Hivi Unazipenda sehemu za siri za Mwenzio?
>> Friday, January 12, 2007
Samahani ,nimekosea kuuliza. Je, unampenda mwenzio?
Inasemekana ukiwa umependa ubongo wako unaonyesha dalili sawa na mtu mwenye ugonjwa wa akili. Na mchezo mzima ni matokeo ya makemikali ndani ya mwili ambayo yanatabiri unavyojisikia na pia unachotenda.
Je, unampenda huyo mwenzio au ni matokeo tu ya mkorogo wa makemikali ndani yako ambayo huna utawala nayo?
Kuna wataalamu kama huyu Helen Fisher ambaye amebobea katika maswala taaluma ya jinsia ambao wamejaribu kuangalia sayansi ya kupenda.
Yeye anaigawa sanaa hii ya kupenda katika makundi matatu yanayo tawaliwa na kemikali tofautitofauti.
-Uchu(lust)
-Mvuto(attraction)
-Mahuba, (attachment)
Anasema Uchu hutokana na kemikali au homoni testosterone na oestrogen. Testosterone zaidi ni kwa wanaume na hizi homoni ndio zikusababizasho uwe unachekicheki kulia nakushoto kwa apitaye.
Mvuto unatokana na kemikali Dopamine, Norepinephrine ,na Serotonin. zikisaidiwa na neuro-transmitters ziitwazo monoamines. Hapa unaambiwa kuwa Serotin ni muhimu sana katika kupenda lakini ndio ikuleteayo kauchizi kidogo ukipenda kakidudekako
ukapendako. Norepinephrine au adrenalin ndio ikusababishayo kutoka jasho debe na moyo kudunda kama ngoma za Morris Nyunyusa.
Mahuba (attachment) hii husababishwa na na homoni zimwagwazo kutoka katika mfumo wa nevu(nervous system) ziitwazo oxytocin na Vasopressin. Oxytocin hutolewa na glandi iitwayo hypothalamus tokea utotoni. Na pia husaidia wakina mama kutoa maziwa.Hii inasemekana husababisha uhusiano wa karibu kati ya mama na mtoto. Na pia hii inasemekana mwanamme na mwanamke wanapofikia katika kilele cha ngono hutoa au hutoleana hii homoni ikiwa pamoja na chachandu nyingine, hivyo kusaidia mahusiano ya karibu kati ya mwanamke na mwanaume.
Sasa tukiachana na Helen Fisher na machambuzi yake, tunaweza kukubaliana mchezo wa kupenda ni mchanganyiko wa makemikali kibao.Na uhakika haya makemikali aliyoongelea Helen ni baadhi tu na hapo ujachanganya na vindumbwe vingine.
Swali:
Je, kupenda ni aina ya kichaa?
Maana mtu akipenda inasemekana huweza kufanya mambo yaajabu.Tushukuru hatushuhudii kila siku wafanyayo,lambayo, ....nk wapendanao
Dondoo:
Je, unawashangaa wasenge,mabasha, wasagaji nk kwa chaguo la pendo lao?
Usitishike!Wewe kweli unapenda kakitu kako ukapendako. Mimi najiwazia tu hapa bloguni.
Lakini kumbuka kama alivyosema Dr Franklin Tallis kuwa penzi na woga huingilia mlango mmoja.
Swali :
Hivi hizi sehemu za siri ni za siri kweli wakati matokeo ya matumizi yake yako waziwazi namna hii?Hapa nazungumzia watoto bwelele mitaani, ukimwi nk......
Msalimie umpendaye!Wikiendi njema!
7 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Mzee Simon,ajenda ya mwaka mpya ausio naona unakuja na mambo mazito sana,toka mwaka umeanza naona blogu yako inayoa mifano hai na unazidi kuchimbua,safi sana keep it up.Jah live.
Mzee Simon,naomba unisaidie,katika blogu yangu nataka kuweka baadhi ya blogu katika kurasa ya kwanza kama blogu yako.naomba msaada wako.
@Luihamu:Nipe e-mail yako nitakutumia codes na maelezo hapo.Email ulioiandika kwenye blogu yako meseji zina baunsi.
Simon,
TUTAJIE! NANI???????
Ahsante kwa somo la mahaba... siku zote nilikuwa ninahisi kuna aina fulani ya wehu kwenye mahaba.
Mtu akiwa anazengeya huwa anakuwa na mabadiliko sana akikutana na windo lake, saa nyinginewe anabadilisha lafudhi au miondoko... au anapata kigugumizi anaposema, wengine wanasema "anakuwa anajigonga-jigonga" Kumbe zote hizi ni kimekali tu.
Simon, niliwahi kuandika shairi kuhusu topic hii hii. Shairi lenyewe linaitwa Is It Love, Lust or Infatuation. Waweza kulipata hapa - http://www.authorsden.com/visit/viewpoetry.asp?id=137983&AuthorID=28003. Nilichoandika ilikuwa ni wazo langu tu - wengine wanaweza wasikubaliane nalo.
@Sahara: Nimelisoma shairi lako. Mimi nimelikubali. Na asante kwa kunitembelea.
Post a Comment