Vita vya Tanzania na Malawi vyaanza!
>> Monday, January 08, 2007
Naombea hili lisije tokea!
Lkini, hivi swala la mpaka wa Malawi na Tanzania limefikia wapi? Najiuliza kutokana na ukweli serikali yetu Tanzania inajulikana kwa kutotafuta majibu ya matatizo kabla tatizo halijakuwa sugu au kutoa makucha.Naona Somalia walipochukua utawala kwa muda mfupi watu wa Mahakama ya Kiislamu, wakaanza kudai sehemu iliyopo Ethiopiaiitwayo Ogaden, waishio Wasomali wengi.Nisikutishe labda Malawi haitapata mtawala atakayedai songea ni Malawi!Sawa basi nimekubali, hata dai Songea , atadai Mtwara tu au sehemu walizopo watu wakabila fulani!
Tukiacha utani;!
Ukisoma habari za Tanzania utakuta mara nyingi zinaongelea matatizo ambayo yameshajitokeza.Mambo ni mengi.Baadhi ni kama haya ya matatizo ya umeme, mafuriko, chakula.....nk. Sababu kubwa mimi naona nikutokuwa na mikakati yenye kuona mbele ambayo inaelezeka.Serikali husemekana ni watu, na watu ni serikali, lakini ndani ya Tanzania serikali ni serikali na watu sharti kuwakimbia polisi.
Dondoo:
Hivi unafikiri ilitatizo la umeme halitatokea tena?
Hivi kama Dar es Salamu mafuriko yanatokea kutokana na sababu zijulikanazo je huko kwingine itakuaje?
Inasikitisha kujua sababu nyingine za mafuriko Dar eti ni kwa sababu Diwani kajenga nyumba kwenye njia ya mfereji wa maji na sababu nyingine kama hizo.
Haya leo hii katika CIA Fact BOOk
Watumia intanet Tanzani nzima hadi kufikia 2005: Watu 333,000
Meli zilizoko Tanzania: Za mizigo tu 1. Za abiria na mizigo 4. Za mafuta 4
Wakimbizi: 443,706 (Burundi). 153,474(Kongo).3,036 (Somalia) makadirio ya 2005
Simu:148,400 za nyumbani kwa makadirio ya 2004. Simu za mkononi 1.942,000(2005)
Kiasi cha gesi ya aslikipatikanacho Tanzania: 22.65 billion cu m (1 January 2002)
Kiasi kitumikacho Tanzania: 0 cu m (2003 est.)
Kiasi cha gesi itengenezwayo Tanzania:0 cu m (2003 est.)
Uhakika kuwa kuna mafuta Tanzania:0 bbl (1 January 2002)
Umeme utengenezwao Tanzania:3.152 billion kWh (2003)
Umeme utumikao Tanzania:2.959 billion kWh (2003)
Umeme Uuzwao nje na Tanzania:0 kWh (2003)
Umeme Ununuliwao na Tanzania:28 million kWh (2003)
Watanzania huishi miaka mingapi:Miaka 45 kwa wanaume.Miaka46 wanawake.Makadirio(2006)
Idadi ya Watanzania kimiaka:
Miaka kati ya 0-14 : 43.7% (wanaume 8,204,593/wanawake 8,176,489)
Hapa kunao ambao watakosa wake.Kasheshe!
Miaka kati ya 15-64: 53.6% (wanaume 9,906,446/wanawake 10,178,066)
Nafikiri ndio maana wengine walipata mke zaidi ya mmoja
Miaka 65 na zaidi: 2.6% (wanaume 422,674/wanawake 557,124) (makadirio ya 2006)
Migogoro ya kimataifa:Tanzania inamgogoro na Malawi kuhusu Ziwa Malawi na Mto Songwe.
Samahani, ziwa Nyasa.
Hivi Ushajiuliza kwanini nchi zote waziitazo zilizoendele zina mchezo wakufuatilia habari za nchi nyingine?Zote zina watafiti waliobobea katika masomo ya nchi nyingine.Hivi Tanzania tunaijua Kenya?
KAMA UNATAKA KUMSHINDA UNAYE MKABILI, MJUE! JE SISI TUNAWAJUA TUNAOKABILIANA NAO JE TUNAJIJUA+
6 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Kiboko, mbona hukutuwekea takwimu ya jeshi na silaha zake za kizamani? Kiasi cha mapato na matumizi yetu? na mengine mazuri pia?
Hivi hawa watu wanafanyia nini takwimu hizi? Wao kujua hayo yanatusaidiaje au kutuumuza vipi?
Inashangaza jinsi wao wanavyotujua na sisi hatuwajui, nadhani tulishajitoa kwenye ushindani wa maendeleo ila tunageresha kama tupo tuu!
Bado nina mawazo mengine, kwenye hii dunia ya kidemokrasia hatuna maadui, tunachotakiwa kujua ni wenzetu wanafanikiwa vipi kiuchumi nasi tufanye njia hizohizo.
Matatizo yetu mengi huwa yanajirudia maana yanapotokea mara ya kwanza, tunashtuka. Kisha yakipita tunasahau. Tatizo la umeme limekuwepo katika uongozi wa marais watatu! Sitashangaa likiendelea kuwepo. Mafuriko Dar nayo kila masika. Viongozi wapo, wahandishi wapo, halmashauri zipo. Nchi inachezewachezewa tu na hawa watu tunaowaita viongozi. Na wanaoongozwa wanaridhishwa na kauli mbiu badala ya vitendo na rekodi zao.
Takwimu za CIA nilikuwa sijazitazama muda mrefu. Ngoja nianze tena kuziangalia na kutafakari jinsi watu wengine wanavyokusanya habari zetu zaidi yetu sisi wenyewe.
Nakumbuka Nyerere aliwahi kutoa hotuba akaongelea jinsi rais wa kwanza wa Malawi, Banda, alivyomwendea na ramani kuukuu akionyesha jinsi ambavyo sehemu ya Tanzania inapaswa kuwa ni nchi ya Malawi. Kuna mwanajeshi mmoja pale Dar alinionyesha ramani mwaka juzi (sikumbuki imechapwa na nani) ikionyesha eneo alilosema Banda likionyeshwa kuwa ni sehemu ya Malawi. Najilaumu kwanini sikuhifadhi nakala ya kalenda ile.
Ndesanjo nimestukia Snap haipigi picha kwenye link ya C.I.C fact book kwenye site yangu.Au ndio hivyo tena kwasababu ndio page ya serikali ya Marekani?
Halafu hawa jamaa wanatusoma kweli.Naamini kabisa haya wanayotuonyesha kwenye kurasa kama hizi ni madogo sana kutoka kwa wanayo yafuatilia kila siku na wanayo yajua.Nauhakika wanaweza wakawa wanajua Hata kama Kikwete alishawahi kuugua kaswende:-)
Meseji ya juu C.I.C nilimaanisha C.I.A.
@Mloyi ,habari zaidi ziko kwenye hhiyo link ya CIA fact book.Niliamua tu kunukuu baadhi kwa kiswahili.
Sikujua kuwa Snap haifanyi kazi kweney tovuti ya majasusi. Hebu nitazame nijionee mwenyewe. Yaani hata picha za tovuti zinazuiwa?
Hawa wanaotupangia mipaka wana mashaka sana! Miaka ile katika atlas hakukuwepo na ziwa Malawi bali ziwa Nyasa, tena mpaka ukionyeshwa kupita kati kati ya ziwa hilo. Lakini katika siku za karibuni ramani nyingi mpya zimekuwa zikionyesha kuwa ziwa Nyasa ni ziwa Malawi huku mpaka wake ukiwa ni kingo za ziwa hilo!
Kwa maneno mengine huko Mbamba Bay wakitembea hatua kidogo kuelekea ziwani watakuwa tayali ndani ya Malawi!
Kwa kweli inasikitisha jinsi ardhi hiyo inavyomegwa!...
Post a Comment