WACHAWI WA TANZANIA MKO WAPI?
>> Saturday, January 27, 2007
Hivi hakuna kanjia kakuuweka uchawi wenu ukawa unatusaidia wote
katika dunia ya sasa?
Je, haiwezekani kuwaloga wamagharibi wakatuletea teknolojia , halafu wakasahau tukaacha kuwalipa?
Mvua je?Wakati wa ukame mbona hamzileti?
Ningependa uchawi utusaidie kusafirisha vyakula nchini kuwafikia wenye njaa kwa kutumia Air Ungo. Ningependa mngesaidia kusafirisha Watanzania kwenda kwenye shule na vyuo babu kubwa vyote, halafu wasome bure bila kuonekana.
Ningependa mgundue kondomu zisizo onekana. Wavalishwe wote wenye mdudu.
Watembee wamezivaa bila kujua.
Mambo yenu ya kutishana nayaona ni nishai!
Mambo yenu ya kurudishana nyuma nayaona ni nishai!
SASA HIVI, NYIE WASHIKAJI MNAFIKIRIA NINI?
HIVI HIYO SAYANSI YENU NI LAZIMA IBAKIE HIVYOHIVYO KARNE ZOTE?
Nauliza tu!
Msiniloge!
Hebu nimwache Jimi Hendrix aachie VOODOO CHILD
1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Uchawi wetu unatumika zaidi katika kuumiza na kutesanatesana. Habari mpya kabisa juu ya uchawi hii hapa chini:
Popobawa atesa watu
2007-01-27 14:27:19
Na Yasmine Protace, PST, Mkuranga
Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Kitonga, Wilaya ya Mkuranga, mkoani Pwani, wamedaiwa kuyakimbia makazi yao baada ya kuvamiwa na popobawa na kuwafanyia mchezo mbaya.
Mwenyekiti wa kijiji hicho, Bi. Toshi Shaha ameiambia PST kwamba popobawa huyo aliingia kijijini hapo tangu Januari 21 mwaka huu.
`Mpaka sasa nina majina ya walioingiliwa na popobawa zaidi ya watu 21 ikiwa ni wanaume na wanawake,`akasema mwenyekiti huyo.
Aidha Bi. Shaha amefafanua kuwa kupatikana kwa orodha hiyo kulitokana na agizo alilotoa popobawa huyo kutaka kila anayefanyia kitendo hicho kujiorodhesha kwenye uongozi wa kijiji.
`Wanasema kila anayefanyiwa mchezo huo anaambiwa lazima atoe taarifa na kwamba asipofanya hivyo, atamrudia tena,` akasema mwenyekiti huyo.
Amesema mpaka sasa wanakijiji wengi wamejawa na hofu ya kuingiliwa na popobawa.
`Wengine wameyakimbia makazi yao ili kuepukana na tishio la popobawa,` akasema.
Amesema ili kutatua tatizo hilo inabidi wapatikane `wataalam' ambao wataweza kupambana na popobawa huyo.
``Tuna wasiwasi bila kufanya hivyo, popobawa huyo atawamaliza wana kijiji wote na kuhamia vijiji vya jirani,'' akasema mwenyekiti huyo.
Naye diwani wa kata ya Kisiju, Kidawa Kiwinga amesema popobawa huyo aliingia kijiji cha Kitonga akitokea kijijini kwao Kisiju.
`Alikuja mwanzoni mwa mwaka huu katika kijiji chetu, na alipokuwa akijaribu kuingia kwenye majumba, watu wanapiga makelele na kukimbia kabla hajadhalilisha watu,`akasema.
SOURCE: Alasiri
Post a Comment