zake ni nyingi lakini moja isaidiayo Kenya ni michezo.Kwa mfano hakuna mashindano ya mbio yenye kusifika ambayo watataka kuyaendesha bila kuwa na timu ya Kenya na Ethiopia. Kwa sababu hakuna atayeshinda atakayeaminika kashinda kikweli bila ya timu ya Kenya kushiriki mbio za masafa marefu. Ni sawa na mtu ashinde mbio za masafa mafupi kama mita 100 bila ya kuwa na washindani kutoka Marekani.Likifanyika hilo, ushindi wako hautathaminika.

Lakini ukimsoma Naomi Klein katika kitabu chake cha NO LOGO
utakubaliana naye mambo mengi kuhusu matumizi mabaya ya lebo. Lakini mimi nafikiri kuwa Tanzania, Afrika hata matombo kama jina lituwakilishalo linahitaji kung'arishwa.
Tanzania kama nchi naamini inastahili jina zuri .Na ni lebo (brand)tujihusishayo nayo tutaketusitake.

Bahati mbaya vyombo vingi vya taaluma kuanzi shule , dini hata maongezi yako na yule yanapanda mbegu zakutojiamini kuwa kifuambele kama Waafrika, Watanzania nk.Naamini watu weusi tuna kazi ya kungoa mimea yakutojiamini na ya kujipenda.Pale ambapo vyombo vya wenzetu vinapozidi kutuhusisha na njaa na magonjwa, ni sisi tunaohitajika kuweka sura mpya ya ukweli, kujenga sura mpya ya taifa litakalo tufanya tujivunie.

Nashukuru siku hizi ni kawaida kuona watu wamevaa mashati ya Tanzania.Kwa maana ilikuwa si muda mrefu watu wengi waliona ni ujanja kuvaa bendera za nchi nyingine kama Marekani na Uingereza. Na kwa baadhi ya niliowahi kuwauliza walisema kuvaa ya bongo ni nishai.Ingawa kuna ukweli kuwa yalikuwa haya patikani sana si kipindi kirefu kilicho pita.

Baada ya yote haya nakubali Tanzania tunamatatizo mengi. Lakini Marekani , Uingereza na Saudi Arabia wanayo pia. Sasa kwanini sisi tu ndio tukubali mpaka ambayo hatustahili. Kama ujinga, sisi si wajinga.

Lakini hivi kama Tanzania ni bata , nyama yake ni tamu?

Business in Tanzania

Read more...

Mchango wangu na wewe kwenye habari za dunia yetu ya kiungwana iongozwayo na George Bush

Ukitazama televisheni au hata kusoma magazeti ni mara nyingi kukuta habari mbaya ndio zimetawala. Ni rahisi kulalamikia vyombo vya habari lakini ukweli ni kwamba vyombo vya habari mara nyingine navyo huandaa mambo yake kutokana na kuijua saikolojia ya wasomaji wake.Naamini kuwa vyombo vya habari vinanguvu ya kuchonga mitazamo ya waletewa habari, lakini naamini pia vyombo hivi pia vinaweza kubadilishwa kutokana na wateja wake kubadili msimamo na mitazamo yao kuhusu habari wapashwazo. Kwa ujumla hali ya dunia ni matokeo ya nini binadamu wanafikiria na wanavyotenda. Cha kusikitisha ni kwamba, sura ya dunia leo hii inatokana na binadamu asivyofikiria.

Vitu tuvipavyo kipaumbele mara nyingi hata bila kufikiria ndio vichongavyo hali halisi ionekanayo.

Naamini shida na raha lazima vitakuwepo hapa duniani kwasababu shida huhitaji raha na raha huhitaji shida ilikuonyesha utamu wake. Lakini halihalisi ambayo inafanya wengine wasaze na wengine wakose kabisa haikubaliki. Kuna mambo mengi ni rahisi mtu kujitoa kuwa yako nje ya uwezo wake.lakini kila mtu akifanya machache aliyonauwezo kupeleka muelekeo wa mambo akupendako inasaidia sana.

Naamini habari mbaya zitakuwepo , lakini je, ni lazima ziwe zina tawala kwenye vyombo vya habari za dunia?Na sivitendo vyetu visababishavyo baadhi ya habari hizi?


Kila kukicha, vita huku, majambazi kule, magonjwa , njaa na kadhalika.

Inawezekana tunasahau kamchango ketu kamabaya au tunasahau kuchangia mazuri kutokana na kubanwa na mambo kibao.Mambo kibao mengine tuyaitayo maisha magumu.Lakini mimi naamini mchango mwingine si lazima uwe kama wa Mandela katika Afrika. Mimi naamini lolote jema linawezakuwa mchango kama mtu atalifanya.

Mfano unaweza kumonyesha pendo mtu na kumfanya afurahi?Aliyefurahi naye ni rahisi kumfurahisha mwingine. Kwa hilo tu watu kadhaa watakuwa wamepitisha wakati kwa furaha.

Duh , lakini ushawahikupenda kitu mpaka ukalazwa kwenye hospitali ya wagonjwa waakili kama Alpha Blondy asemavyo hapa...


Kuna viongozi fulani mimi naona wanachangia sana duniani tuwe na habari mbaya.
Nikiulizwa kwa nini viongozi wengi duniani huwa hawapendi kuachia uongozi naweza kushindwa kuwa na jibu.Nashindwa kumuelewa kabisa huyu Mzee Lansana Conté. Huyu Mzee ni mgonjwa na amekuwa katika uongozi tokea mwaka 84. Hivi ndio tuseme hakuna mwingine ambaye ataweza kuongoza nchi?.Huyu Mzee habari zake na mambo yake yametawala sana wiki hii. Na sioni ni kwa sababu gani anatoa mchango huu. Viongozi wengine kama akina Museveni mimi nashindwa kuelewa kwanini wawetu madarakani. Kwa maana unakuta kiongozi anapitiliza mpaka kuondoa hata yale mazuri aliyochangia kwa sababu tu awe kiongozi.

ukiongelea wachangia habari mbaya si viongozi wa Afrika tu. Ukianza kuwaongelea wakina George Bush, ndio basi tena. Chaajabu yeye ndio anayesemekana kuwa ni kiongozi wa dunia ya kiungwana(civilized world).

Naogopa kukiri kuwa tusipokuwa waangalifu au kama si waangalifu, ni mimi na wewe tunaoweza kuwa kiini cha habari mbovu kutawala dunia. Tusisahau kuwa ni mimi na wewe miongoni mwa waijazao dunia hii kimawazo na hata ki-kabon daioxaidi.
Watu wengi husema ni ndoto kuondoa matatizo duniani. Mimi nasema haiwezekani kuondoa matatizo duniani. Lakini ni matatizo, shida na madhara mengi duniani ambayo hakuna haja ya hayo kuwepo. Haya ambayo yapo kutokana na kuchangiwa na sisi binadamu kutokana na mitazamo yetu potofu na kufikiri kwetu au kutokufikiri kwetu yatutesayo au yatesayo wengine ambayo yanakwepeka, yanatibika ,hayastahili kuwepo. Ni vizuri tukijaribu kukumbuka hili.

Hivi ingekuwaje dunia ingekuwa kama John Lennon alivyoimba katika wimbo imagine?....


Read more...

Jana-Feelin Irie!

>> Saturday, January 20, 2007


Duh , kumbe sio sama taim!Hivi Mwandani huko ni sama eeh?


Mimi na T.I

















Mimi na Chacha







Mimi na Biyamungu







...na Mimi






Mimi na......









Lakini hivi....




Johan na Raymond aka Mkuu wa kikao




Deo







T.I na Biyamungu









Kenya na Tanzania




Martin, Allen na Biyamungu






Lakini bado.......

Read more...

Malcom X akifufuka leo!

>> Friday, January 19, 2007



Katika safari ya Malcom X iliyomleta mpaka Afrika , alikuwa anataka kujifunza imekuwaje waafrika ndani ya Afrika wamejikomboa haraka kuliko Wamarekani weusi. Katika moja ya jambo ambalo alikuwa anaona Waafrika wamepiga hatua ni hili la kuanzisha umoja wa nchi za Afrika. Alikuwa anatumia hoja hiyo hata kujaribu kuunganisha Wamarekani weusi au msikilize kwanza........


OAU ingawa imesifiwa na Koffi Annan kuwa imeleta umoja wa Afrika , mimi siamini katika hilo.

Hivi umoja wa Afrika tuuzungumziao uko wapi?

Ikiwa Tanzania na Kenya kuwa na umoja ni kasheshe hivi kweli tunaweza kusema OAU ilileta umoja wa Afrika? Hivi si ndio OAU hii hii ambayo iliongozwa na akina General Gnassingbé Eyadéma , Mobutu Sese Seko Nkuku Ngbendu wa za Banga , Mohamed Siad Barre, ambaye alikuwa anajulikana kutaka kuichukua Jibuti ,ogaden na hata sehemu za Kenya akiamini kuwa Somali kubwa ni zaidi ya mambo mengine? Je , si na Idi Amini naye alishika hatamu wakati anajulikana mambo yake kwenye OAU hii hii?

Swali:
Hivi inawezekanaje chombo kitarajiwacho kuelekea kulia kikawa kinaendeshwa na dereva mwenye nia yakwenda na aelekeaye kushoto?

Sasa labda nimechanganya mambo kuhusu hii OAU, nasikia siku hizi tuna AU.
Lakini nasikia pia hii AU inataka kumpa kiti cha kushika hatamu Raisi wa Sudani, Field Marshal Omar Hasan Ahmad al-Bashir .

Dondoo:
Hivi unajua kuwa Sudani inatambulika kama ndio nchi ya Kiarabu kubwa kuliko zote kieneo?

Sasa kama ni kweli , huyu raisi wa Sudan si ndio yule yule anayewabagua baadhi ya Wasudani ndani ya nchi yake? Hivi kweli hii AU itafikia siku moja ikawa na meno ya kutatua matatizo ya Afrika?

Hivi Malcom X akifufuka leo atauonaje muungano wa Afrika?

Sawa, labda ni kweli mwanzo mgumu! Lakini hivi kipimo cha mwanzo ni kipi? Mwaka, miaka, mlongo,au karne?

Read more...

Nani mbaguzi zaidi?


*Watu weupe au weusi?

Duh, nilisahau kuwa katika makundi mengine Ndesanjo ni mweupe.
Sijui Marekani wanajua hilo?

*Wazungu au Waasia?


Duh, hivi kumbe Wachina na Wahindi wote ni Waasia!

*Wakristo au Waislamu?
Hivi kumbe Waothodox , Wakatoloki na Wasabato wote ni wakristo!
Hivi kanisa lipi linapeleka watu mbinguni?

Hivi kumbe Washia na Wasunni wote waislamu!

*Wachaga au Wapare?

Duh, nilisahau kuwa kuna ubaguzi ambao uko na umejijenga pia ndani ya makabila yenyewe bila kwenda nje ya kabila!

*Wewe au Mimi?
HIVI KWANINI HATUFURAHII TOFAUTI ZETU?

KWANINI TWAZITUMIA SANA KUTUTENGANISHA BADALA YAKUTUUNGANISHA?

Hivi ni kwasababu ya uoga tu, au ndio kwamba ubaguzi uko ndani ya chembe zituundazo zilizojengwa kuhimili uwepo wetu hapa duniani?

Hivi tunajifunza kweli? Au ndio siku moja hapa duniani itakuwa ni watu weusi wanakandamiza watu wa rangi nyingine?

Hivi watu wote wakiwa sawa , nchi zote hazina tofauti, kila kitu sawa , itakuwa bomba?

Wewe unafikiria nini kuhusu hili?

Read more...

Hivi Masista wao hawataki ku..........!

>> Thursday, January 18, 2007



Siku hizi ni kawaida kusikia mapadri na maaskofu wakitaka waruhusiwe kuoa. Hivi mbona sisikii masista wakitaka ku......!

Napenda GADO awakilishavyo jambo hili.

Read more...

Unapenda kula mate eeh?


Unalikumbuka busu la Yuda Iskarioti?

Nilikuwa na jaribu kuelewa historia ya busu kwa kipindi kirefu kidogo. Hii ni baada yakuanza kujiuliza hivi ni kwanini watu wanapigana mabusu. Pia baada yakuona mabusu ya kila aina. Mabusu ambayo mara nyingi hunichanganya akili ni yale nionayo Viongozi wa siasa wakipigana mbele ya kamera ilikuashiria salamu ,uelewano.....nk.

Ukifuatilia kuna mambo mengi yanayo ashiria hii tabia binadamu walijifunza tu. Katika kufuatilia ndio nikaja kugundua kuwa kumbe kuna watu wamesomea mpaka udakitari katika kuchunguza busu.Nikaja kugungua kuna somo la philematology ambalo ndio likufanyalo ubobee katika stadi za denda.

Inasemekana inawezekana kabisa kuwa binadamu wamejifunza tabia hii kutoka kwa wanyama wengine. Kama ni kweli, mimi siwezi kushangaa kwa maana ukishuhudia mambo ya fanywayo na binadamu wapiganao busu unaweza kustukia mengi tu niya kinyama.

Lakini ni binadamu pekee ambaye amelipa busu sura na maana nyingi. Utasikia Waeskimo wanapigana busu kwa kugusanisha pua ilikuashiria salamu. Wafaransa wanakupa hili busu la kifaransa, mara nyingi kuashiria pendo kwa wapendanao, ambao wanapeana ruhusa yakunyonyana ndimi, ruhusa ambayo inaweza kuambatana na ruksa nyingine za miingiliano. Kuna busu takatifu ambalo lilizoeleka makanisani na kadhalika. Utasikia kuwa Yuda Iskarioti alimpiga busu Yesu ilikumsaliti. Utasikia mwingine kapigwa busu ilikuzalilishwa. Vilevile nafikiri uliwahi kuona Kofi Annan akimpiga busu Arafat katika kuashiria salamu.Lakini busu maarufu ni la wapendanao. Ukiwakuta wapendanao wakilana denda mwenyewe utakoma na jinsi waonyeshavyo kusikia utamu.

Katika haya yote mabusu mimi naliogopa zaidi hili busu la Yuda Iskarioti, busu la usaliti.

Dondoo:
Lakini unakumbuka kuwa mdomo unasemekana kuwa una bakteria wengi kuliko hata sehemu za siri?


Inasemekana zamani Afrika ,hasa sehemu za chini ya jangwa la sahara hatukuwa na tamaduni za mabusu(hapa naongelea denda la kimapenzi).

Inasemekana mara ya kwanza Waafrika Afrika Kusini walipoona wazungu wanakulana denda walidai hii si poa ni uchafu .

Look at these people! They suck each other! They eat each other's saliva and dirt! — Tsonga people of southern Africa on the European practice of kissing, 1927

Lakini naamini ukienda sasa sehemu hiyo hiyo jambo hili litakuwa ni la kawaida.

Inawezekana kuwa kusalitiana kulikuwepo , lakini ukweli ni kwamba kupo. Sasa mimi naona hata busu la usaliti limeota mizizi.

Inashangaza jinsi binadamu tunavyojifunza kirahisi kuzoe mambo.

Sijui sana historia ya busu Tanzania . Nachojua denda linanguvu Tanzania. Watu wanakuladenda la nguvu.Lakini linanisikitisha kuwa denda la usaliti halichukuliwi umaanani na wala halionekani.

Swali:
Hivi sisi Tanzania ndio tungekuwa tumeendelea, matajiri, na wenye uwezo unafikiri tungekuwa tunatoa busu gani?

Mimi natishika sana na jinsi sisi tunavyozoea mabusu haya ya kutusaliti. Natishika na jinsi kwa kisingizio cha diplomasia viongozi wetu wamebobea katika mabusu ya usaliti,busu la Yuda Iskarioti.

Nasikitika kuwa wengine tunazoea hata kudanganywa, shida, ...nk kwa kisingizio kuwahiyo ndiyo hali halisi.


Unapenda denda eeh?
Ngojea niwaachie Ladysmith Black Mambazo wakuletee wimbo ...

Read more...

Tufanye tu kwa vitendo!

Kuna mambo mengi sisi binadamu
tuyaongeleayo,
tuyalaamikiayo,
tuyapendayo ,
tuyachukiayo,
tuyatamaniyo,
tuyaombeayo,
tuyaviziayo,
tuyasengenyayo,
tuyachombezayo,
tuyakanayo .......... tutakayo kuyaacha.................nk

Kuna mambo mengi tujuayo kabisa kuwa ndio jibu la maswali
tujiulizayo,
ndio jawabu ya matatizo tuliyonayo,
ndio tuyatakayo,
ndio ukweli, ndio busara,..............

Cha ajabu pamoja nakujua yote hayo , haya mambo hata sikumoja hatuchukui hatua kuyafanya , kwa vitendo, hatuyatekelezi kutokana na ukweli hatuanzi kupiga ile hatua ambayo ni ya utekeleza tu.

Inasemekana asilimia kubwa ya watu kabla hawajafa hujutia yale ambayo walikuwa nauwezo wa
kuyatenda,
kuyafurahia,
kuyajaribu..........
halafu hawakuchukua hatua walizojua kuwa zitatimiza matakwa hayo, kwa kifupi hawakuyatenda.
Asilimia kubwa yetu tunaogopa kufanya makosa, hivyo tunajichunga kuchukua hatua kwa kuogopa tusije tukajuta. Chakufurahisha ni kwamba kutokana na kujichunga na kutochukua hatua ni ukweli hatufanyi makosa , hatukosei lakini pia hakuna litendekalo, hivyo hatupati tuyatakayo.

Swali:
Hivi sisi kama binadamu, tunaweza kweli kukwepa kukosea?
Hivi ni busara kutotimiza matakwa yetu kwa sababu ,labda tutachekwa,au kwa kuhisi tu haiwezekani?

Basi kama nikutafuta shule , tuzitafute
kama ni kazi , tuende kuzitafuta
Kama ni kuandika kitabu, siri ni kuanza kuandika tu.

Kama ni kumueleza Zubeda kuwa unampenda basi tufanye hivyo
Tuanze kufanya na........,tutekeleze..........., tuombe msamaha kwa......., na tu..........

Au ngojea niseme...


Ukweli ni kwamba bila kuchukua hatua mpaka milele hakuna kitakacho fanyika!
Sijui unanielewa?

Tukumbushane kuchukua hatua na kutekeleza.Tuamue na tutekeleze.

Mimi naamini inawezekana.Tujaribu ,halafu tujaribu tena na tena na tena.......
Kama ni kweli ndicho,ndilo,....tutakalo, takacho....tutafurahia matokeo, tutajua utamu wake, tutaendelea.

Read more...

Nina Ndoto!-Martin Luther King Jr

>> Monday, January 15, 2007

Inasikitisha kuwa tokea Martin Luther King Jr afariki mpaka leo hii siku rasmi ya kumkumbuka, hali haijabadilika sana.Sina cha zaidi ya kumuachia mwenyewe aelezee ndoto yake......


Kazi bado tunayo!
Lakini ninafaraja moyoni kwasababu naamini kuna vijana wengi weusi na wakiafrika ambao wanauwezo wakuendeleza kazi hii aliyoiacha Martin Luther King Jr, wapo.
Ingawa watu wengi huwa wanaiunganisha ndoto yake na Wamarekani weusi tu, wanaiunganisha na Marekani pekee, lakini tatizo alilokuwa analipigania linaunganisha haki za watu wote weusi.

Mimi na Nina Simone tunaamini vijana weusi wenye uwezo wapo, tupo.
Au Nina Simone anasemaje?.....

Read more...

Nguvu ya Wasanii !AU?

Nakumbuka wakati ambao usanii haukuheshimiwa kabisa Tanzania.

Swali:
Hivi sanaa inaheshimika Tanzania?

Ilikuwa kawaida sana kusikia watu wazima wakiizungumzia sanaa vibaya.Hasa sanaa yenye asili ya tamaduni zetu za kiafrika.
Shule zetu ambazo zimehusika kutujenga kifikira , zimetujenga vilevile kuamini ukifuata mdundiko basi wewe hujaelimika.
Nakumbuka enzi zangu zakufuata mdundiko huku najifanya kama vile ni bahati mbaya tu kuwa ngoma na mimi tunaelekea njia moja!
Nakumbuka ilivyokuwa vigumu kujumuika barabarani katika kufurahia ngoma hii.
Nakumbuka kuwa hata dini zetu zimesaidia sana kutufundisha kuwa maswala ya ngoma na tamaduni zetu yanauhusiano sana na ushirikina, na hata shetani mwenyewe.lakini dini hizi hazikukawia kutuletea piano,violin nk. wakati zikiondoa ngoma zetu.

Chakujiuliza ni kwamba inakuwaje kwa wenzetu sanaa zao za asili na za zamani zina heshima zaidi kuliko hata hizi zisifikazo na tuzionazo na kuzisikia kila mahali?. Ukienda kwa waheshimiwa wa magharibi, utakuta kwao ujanja ni kujikusanyia kazi za sanaa za zamani na miziki ya zamani wengine waiitayo classical nakadhalika.
Sasa sisi Watanzania ambao tutazaliwa kesho tutazikuta hata dalili za sanaa zetu za zamani?

Sisemi kuwa sanaa zetu za sasa sio poa, sisemi kuwa za zamani ndio bora zaidi, nachojiuliza ni kwamba tunaziheshimu na kuzitunza sanaa zetu?

Mimi naheshimu sana wasanii na kazi zao. Nasikia siku hizi kuna dalili kuwa heshima kwa wasanii na sanaa inazidi kukua Tanzania. Na nasikia ni kwasababu imejulikana kuwa wasanii wanaweza kupata fedha kwa kutumia vipaji vyao na kuishi maisha mazuri tu. Nachojiuliza ni kama tumegundua kuwaheshimu wasanii wa Tanzania kwa sababu baadhi yao wamefanikiwa kutuzidi, lini tutajifunza kuwaheshimu kwa kazi wazifanyazo?
Lini tutawaheshimu kwa elimu watupayo...nk?

Wasanii wana nguvu sana! Na naamini kuwa sanaa imekuwa na itazidi kuwa shule kubwa kwa jamii yetu Watanzania.Hata katika kipindi kilichokuwa kawaida kabisa kudharau wapiga na wacheza ngoma za kienyeji. Ngoma hizi za kienyeji zilikuwa na ni shule ambazo zimehitimisha asilimia kubwa ya Watanzania vijijini na mjini.Na ukizingatia zaidi vijijini ambako asilimia kubwa ya Watanzania wanaishi , unaweza hata kujua wanafikiria nini kwa kufuatilia nyimbo za ngoma za asili zinasemaje.

Hapa nimeongelea ngoma sana nikizungumzia sanaa. Kunawengine wanafikiria miziki tu wakifikiria sanaa! Nataka kukukumbusha kuwa naongelea sanaa kwa mapana na marefu yake hapa.

Swali:
Hivi kwanini hizi ngoma zinaitwa za kienyeji?
Msanii: Sema Yeee!
Watu: Yeeeee!
Msanii:Mikono ju! mikono juu!
Ukumbini:Watu wote mikono juu.


Kuna nguvu za wasanii ambazo mimi daima hunistaabisha sana!Naongelea wasanii wa aina zote.Lakini kuna Amri za baadhi ya wasanii naamini ndio zitiizwazo mara nyingi kwa furaha na bila mabavu kutumika kabisaaaaa!
Mcheki Bobby McFerrin alivyoushika ukumbi hapa chini hata bila kuongea

Huyu jamaa ni miongoni mwa wasanii ambao nimewashuhudia akikamata ukumbi akiwa pekee bila chombo chochote cha muziki na akawakamateni kwa zaidi ya saaa mmekaa kitako mkifurahi.Kama ushawahi kujaribu kukaa mbele ya watu unaweza ukajua ugumu wa kuushika ukumbi hata ukiwa na bendi nzima.
Mcheki hapa :


Wasanii mnanguvu sana za hata kuingiza watu mkenge bila wao kujijua.

Swali:
Au ndio maana wazazi wengi hupenda kuwaepusha mabinti zao kuwa na mahusiano na wasanii?

Hivi wasanii mnatumia nguvu zenu za usanii kusema nini au kutufundisha nini?
Nakubali mnatuburudisha.
Asanteni!

Read more...

Nakuheshimu -SHIKAMOO!Hivi hii ni Salamu?




Ni rahisi kusema Watanzania tumelelewa katika maadili yatufanyayo tuheshimu wakubwa zetu. Wengine watasema tunawaheshimu sana ndio maana hata katika salamu tunasema -SHIKAMOOO!Tukitarajia Wakubwa wajibu MARAHABA!

Swali:
Lakini ni kweli kuwa tunawaheshimu tuwapao Shikamoo?

Au tunawaogopa?

Nakumbuka tulikuwa tunatoa shikamoo kwa walimu tuliowadharau!
Nakumbuka tulitoa shikamoo kwa ndugu na jamaa ambao kisirisiri hatuwaheshimu lakini hatuwezi kusema.
Wengine hutoa shikamoo hata kwa wazazi kwa sababu usipoitoa utapigwa bakora.

Shikamoo= nikochini ya miguu yako.Hivi ni kweli hiyo?
Acha kunizingua!

Dondoo:
Unakumbuka ulivyotoa shikamoo kwa mtu halafu ukastukia ni mdogo kwako?

Hivi Shikamoo yako ni heshima , uoga au umekosa chakusema?
Haya bwana nakukubalia , labda ni salamu!

Lakini kama ni salamu, salamu maana yake ni nini?
Kama salamu ni kujuliana hali, sasa unapata kujua hali ya mtu kwa kumpa shikamoo?

Hivi shikamoo ni nini?

Simon: SHIKAMOO!
Wewe jibu lako:.........

Read more...

Hapo Zamani Sikuwa Hivi!

>> Sunday, January 14, 2007

Ukisikia msemo usipofundishwa na wazazi utafunzwa na ulimwengu unaweza ukafikiri maana yake ni kwamba upumzike kama wazazi washakufundisha. lakini ukweli ni kwamba hata ufunzwe vipi na wazazi ulimwengu hautakuonea aibu kukufunza, utakukatia denge tu na kukuweka kwenye kona.

Nazitamani enzi za utoto ambapo ukitaka kitu wazazi wanakupa tu. Halafu wakichelewa unaweza ukalia au kununa mpaka unapewa. Siku hizo kwa bahati mbaya ni za mpito. Ukweli wa maisha unaanza kuingia na siajabu ukakushtukizia tu.Ghafla unaanza kusikia unaanza kupewa shikamoo.Inafikia siku unastukia kuwa uko peke yako au labda ndio wewe unategemewa.

Dondoo:
Je , unawakumbuka watoto yatima na wale ambao inabidi wajitafutie wenyewe tokea utotoni?

Ukiwa na bahati unastukia mambo ya starehe au usipo bahatika moja kwa moja jasho linakutoka. Kwa wengine mtungi, mivuto na ngono inapata nafasi zake kutokana uhuru unaojitokeza kutokana na umri au kukua na kipato.Kama wanabongo fleva vijana wa Ngweair
hapa chini wanavyotuelezea siku yao.


Dondoo:
Lakini unawasikiliza wanasema nini?

Hapa sasa ni patamu kwa sababu kutokana na nguvu za ujana lolote laweza kutokea ambalo lika elekeza maisha yako kulia au kushoto. Enzi za mababu zetu au hata mababa zetu kulikuwa na taratibu zinazofuatwa za kimila ambazo zinamuongoza mtu katika kukabiliana na mambo mbalimbali ya maisha. Kwa wale waliokuwa wanapelekwa jandoni, walikuwa wanafunzwa jinsi ya kuwa mwanaume ndani ya familia. Na kwa wanawake walikuwa wanafunzwa jinsi ya kuishi na mume na kulea watoto na mambo mengine muhimu katika familia. Uchaguzi wa mke au mme ulikuwa ni wa wazazi ambao walihakikisha kuwa wanakutafutia mtu ambaye anasifa waaminizo zinakufaa.Kupendana mlikuwa mnajifunza baadaye. Hili jambo pamoja na mapungufu yake lilikuwa linaondoa baadhi ya matatizo ambayo tunakutana nayo hivi sasa.

Kizazi chetu ambacho tumejichukulia jukumu kina kasheshe zaidi.Halafu jinsi dunia inavyobadilishwa haraka na mateknolojia na mambo mengine kadhaa, kwa asilimiakubwa unaweza kujikuta mambo ya busara na ujinga kwa wengi ni magumu kuyatenganisha.Kuna mambo mengi unaweza kuyachukulia mfano lakini moja wapo ligusalo watu wengi ni mahusiano. Mahusiano katika jamii yanabadilika. zamani ulikuwa unawezatu kuamua kumtembelea mtu kwa sababu ni ndugu yako. Siku hizi pamoja na kwamba jambo hili linatendeka ,lakini hata ndugu anaweza kukustua ebwana eeh!Umekuja kufanya nini ?Unajua hapa waya mkali hivyo kama huna mpango afadhali anza tu.
Siku hizi hata wazo la mahusiano na umpendaye au hata wazo zima la kupenda tumelitafsiri vingine.Hivyo tunaanza mapema zoezi la mahusiano. Na mara nyingi inachukua kuvunjika kwa mahusiano kadhaa kabla hatuja tulia. Na hata tukitulia bado zoezi zima la mahusiano si rahisi. Tena afadhali siku hizi tuna simu nyingi bongo hivyo simu kama hizi aziongeleazo Muddy Waters hapa chini ni kawaida sana.


Maisha ni mchezo wa ajabu sana. Kwa maana unachezeka kinamna nyingi. lakini kitu kimoja cha ajabu ni kwamba siamini kuna anayeshinda kila kitu. Ukiwa angalia akina Mandela utagundua kunasehemu kuna mapungufu. Halafu utasikia Mfalme hana furaha na masikini anacheka mtaani. Halafu mchezo huu hauchagui shehe wala mwizi.

Lakini katika yote ,wengine hatutakwepa kukubali pamoja na ugumu wa maisha na yote mengine yatufanyayo tuishi namna hii , HAPO ZAMANI HATUKUWA HIVI.

Au Miriam Makeba anasemaje?.......



Lakini usiwe na wasiwasi ,kuwa na furaha kama akwambiavyo Bobby Mcferrin hapa chini.



Kuna marafiki zangu kadhaa wapitiao hapa wanasema niache kuongelea mambo haya. Lakini kabla sija acha niachie maoni yako .

HAPO ZAMANI WEWE ULIKUA Je?

Read more...

Hivi Wewe Jina lako Nani? Au...?


Haloooooooooooooooooooooooo!
Habari gani!
Shikamomoo!

Wewe: Mmmmm!Duh! Naona mambo yako si mabaya!
Yeye:Acha hizo Mshikaji!

Dondoo:
Unajua unaweza kuendeleza uhusiano wa ajabu na mtu kwa sababu hutaki tu kumwambia kuwa humjui?

Swali:

Uhusiano wako na Jina lako ni nini?

Nikawaida kusikia kua watu wamepata mtoto, halafu wanahangaika kupata jina la mtoto.Lakini labda hawahangaiki ila wanataka kupata jina zuri tu.

Au.....?

Lakini ni kawaida kwa wale ambao wanajenga taifa la kesho lenye mbegu zilizo pandikizwa shamba la nyumbani, jirani au pembeni kujikuta wako katika majadiliano ya jina la mtoto.


Au...?

Hivi mtoto jina lake.... au awe na jina gani?

Awe na jina la mama yake mzazi,baba,bibi,babu yake,... au?

Au awe na jina la shujaa wako, yake ..... AU?


Samahani najua unaweza au anaweza kuleta kibezi ilimradi ashikilie nguvu au maamuzi ya jina.

Au..?

Okei, ndio mapenzi na ndio siri ya mahusiano hayo!


Au?

Samahani , nilivyopiga hodi nilifikiria Alufani yuko nyumbani....!

Hivi Elizabeti atarudi nyumbani saa ngapi?...
Swali:
Hivi Mbwa wako uta muita nini au anaitwa nini?



KWA NINI?


Hivi wewe unauhusiano gani na jina lako?

UNAITWA NANI?

Samahani kwa kukusumbua!
Samahani inabidi nikuulize......!



AU...?


Samahani kwasababu ................
NAJUA UNALIPENDA JINA LAKO.

Au?!!!!!

Samahani!!!
Jumapili Njema!

Au...?

Read more...

Chuki

>> Saturday, January 13, 2007

Naipenda chuki
Chuki ambayo ni kiwanja cha upendo
Napenda kuichukia chuki
Nimejengwa na matofari ya kuamini chuki ni chungu, upendo ni utamu
Napenda kuchukia, naaibu kuonyesha chuki
Aibu ya kuonyesha chuki za vipendwavyo
Vipendwavyo vifyonzavyo uhai wa maangavu ya macho yangu
Napenda kupendwa, naogopa kuchukiwa
Asante Chuki
Asante kwa kuangaza upendo
Na Simon Kitururu 13.01.2007

Nakuacha na Nina Simone Leo aendelee kuelezea hisia za Upendo wakati nikiendelea kutafakari mstari mwembamba utenganishao upendo na chuki.

Read more...

Hivi Unazipenda sehemu za siri za Mwenzio?

>> Friday, January 12, 2007


Samahani ,nimekosea kuuliza. Je, unampenda mwenzio?




Inasemekana ukiwa umependa ubongo wako unaonyesha dalili sawa na mtu mwenye ugonjwa wa akili. Na mchezo mzima ni matokeo ya makemikali ndani ya mwili ambayo yanatabiri unavyojisikia na pia unachotenda.

Je, unampenda huyo mwenzio au ni matokeo tu ya mkorogo wa makemikali ndani yako ambayo huna utawala nayo?

Kuna wataalamu kama huyu Helen Fisher ambaye amebobea katika maswala taaluma ya jinsia ambao wamejaribu kuangalia sayansi ya kupenda.

Yeye anaigawa sanaa hii ya kupenda katika makundi matatu yanayo tawaliwa na kemikali tofautitofauti.

-Uchu(lust)
-Mvuto(attraction)
-Mahuba, (attachment)

Anasema Uchu hutokana na kemikali au homoni testosterone na oestrogen. Testosterone zaidi ni kwa wanaume na hizi homoni ndio zikusababizasho uwe unachekicheki kulia nakushoto kwa apitaye.

Mvuto unatokana na kemikali Dopamine, Norepinephrine ,na Serotonin. zikisaidiwa na neuro-transmitters ziitwazo monoamines. Hapa unaambiwa kuwa Serotin ni muhimu sana katika kupenda lakini ndio ikuleteayo kauchizi kidogo ukipenda kakidudekako
ukapendako. Norepinephrine au adrenalin ndio ikusababishayo kutoka jasho debe na moyo kudunda kama ngoma za Morris Nyunyusa.

Mahuba (attachment) hii husababishwa na na homoni zimwagwazo kutoka katika mfumo wa nevu(nervous system) ziitwazo oxytocin na Vasopressin. Oxytocin hutolewa na glandi iitwayo hypothalamus tokea utotoni. Na pia husaidia wakina mama kutoa maziwa.Hii inasemekana husababisha uhusiano wa karibu kati ya mama na mtoto. Na pia hii inasemekana mwanamme na mwanamke wanapofikia katika kilele cha ngono hutoa au hutoleana hii homoni ikiwa pamoja na chachandu nyingine, hivyo kusaidia mahusiano ya karibu kati ya mwanamke na mwanaume.

Sasa tukiachana na Helen Fisher na machambuzi yake, tunaweza kukubaliana mchezo wa kupenda ni mchanganyiko wa makemikali kibao.Na uhakika haya makemikali aliyoongelea Helen ni baadhi tu na hapo ujachanganya na vindumbwe vingine.

Swali:
Je, kupenda ni aina ya kichaa?

Maana mtu akipenda inasemekana huweza kufanya mambo yaajabu.Tushukuru hatushuhudii kila siku wafanyayo,lambayo, ....nk wapendanao

Dondoo:
Je, unawashangaa wasenge,mabasha, wasagaji nk kwa chaguo la pendo lao?


Usitishike!Wewe kweli unapenda kakitu kako ukapendako. Mimi najiwazia tu hapa bloguni.

Lakini kumbuka kama alivyosema Dr Franklin Tallis kuwa penzi na woga huingilia mlango mmoja.


Swali :
Hivi hizi sehemu za siri ni za siri kweli wakati matokeo ya matumizi yake yako waziwazi namna hii?Hapa nazungumzia watoto bwelele mitaani, ukimwi nk......

Msalimie umpendaye!Wikiendi njema!

Read more...

KIFO-Usitishike tunakumbushana tu!


Read more...

Umekumbuka kumshukuru Mama!

>> Thursday, January 11, 2007

Naamini kuna mambo mengine kuhusu wewe anayajua mama yako tu!
Labda kwako si muhimu kumshukuru mama yako, lakini kwangu ni muhimu.
ASANTE MAMA!

Read more...

Watanzania na matakwa Gari Mkweche!

Binadamu anazaliwa tayari akitaka. Kuna mambo mengi watu wamejaribu kuelezea kuhusu matakwa ya binadamu. Mtoto akizaliwa tu atalia kuashiria kuna mapungufu. Kuanzia hapo safari ya kutaka inaanza. Wengi nafikiri tumeanzia katika kutaka maziwa ya mama, lakini leo hii matakwa yetu yashakua magumu hata kuyaelezea. Na ukichanganya matakwa yetu yote Watanzania ukayaweka katika umbo la gari basi gari hilo ni mkweche.Mkweche kutokana na ukweli halina mbio na huaribika haribi kila wakati. Na ukimuuliza mtu mwingine anaweza kusema hata maili kadhaa lilizovuka ni kutokana na kuvutwa. Sasa gari hili ni lazima litengenezwe la sivyo tutabaki maporini.

Baadhi ya watu waliojaribu kuelezea matakwa ya binadamu na nini kinawasababisha wachukue hatua fulani fulani ni huyu Abraham Maslow.
Yeye aliyagawa matakwa haya katika sehemu tano katika miaka ya arobaini huko.

1.Kibaolojia na kimaumbile kama:hewa, chakula, kinywaji, pakuishi, ngono, kulala nk
-Biological and Physiological needs - air, food, drink, shelter, warmth, sex, sleep, etc.

2.usalama: kujikinga na mambo kama mvua,juakali, usalama kama kutozurika na wanyama watu wengine,nk
-Safety needs - protection from elements, security, order, law, limits, stability, etc.

3.Kukubalika kundini na kupendwa au kupenda:Kundi la kikazi,famili,mpenzi nk
- Belongingness and Love needs - work group, family, affection, relationships, etc.

4. Sitaha/heshima:heshima binafsi/kujiamini, kuwa huru, kuheshimika katika jamii,cheo nk
-Esteem needs - self-esteem, achievement, mastery, independence, status, dominance, prestige, managerial responsibility, etc.

5.Haja ya kujitimizia mambo:
-Self-Actualization needs - realising personal potential, self-fulfillment, seeking personal growth and peak experiences.


miaka ya tisini mwingine katika kumuelezea Maslow akaongezea nyingine tatu

1.Kujua:
-Cognitive needs - knowledge, meaning, etc.

2. Maswala ya kutafuta uzuri wa kujitakia. Kama vile uzuri kwa kufanya mazoezi...nk
-Aesthetic needs - appreciation and search for beauty, balance, form, etc.

3. Matakwa ya kusaidia wenzako kufikia pale watakapo
-Transcendence needs - helping others to achieve self actualization.

Ukitumia mtazamo wa Maslow katika kuangalia Watanzania utakuta kila mtu yuko katika sehemu tofauti kimatakwa. Wengine ndio kwanza wako katika namba moja wakati wengine wako namba nane. Wanyonge wanahangaika kupata msosi na pakulala wakati wengine wanayasikia matatizo haya redioni.Hili ni jambo lakawaida ni liko duniani kote. Ila nadhani tofauti ya Tanzania ni kwamba matakwa yetu hayafuati mkondo mmoja.Na Tanzania hakuna mfumo uliojijenga uongozao utimilizaji wa matakwa ya watu katika mwelekeo mmoja. Hivyo tajiri na masikini mara nyingi ukifumba macho husikii tofauti. Vilevile mwenye busara na mjinga mara nyingi ukifumbua macho huoni tofauti.

Tatizo jingine katika gari matakwa mkweche hili ni ukweli linaendeshwa na dereva anayebunia barabara. Basi hapo ndio utamu ulipo.

Pamoja na ugumu wa kuyachambua matakwa ya binadamu ,mimi bado nafikiria kuwa ni vigumu zaidi pia kuyaelewa kabisaaaaa matakwa ya viongozi wa Tanzania. Kwa maana mara nyingine naona kama wanatabia zilizo changanyika.Wanafanya mambo kama walalahoi halafu hapo hapo wanafanya mambo kama ya wenyenazo. Viongozi wengi wa Tanzania ni ombaomba halafu hapohapo wafujaji. Rushwa wanataka katika ombaomba zao halafu vilevile hukawi kusikia wanavyofuja mali za umma.

Hivi Watanzania wanataka nini?

Dondoo:
Hivi wewe unataka nini?
Labda tuseme unataka mtoto. Wa nini? Labda ili familia ikamilike? Ili iwe nini? Labda iliakusaidie Uzeeni. Ili iwe nini? Kama ni ili akusaidie uzeeni. Je, wewe unataka mtoto au unaweka bima ya uzeeni? Majibu na maswali ya unataka nini ni mengi.

Lakini hebu niambie! Hivi ni kweli unataka hicho unacho kitaka au unadhania tu kuwa una kitaka?

Umuhimu wa kujua matakwa yako na kwanini unataka ni muhimu. Mara nyingi unaweza ukadhania tu unataka kitu kumbe ukweli ndio huo kuwa unadhania tu. Ukipewa hicho kidude unagundua wala hukihitaji. Kujua ukweli kuhusu tabia za matakwa yako si rahisi lakini ni muhimu kujaribu kufikiria jambo hili. Unaweza kujikuta kuwa unapoteza muda kwa vitu ambavyo si muhimu kwako.

Dondoo:
KUJUA. Je, unajua?
Mwandishi Robert Fulghum alishawahi kuandika katika kitabu chake kiitwacho All I Really Need to Know I Learned in Kindergarten kuwa baada ya mihangaiko yote akagundua cha muhimu alichokuwa anataka kujua maishani mwake alijifunza shule ya vidudu.
Mimi nafikiria katika matakwa pia unaweza ukakuta baadhi ya mambo mengi tulisha yapata zamani. Sasa kilichobakia ni kujua kuwa hakuna haja ya kuhangaikia mambo ambayo tunayo tayari. Tulenge mambo ambayo tunayahitaji au kwa maneno mengine twende katika ngazi nyingine katika matakwa. Tatizo lililopo mimi nadhani ni kuchanganya yale matakwa tuyatakayo ya muhimu na yale matakwa ambayo tunadhani tunayataka.
Tatizo pia ni kwamba tunaongozwa katika chi yetu itupayo uwanja wa kutimiza matakwa na viongozi wanao dhania tu. Nafikiri inabidi tufikie wakati ambao tutapata viongozi watuongozao katika safari hii ya kutimiza matakwa wanaojua na sio kudhania tu.Kiongozi anayejua atajua kutumia watu wote katika hamu zao tofautitofauti za kutimiza matakwa kujenga mfumo ambao ni mzuri katika kutimiza matakwa ya watu wote.

Sun Tzu katika kitabu chake cha The Art Of War anasema:
The skilful employer of men will employ the wise man, the brave man, the covetous man, and the stupid man. For the wise man delights in establishing his merit, the brave man likes to show his courage in action, the covetous man is quick at seizing advantages, and the stupid man has no fear of death.

Mtumiaji mzuri wa watu ataajiri mtu mwenye busara, mtu shujaa, mroho wa vitu,na mjinga. Kwa sababu mwenye busara hupenda kujulikana ana busara, shujaa hupenda kuonyesha ushujaa, mroho ni mwepesi kudaka upenyo wa kujipatia, na mjinga haogopi kufa.

Nilipenda mfano wake huu kwa sababu alionyesha kuwa katika vita mjinga na mwenye busara wote ni muhimu. Mimi nasema katika vita yetu hii ya kujikomboa matakwa yetu wote ni muhimu. Na yakijulikana na tukiwa na madereva wanaojua barabara yatazaa jamii ambayo iliyoendelea , inayotatua matatizo yake bila kuomba msaada wa kuvutwa. Kwani katika kutimiza matakwa yako unatimiza na matakwa ya wakuzungukao. Na kama barabara inajulikana daima hatua itakuwa ni mbele na kwa mwendo mzuri.

Katika dunia ya leo ambayo Afrika, tanzania na mtu mweusi ametumiwa sana kutimiza matakwa ya wengine ni muhimu Afrika,Tanzania na mimi nawewe tupate matakwa yetu. Hivyo basi tuyajue matakwa yetu.

Sun Tzu pia anasema:
Knowing the enemy enables you to take the offensive, knowing yourself enables you to stand on the defensive.Attack is the secret of defence;defense is the planning of an attack.
Ukimjua adui unaweza kumshambulia, ukijijua unaweza kujilinda. Kushambulia ni siri ya kujilinda; kujilinda ni kupanga kushambulia.

Narudia tena:
HIVI WEWE UNATAKA NINI?

Haya nawaacha wakati mawazoni nikiendelea kufikiria haya maisha tuliojikuta tumezaliwa na kuishi katika mstari wa mbele vitani kama Eddy Grant aelezeapo hapa chini katika wimbo Living on the frontline

Read more...

Unakumbuka Enzi za Utumwa wa Mtu Mweusi?


Mimi nisikufiche , kwa muda mrefu nilikuwa naamini kuwa utumwa ni jambo lililopita enzi hizo na wala halinihusu mpaka nilipogundua kuwa bado naishi katika enzi za utumwa.
Ingawa utumwa wa kimawazo ndio umetawala lakini utumwa uleule unaosemekana ulifutwa bado upo.

Watu weusi hata ambao wanadhani hawakuishi utumwani tumeathiriwa na tunazidi kuathiriwa na utumwa.Kimawazo, kiakili na ki kona zote zimgusazo mtu mweusi.UNABISHA!
Dondoo:
Je , wewe unadhani uko tayari kununua mtu kwa shilingi ngapi?
Hapa siongelei sehemu yake ya mwili.

Namuachia Burning Spear ambaye anajaribu sana kukumbusha watu kuhusu swala hili na .....

Read more...

Vita vya Tanzania na Malawi vyaanza!

>> Monday, January 08, 2007



Naombea hili lisije tokea!
Lkini, hivi swala la mpaka wa Malawi na Tanzania limefikia wapi? Najiuliza kutokana na ukweli serikali yetu Tanzania inajulikana kwa kutotafuta majibu ya matatizo kabla tatizo halijakuwa sugu au kutoa makucha.Naona Somalia walipochukua utawala kwa muda mfupi watu wa Mahakama ya Kiislamu, wakaanza kudai sehemu iliyopo Ethiopiaiitwayo Ogaden, waishio Wasomali wengi.Nisikutishe labda Malawi haitapata mtawala atakayedai songea ni Malawi!Sawa basi nimekubali, hata dai Songea , atadai Mtwara tu au sehemu walizopo watu wakabila fulani!

Tukiacha utani;!

Ukisoma habari za Tanzania utakuta mara nyingi zinaongelea matatizo ambayo yameshajitokeza.Mambo ni mengi.Baadhi ni kama haya ya matatizo ya umeme, mafuriko, chakula.....nk. Sababu kubwa mimi naona nikutokuwa na mikakati yenye kuona mbele ambayo inaelezeka.Serikali husemekana ni watu, na watu ni serikali, lakini ndani ya Tanzania serikali ni serikali na watu sharti kuwakimbia polisi.


Dondoo:
Hivi unafikiri ilitatizo la umeme halitatokea tena?
Hivi kama Dar es Salamu mafuriko yanatokea kutokana na sababu zijulikanazo je huko kwingine itakuaje?

Inasikitisha kujua sababu nyingine za mafuriko Dar eti ni kwa sababu Diwani kajenga nyumba kwenye njia ya mfereji wa maji na sababu nyingine kama hizo.

Haya leo hii katika CIA Fact BOOk

Watumia intanet Tanzani nzima hadi kufikia 2005: Watu 333,000

Meli zilizoko Tanzania: Za mizigo tu 1. Za abiria na mizigo 4. Za mafuta 4

Wakimbizi: 443,706 (Burundi). 153,474(Kongo).3,036 (Somalia) makadirio ya 2005

Simu:148,400 za nyumbani kwa makadirio ya 2004. Simu za mkononi 1.942,000(2005)

Kiasi cha gesi ya aslikipatikanacho Tanzania:
22.65 billion cu m (1 January 2002)

Kiasi kitumikacho Tanzania: 0 cu m (2003 est.)

Kiasi cha gesi itengenezwayo Tanzania:
0 cu m (2003 est.)

Uhakika kuwa kuna mafuta Tanzania:
0 bbl (1 January 2002)

Umeme utengenezwao Tanzania:
3.152 billion kWh (2003)

Umeme utumikao Tanzania:
2.959 billion kWh (2003)

Umeme Uuzwao nje na Tanzania:
0 kWh (2003)

Umeme Ununuliwao na Tanzania:
28 million kWh (2003)

Watanzania huishi miaka mingapi:Miaka 45 kwa wanaume.Miaka46 wanawake.Makadirio(2006)

Idadi ya Watanzania kimiaka:
Miaka kati ya 0-14 : 43.7% (wanaume 8,204,593/wanawake 8,176,489)
Hapa kunao ambao watakosa wake.Kasheshe!

Miaka kati ya 15-64: 53.6% (wanaume 9,906,446/wanawake 10,178,066)
Nafikiri ndio maana wengine walipata mke zaidi ya mmoja

Miaka 65 na zaidi: 2.6% (wanaume 422,674/wanawake 557,124) (makadirio ya 2006)

Migogoro ya kimataifa:
Tanzania inamgogoro na Malawi kuhusu Ziwa Malawi na Mto Songwe.
Samahani, ziwa Nyasa.


Hivi Ushajiuliza kwanini nchi zote waziitazo zilizoendele zina mchezo wakufuatilia habari za nchi nyingine?Zote zina watafiti waliobobea katika masomo ya nchi nyingine.Hivi Tanzania tunaijua Kenya?

KAMA UNATAKA KUMSHINDA UNAYE MKABILI, MJUE! JE SISI TUNAWAJUA TUNAOKABILIANA NAO JE TUNAJIJUA+

Read more...

Yote Maisha ,Yote Shule! Naheshimu shule ikufunzayo kwa kukupiga ngwala

>> Sunday, January 07, 2007

Nakataa kukubali kuwa mambo barani Afrika yatakuwa katika hali ya kusikitisha daima. Naamini tukiendelea kujielimisha na kuelimisha wenzetu nini kinaendelea duniani tutafikia hatua ambayo hakutakuwa na ujanja zaidi ya kujikomboa, kujiheshimu, na kupendana au kujifunza kuishi pamoja huku tukijua kuwa tunahitajiana hapa duniani.Kujielimisha hapa namaanisha kuzingatia mafunzo ya shule ya maisha, shule ya uzoefu, shule uipatayo kwa kupigwa ngwala na pia shule tuipatayo baada ya kuona mwenzetu kapigwa mueleka.

Baadhi ya mafunzo haya hupatikana kwa kuishi katika eneo fulani. Nimekutana na mijadala mingi mtandaoni kuhusu faida na hasara za wabongo kukaa ughaibuni. Kuna hasara nyingi na faida zake. Lakini kama kuna faida moja niijuayo ni ile ya kupata funzo kwa kupigwa ngwala na hali halisi.Nakumbuka bongo tulikuwa tunaimba nyimbo za kumsuta kaburu kwa ubaguzi na nilikuwa nafikiri najua ubaguzi ni nini. Kusema ukweli ubaguzi hauwezi kuuelewa kwa kusoma kitabu au kuaangalia sinema. Ni mpaka ukutane nao uso kwa uso uwe unakulenga wewe ndio hapo utajua ladha yake. Kuna maswali mengi yanaulizwa kuhusu tofauti za ughaibuni na bongo! Hakuna mtu mwenye jibu moja kwani hali halisi kwa kila mtu ni tofauti na shule ya maisha ni tofauti kwa kila mtu akutananaye nayo.Hapa siongelei watu watembeleao nchi nyingine kwa wiki kadhaa na ambao hawaishi na mifumo ya nchi hizo.Hapa siwaongelei mabalozi ambao kwa taratibu ofisini kwao ni nchini mwao. Hapa nawazungumzia watu ambao wanaingia mtaani wanakabiliana na wazawa walalahoi na waliofanikiwa.Wanakutana na kujifunza kutoka kwa watu wa kawaida mtaani kwa kupigana mieleka ya kiakili, kisaikolojia na hata ya kinguvu za mwili. Hapo ndipo unaweza ukasema umeenda shule ya maisha ughaibuni.Na shule hii mafunzo yake hayasahauliki. Na shule hii katika mengi ikufundishayo ni kumjua mtu unayekabiliana naye.

Dondoo:
JE, UNAKUMBUKA HADITHI ZA JESHINI?jE , KUNA WATU WAWILI WALIOWEZA KUKUSIMULIA KUWA WALILIKABILI JESHI KWA NJIA ZILIZOFANANA?

Kwanini ninaongelea shule hii?
Naamini Afrika imenyonywa sana na mataifa ya magharibi ,kiarabu na kwingineko. Na bado inanyonywa sasa hivi!Basi kama kunakitu kiitwacho adui au kitu chakujiadhari nacho itakuwa ni mataifa haya mageni ambayo yamebobea katika kutuingiza mkenge. ILI KUMSHINDA ADUI SHARTI UMJUE ni kiini cha kujikwamua katika janga.Na narudia hakuna shule nzuri ya kumjua mtu kama kuishi naye kwake ambako haitaji kujifanya mzuri ili akuridhishe.Basi kwa hilo walioko ughaibuni wanapata shule nzuri sana.


Naamini watu wengi hapa duniani hasa Afrika kwa muda mrefu tumenyonywa na mataifa ya nje kutokana na kutokujua ni nini wanafanya na ni nini kinaendelea. Naamini pamoja na watu kwenda shule, kuna mambo mengi watu hujifunza kwa kukabiliana na hali au hata kupigwa gwala na halihalisi.


Mara nyingi tunapoishi na kukabili siku hadi siku ni rahisi kusahau kuwa kila siku ni siku moja ya shule katika maisha. Mara nyingi tuongeleapo shule humaanisha mahali paitwapo shule na elimu ni ile ifundishwayo shule na mtu aitwaye mwalimu. Kwangu mimi naamini nimejifunza mengi mashuleni na mengi nimejifunza kutoka katika mazingira ya shule bila mtu aitwaye mwalimu kuhusika. NAAMINI KILA MTU NI MWALIMU NA KILA MTU NI MWANAFUNZI.

Ngoja nikuelezee baadhi ya elimu niliyopata mtaani ambayo mpaka leo inanipa mwelekeo wa maisha.Nakupa baadhi tu ya mambo ambayo nilijifunza kutokana na kuwepo mahali bila ya funzo hilo kuwepo kwenye silabasi.Kwani naamini kila siku tunafunzwa kitu fulani iwapo utafungua macho na kujifunza.

Ninaanzia nilipo kwenda shule ya vidudu ya Jeshi, Mbeya,wakati nakaa Simike .Pale nisichokisahau ni jinsi nilivyoumwa na mbwa wa Jeshi baada ya kuwachokoza kwa kuwapiga na rungu nililolitengeneza kwa kutumia lami.Nilijifunza kuwa pamoja na kujiamini, haitoshi nilijifunza kujenga heshima kwa wanyama.

Nikaendelea shule ya vidudu ya kanisa la Katoliki,Songea . Hapo pamoja na kujifunza kuwa mahiri katika AEIOU,nilipata darasa la mambo ya dini ambayo yananizingua mpaka leo hii.Pia ndio mara ya kwanza kujua wakubwa wananywele sehemu za siri, kwasababu mlinzi wa shule alituonyesha.

Dondoo:
HIVI KWANINI SHULE HIZI HUITWA ZA VIDUDU?KWA NINI SHULE HIZI SIO ZA MSINGI?


Nikaenda kuanza shule ya msingi Mfaranyaki.Hapo nakumbuka ni mara ya kwanza katika kupigana nilipigwa na mjamaa aitwaye Deogratus ,nimesahau jina lake la ukoo.Tulipigana raundi mbili zote nikapigwa.Nilivyopigwa raundi ya kwanza nilidai kwasababu ya viatu.Tulivyovua viatu nikapigwa tena nikavimba jicho nikasingizia aliniwekea pilipili jichoni.Funzo nililolipata kisawasawa ni jinsi gani mtu mwingine anavyoweza kunizidi nguvu kisawasawa. Hapa ,Mfaranyaki pia nilishikwa nikimbashia msichana darasani na mwalimu ambaye alikuwa ni rafiki wa wazazi wangu.Hakunisemea nyumbani lakini tokea siku hiyo sijawahi kubashia mwanamke tena hadharani , labda hata chobisi.Hapa Mfaranyaki ndio nilikutana na msichana wa kwanza ambaye nilimpenda kama msichana.Ingawa alikuwa anaishi mbali na nilipokuwanaishi nilikuwa najaribu kupita nje ya geti lao ilimradi nimuone tu ,halafu narudi nyumbani nikiwa mwenye furaha.Nilijifunza sana kuandika barua za mapenzi,nilifanya majaribio ya kuweka poda na hata kuchora maua.Kwa bahati mbaya barua yangu moja ya mapenzi ilishikwa na dada yangu na kusomwa na familia nzima !Nafikiri unajua jinsi gani nilitaniwa na jinsi gani niliingia aibu.Kwani hata umahiri wa kauli kwa wanadada sikua nao.Nafikiri unajua nilijifunza nini hapa.

Nikahamia shule ya Mchikichini ,Morogoro. Hapa ni sehemu ya kwanza nilipogundua kupendwa na wanawake na pia kugundua si kila umpendaye anaweza kukupenda pia.
Nafikiri utagundua kuwa hapa nilikuwa katika kipindi gani kwa maana mapenzi na wanawake walikuwa muhimu. Kipindi hiki nilipata uhakika kuwa wazazi sio ukweli kuwa hawaishiwi pesa.

Nikahamia Morogoro ,Sekondari. Hapa kwa mara ya kwanza niliona maiti ya mwanafunzi mwenzangu wa darasa moja ikining'inia kwenye kitanzi cha kanga, ambaye alijiua kutokana na matatizo ya kifamilia.Hili jambo mpaka leo silisahau.Huyu mwanadada alikuwa yuko sawa tu darasani. Anacheka na kila mtu darasani.Mchana tulivyoenda kula iliturudi shuleni baadaye akajiua.Nilijifunza si kila akuchekeaye anafuraha moyoni. Hapa Moroseki pia niliitiwa kundi ilikunipiga kutokana na kumtosa mwanadada kimapenzi.Cha ajabu kundi lilokuja kutaka kunipiga ni la marafiki zangu au watu niodhani ni marafiki zangu.Sikupigwa kutokana na wao wenyewe kuona aibu.Lakini nilijifunza jinsi gani mwanamke ananguvu yavishawishi.Aliweza kututenganisha marafiki kirahisi tu. Nilipoteza marafiki wengi kwa mara moja kwa mara ya kwanza siku hiyo.Nilijifunza kuchagua marafiki.Wakati niko Morogoro Sekondari pia ndio mara yangu ya kwanza kuanza kufanya kazi kama kiongozi wa misafara ya wageni kutoka nchi za nje, waendao vijijini kujifunza maisha ya Kiafrika.Nilipata kazi hii kwa sababu ya kujua ung'engé. Kwa mara ya kwanza nilijua utamu wa pesa uliyoitolea jasho.

Nikahamia Mazengo Sekondari, Dodoma. Hapa jambo kubwa nililojifunza ni jinsi ya kuishi na watu mbali na nyumbani.Nilijifunza pia umuhimu wa chakula.Hapa sisi wanafunzi tulikuwa tunachukia vyakula vya shule lakini wanakijiji kutoka vijiji vya karibu walikuwa wanakuja kuokota maugali hata ambayo wanafunzi wametupa au kudondosha kwenye michanga.Baadaye nilikuja kugundua kuwa wakisha okota vyakula hivi huenda nyumbani kuvianika halafu hutwangwa nakuwa unga tayari kwa msosi wa nyumbani.Nilijifunza pia ladha ya maji hata msosi huzoeleka ukikabwa na kiu au njaa kisawasawa.Unakumbuka ladha ya maji ya dodoma yana chumvichumvi?

Yote Maisha , Yote shule!

Sababu za kukukumbusha kuwa kuna mambo tuyakumbukayo na ambayo yanachonga jinsi tunavyopiga hatua hapa duniani ambayo hayana uhusiano wa moja kwa moja na madhumuni yaliyowekwa wazi kwanini tuko sehemu fulani na ni nini tunafanya.Naamini unajua hilo, lakini naamini ni muhimu kukumbushana umuhimu wa elimu hizi zitulengazo kila siku bila ya sisi kupanga. Kwa wanafunzi baadhi ya masomo muhimu kisawasawa tujifunzayo hayahusiani na yanayofundishwa darasani.Siwezi kusema kuwa yanayo fundishwa darasani hayakunisaidia au nilikuwa siyamudu!Nikisema hivyo nitakuwa naongopa. Nachojaribu kusema ni tuwe na busara ya kujifunza na kutenda kwa vitendo ili kuboresha maisha yetu katika muda huu mfupi tuishio.Tuyape kipaumbele mafundisho ya darasa hili la maisha hata katika kipindi hiki ambacho watu weusi tunajaribu kujikomboa kutoka katika makucha haya yatunyanyasayo hapa duniani.

Nafikiri unajua sasa kua hapa maishani mimi niko shuleni.Hapa nimekazia kujifunza kutokana na maumivu.LAKINI TUJIFUNZE PIA KUTOKANA NA ULAINI,STAREHE,nk wa baadhi ya mambo yatukumbayo.

Narunia:
ILI KUMSHINDA ADUI SHARTI UMJUE, LAKINI INABIDI UJIJUE!Kujijua na kumjua tutumie nyenzo zote tulizo nazo.


Kuna madarasa mengi ningependa kufaulu na mojawapo ni hili la mapenzi. Auningependa niamke tu siku moja halafu niwe na hakika asilimia mia moja kama Billy Ocean asemavyo hapa chini.Lakini najua hii ni ndoto tu kwangu.Mimi ni miongoni mwa wale ambao hata nicheze bahati nasibu sipati.Ni mpaka ni toe jasho.

Read more...

Indian Ocean?

Nimechoka na majina ya bahari zizungukazo Afrika zenye majina ya ajabu ajabu.Hivi kuna mtu anakumbuka Waafrika walikuwa wanaitaje hizi bahari?

Read more...

Heri Ya Krismasi ya Kalenda ya Julian!

Haya tena tufurahie Krismasi ya Kalenda ya Julian.Siku kumi na tatu baada ya Krismasi ya kirumi leo tarehe saba vifijo na vigelegele.Duh Nimesahau, kumbe vifijo na vigelegele ni mambo yetu sisi waafrika kwenye krismasi zetu za kiafrika !Au niseme kwenye sherehe zetu za kiafrika?

NITAWATANGAZIA TAREHE YA KRISMASI YA KALENDA YA SIMON KITURURU HIVI KARIBUNI.

Read more...

Saikolojia ya kumpiga Mwizi

>> Saturday, January 06, 2007

Mtu.1:Mwiziiii!Mwiiizi!Mwiiizzziii!
Mtu.2:Piga huyoooo!...
Mtu.3:Hivi kaiba nini?
Watu:Hatujui lakini nasikia kamuibia mama mmoja , piga huyooo!Pumbafu kabisa huyo!!

Binadamu ni kiumbe kinachopenda kufuata mkumbo kikipewa mazingira yafaayo.Nachojiuliza ni kwa jinsi gani watu Tunasahau hili. Sababu kubwa kwa hili ni tabia ya binadamu yakupenda kurahisisha mambo. Karibu kila kitu binadamu anacho gundua au kupenda kutumia sana ni kifaa kirahisishacho mambo.Kuanzia kijiko, ngazi, baiskeli, jembe, nk. Lakini jambo kubwa binadamu analopenda kurahisisha ni kufikiria. Nirahisi kufuata mkumbo kuliko kufikiria na kuanzisha mambo au jambo mwenyewe.
Madhara yake ni kwamba mfumo huu uliopo duniani sasa hivi ambao umetutenga Afrika ni vigumu kuuondoa.Visingizio tunavyovingi.Kimojawapo ni kuwa kila mtu na maisha yake.Kwa hiyo kama mimi na familia yangu mambo si mabaya basi hakuna haja sana ya kuangaika.Kisingizio kingine ni kuwa ni afadhali zimwi ulijualo kuliko zimwi usilo lijua.
Lakini hivi zimwi hili tunalijua?

Ushawahi kuona watu wanampiga mwizi? Ushasikia jinsi maaskofu na wachungaji wakihutu na kitutsi walivyo shiriki katika chinjachinja?

Nachojaribu kusema ni kwamba, naamini katika kila mtu kunakisehemu kinachoweza kuvuka mpaka.Na katika kila binadamu kunakisehemu kinachojaribu kuhalalisha mambo bila fikira.Kwasababu ni ubinadamu. Lakini ni ubinadamu pia kujua nini kinaendelea na kujikwamua katika zimwi hili ambalo halijatunufaisha Waafrika.
Nimesoma jinsi watu wanavyomshangaa Ditopile kuua!Hivi akikwambia lengo lake lilikuwa si kuua utapinga?

Read more...

Dr. Asha-Rose Migiro


Hongera!

Read more...

Coco Fathi Reinharz- na mapishi ya Kiafrika katika steji ya dunia

>> Tuesday, January 02, 2007

Katika kuongea na rafiki yangu mmoja, nilipata kuzinguka kwa jinsi gani kuna watu wengi duniani wanaamini Afrika hatuna mapishi. Kutokana na vyombo vya habari kuzidisha habari za watu kufa njaa Afrika, basi kuna watu wengi waaminio kuwa Waafrika hula chochote ilikuwa hai tu. Wanadhani kuwa Afrika hatujui ladha za vyakula, kwani hatuna luxury hiyo.Ikabidi nicheke sana, kwa maana nikawauliza hivi hata historia za juzi juzi ambazo zinaikubali Afrika kama sehemu ambayo utundu wa viungo vya Chakula umesahaulika? Hivi hata Zanzibar si ilishawahikuwa maarufu duniani kutokana na viungo?

Lakini sasa hivi naona wameanza kuibuka wapishi wa vyakula vya kiafrika wanaosifika na kuanza kutambulika kimataifa.Mmoja wapo ni huyu Coco Fathi Reinharz aletaye mapishi ya kiafrika kwenye Five Star hotels. Ninachojua, sifa yao kubwa imetokana kuweza kuandaa na kukifikisha chakula mezani kwa staili ambazo Wamagharibi wanazizimia . Pamoja na jambo hili kuwa zuri najiuliza hivi kwanini ifikie mpaka tubadilike ndio tutambulike? Mbona Wachina na staili yao ya kula karibu kila kitu na pia kula na vijiti hawalazimiki kuibadili?Nafikiri mapishi mengi ya Kiafrika kutokana na ugumu wa kupata resepi zake katika maandishi, inapunguza kasi ya kujulikana kwake. Afadhali Miriam anasaidia kutatua swala hili.
Wakati nikiendelea kulitafakari swala hili, ni matumaini yangu siku moja habari ya Waafrika kufa njaa itakuwa inasomwa kwenye vitabu vya histori tu.

Read more...

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP