Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kwa MWALIMU tishaTOTO!

>> Thursday, December 25, 2008

Umejifunza KUTISHA asikuulize....
...kwa imani akiuliza labda hujui.

Katika jamii ya ujanja kujua...
......yasahaulika mwalimu ni mwanafunzi, na mwanafunzi hajui.

Usingetisha...
....ungehakikisha hujui kwa sababu unajua HUJUI.

Labda..
...ungejiuliza kwanini hujui!

Labda ungejiuliza kwa nini HUJUI.

Yasemekana malaika wa Mungu hawajui ,
.. ndio maana malaika shetani anamjaribu Mungu kwa kuwa hajui.

Lakini kwanini ujiulize...
...ikiwa ukijiuliza haitabadili UKWELI tunajua HUJUI nautabaki hujui?

Sijui , hujui!

Labda...
...Unajua , sijui!


Lakini....
...Kifurahishacho ni nini kama sijui?

..........................._________________------------------------

Naacha!
Nawaza tu hapa mkuu!
Nakutakia mafanikio chooni leo!

Ngojea tujifunze jambo muhimu kama kufungua SIDILIA.....katika How To Undo Her Bra With One Hand...(Usiangalie kama wewe mtoto, padre, sister au utakwazika tu!)



Au tu Tenor Saw anisaidie katika Ring the Alarm....

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Koero Mkundi 1:09 pm  

Kaka kitururu, mimi ni mgeni, nimepita hapa kujitambulisha naipenda sana kazi yako. karibu kwenye kijiwe changu, unisaidie kukiboresha.

ni mimi Koero Mkundi

Simon Kitururu 7:34 pm  

@Dada Koero:Karibu sana Kijiweni na asante kwa kunitembelea. Nitakuja kijiweni kwako bila shaka yoyote na karibu tena na tena!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP