Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

KAMA bado unashindana na ASIYE asili ya SHINDANO!

>> Sunday, December 21, 2008

Unaweza kujisifia mpaka kumshinda anywaye juisi ya machungwa kwa kuwa UMEKULA MACHUNGWA.

Inawezekana tatizo utibulo kwa kula machungwa , mwenzio uliyemshinda kalitibu kwa kunywa juisi ya machungwa.

Tusipo angalia tutapigana na mesenja wakati asili ya ujumbe ni kwa kibosile tujipendekezaye kwake kwa kumuona ni mtakatifu kwa kuwa anatupa Fanta ya machungwa.

Swali:

  • Si ni kawaida kuwafukuza na kuwalalamikia ombaomba masikini barabarani bila kutatua au kuondoa umasikini barabarani?

Unaweza kushinda kula machenza katika shindano la MSHINDI kupewa Machungwa ingawa tatizo ni ukosefu wa DAGAA.


Na ..
... inasemekana ushindani ni bora kwa sababu huboresha kuwepo kwa watu wenye mbegu nzuri zifaazo kutengeneza bomba la MKE TREKTA.

Wakati unashindana jaribu kukumbuka kuwa labda UNASHINDANA na ALIYESHINDWA.

SHINDANA LAKINI!
Swali:
  • SI ukishinda tutajipendekeza?
  • AU?


NAACHA!

Endelea kidogo na BEEGEES wajaribu kutukumbusha kuwa hai katika STAYING ALIVE..

AU tuendelee tu na MANU DIBANGO.....

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP