Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Chuki

>> Saturday, January 13, 2007

Naipenda chuki
Chuki ambayo ni kiwanja cha upendo
Napenda kuichukia chuki
Nimejengwa na matofari ya kuamini chuki ni chungu, upendo ni utamu
Napenda kuchukia, naaibu kuonyesha chuki
Aibu ya kuonyesha chuki za vipendwavyo
Vipendwavyo vifyonzavyo uhai wa maangavu ya macho yangu
Napenda kupendwa, naogopa kuchukiwa
Asante Chuki
Asante kwa kuangaza upendo
Na Simon Kitururu 13.01.2007

Nakuacha na Nina Simone Leo aendelee kuelezea hisia za Upendo wakati nikiendelea kutafakari mstari mwembamba utenganishao upendo na chuki.

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Anonymous 6:41 pm  

Naam Simon,

Ushairi mzuri sana kwa mada na mtiririko hali kadhalika.

Jana nilijaribu kuandika ushairi wa beti moja kujipima kama bado nina uwezo. Natarajia kuanza kuandika mashairi na hadithi hivi karibuni.

Huyu Shangazi yetu Nina Simone aliumbwa kwa udongo wa aina yake pekee yake. Namuomba Da'Mija amulete kwenye safu ya Wanawake wa Shoka.

Weekend njema,

F M Tungaraza.

Simon Kitururu 9:01 am  

Brother Mtimkubwa , wengi tunasubiri kazi zako.
Asante kwa kupita hapa. Huwa najaribu mara kwa mara kuandika mashairi lakini hii ni mara ya kwanza kuweka shairi langu wazi kwa watu wote kushuhudia. Nashukuru umelipenda!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP