Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Malcom X akifufuka leo!

>> Friday, January 19, 2007



Katika safari ya Malcom X iliyomleta mpaka Afrika , alikuwa anataka kujifunza imekuwaje waafrika ndani ya Afrika wamejikomboa haraka kuliko Wamarekani weusi. Katika moja ya jambo ambalo alikuwa anaona Waafrika wamepiga hatua ni hili la kuanzisha umoja wa nchi za Afrika. Alikuwa anatumia hoja hiyo hata kujaribu kuunganisha Wamarekani weusi au msikilize kwanza........


OAU ingawa imesifiwa na Koffi Annan kuwa imeleta umoja wa Afrika , mimi siamini katika hilo.

Hivi umoja wa Afrika tuuzungumziao uko wapi?

Ikiwa Tanzania na Kenya kuwa na umoja ni kasheshe hivi kweli tunaweza kusema OAU ilileta umoja wa Afrika? Hivi si ndio OAU hii hii ambayo iliongozwa na akina General Gnassingbé Eyadéma , Mobutu Sese Seko Nkuku Ngbendu wa za Banga , Mohamed Siad Barre, ambaye alikuwa anajulikana kutaka kuichukua Jibuti ,ogaden na hata sehemu za Kenya akiamini kuwa Somali kubwa ni zaidi ya mambo mengine? Je , si na Idi Amini naye alishika hatamu wakati anajulikana mambo yake kwenye OAU hii hii?

Swali:
Hivi inawezekanaje chombo kitarajiwacho kuelekea kulia kikawa kinaendeshwa na dereva mwenye nia yakwenda na aelekeaye kushoto?

Sasa labda nimechanganya mambo kuhusu hii OAU, nasikia siku hizi tuna AU.
Lakini nasikia pia hii AU inataka kumpa kiti cha kushika hatamu Raisi wa Sudani, Field Marshal Omar Hasan Ahmad al-Bashir .

Dondoo:
Hivi unajua kuwa Sudani inatambulika kama ndio nchi ya Kiarabu kubwa kuliko zote kieneo?

Sasa kama ni kweli , huyu raisi wa Sudan si ndio yule yule anayewabagua baadhi ya Wasudani ndani ya nchi yake? Hivi kweli hii AU itafikia siku moja ikawa na meno ya kutatua matatizo ya Afrika?

Hivi Malcom X akifufuka leo atauonaje muungano wa Afrika?

Sawa, labda ni kweli mwanzo mgumu! Lakini hivi kipimo cha mwanzo ni kipi? Mwaka, miaka, mlongo,au karne?

6 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Anonymous 6:42 pm  

Mzee Simon,niwakati wakijivika Malcom au Martin,kwanini tunabaki tukiadithia tu?nani anaweza kuviva viatu vya hawa waafrika wenzetu?we should be martin or Malcom for the better of Africa.

Mzee Simon unaweza kuvivaa vitu vya Malcom au Martin?

Simon Kitururu 11:35 am  

Siwezi! Mimi nitakuwa Simon tu.

Anonymous 12:30 pm  

Mzee Simon,sio kwa sura bali kwa vitendo.Ndio wewe ni Simon na unaweza kupenda tabia ya mtu na kuiga kama ni tabia nzuri inayofaa katika jamii.

Egidio Ndabagoye 8:57 pm  

Rasta Luihamu nani atakuwa wa kwanza kuvivaa viatu vya Malcom?.Ni wewe?.Je na sisi vitatutosha kweli?

Anonymous 1:11 am  

Malcolm alipokuja Dar alikaa kwenye hoteli moja karibu na mnara wa saa. Aliizimia sana Tanzania na Afrika. Afrika ile sio hii. Msemo huu wa mwanzo mgumu wakati mwingine unatumika kuficha mapungufu ya harakati.

Mwanzo tulishaupita siku nyingi. Mwanzo hadi lini? Kama ulivyoonyesha Simon, kuungana kwa bara sio lelemama. NI kazi inayohitaji viongozi wenye uwezo wa kuweka maslahi ya watu na umma wa waafrika mbele ya maslahi yao na mipaka ya kufikirika iliyochorwa na majamaa hawe wezi. Nani mwenye uwezo huu Afrika? nani? Haya, Bashir ndio anapewa uenyekiti wa umoja wa Afrika. Matusi ya nguoni haya.

Umoja huu kama umoja wa afrika mashariki ni vilabu vya viongozi kukutana na suti zao kunywa divai na kupitisha maazimio na maazimio yanayoishia vitabuni.

Angefufuka Malcolm leo hii asingekwenda Afrika kujifunza. Pengine angekwenda kufundisha. Wakati ule alikwenda Afrika akawa anawasikiliza akina marehemu Babu. Akakaa nao kimya, akiwasikiliza. Akiwauliza maswali.

Sio leo Afrika ya leo. Hata kidogo.

Anonymous 7:40 am  

Mzee Egidio,
swali lako nzuri sana,kweli kujivika U-Malcom sio kazi rahisi inabidi ujitolee kwelikweli na uwe tayari kufa kwa maslahi ya wengine.Robert Nesta Marley aliwahi kusema THE TRUTH IS ALWAYS AN OFFENCE.Lakini Mzee Egidio tutakaa na kuangali tu?mpaka lini?

Mzee Ndesanjo,
uliyosema ni kweli,hebu tuchukulie EAST AFRICA COMMUNITY,kichekesho au sio,Hivi kwanini tunakuwa wagumu kuelewa,hivi kwanini tunapelekwa pelekwa?mimi naona kuliko kuendelea kuishi duniani ni heri mungu anichukuwe mapema,sura za watu ndugu zetu zinahuzunisha jamani,tembea uone,yatima,wajane,wasiojiweza inauma sana unajuwa.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP