Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Mambo MENGI ni ya KUFIKIRIKA tu!

>> Wednesday, March 14, 2012

Na jinsi UYAFIKIRIAVYO,...
....labda ndivyo UYAJENGEAVYO shepu au hata kuyapa ROHO mambo!

Swali:
  • Kwani unauhakika swala la BINADAMU wana ROHO na KUKU hawana sio swala la kufikirika tu KIAINA?
  • Na ufikiriavyo WENGINE ndivyo wakuonavyo na wakufikiriavyo si unajua kwa kiasi kikubwa LABDA ni swala TU  la KUFIKIRIKA tu?

Kwa HIYO labda kuanzia;...
  • UZURI wa MOYO
  • Ubaya wa SURA ya NGURUWE katika MTU
  • ...mpaka STAREHE zitegemewazo na WALOKOLE /WASWAHILINA  kule MBINGUNI,....
.... bado labda VYOTE ni tofauti katika FIKIRA za MTU na MTU tofauti asiye WEYE,...
... kwa kuwa VYOTE labda ni vidude tu vya KUFIKIRIKA,...
.... na vyaishi zaidi VICHWANI TU mwa WATU zaidi ya kokote kule KWINGINE!:-(

Swali:
  • AU?

Ndio,...
... tokea uzaliwe kuna kiaina unashepu mpaka ,...
... ufikiriavyo JEHANAMU na machungu yake kitu kifanyacho,...
... kuna wafikiriao MBINGUNI lazima kuna MBEGE na UGALI wa MUHOGO,...
... wakati kwa wengine hivyo ni viburudisho vya JELA,...
.... kwa kuwa vyakufikirika vina MAISHA VICHWANI tu MWA WATU,...
... na kila MTU ana KICHWA chake ambacho labda hata aina za chupi kimfikirio HUFIKIRIKA kitofauti YANI.:-(

Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!
Siku njema MKUU!


Hebu A Tribe Called Quest waingilie kati kwa - Jazz(We've Got) &Buggin' Out


Kabla hatujaendelea hebu Anne Kansiime amwage ya -PUBLIC SPEAKING


Au hebu tu Tshala Muana amalizie kwa-Karibu Yangu

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Goodman Manyanya Phiri 8:27 pm  

Binadamu na kuku ni sawa tu, ila sisi, kutokana na uwingi wa akili yetu, tumebuni utu wetu kuliko unyama wa kuku au hata mbu.


Mawazo kama hayo ya usawa wa viumbe ndiyo yanayonifanya niwaheshimu Waislamu niliewaona. Hawamli kuku asiyeombewa kwa Mungu roho yake iwekwe pema peponi!


Chunga sana, siku za karibuni nami nitaSlimu, aiseee!

emu-three 7:28 am  

Mkuu akili ni nywele na kila
mtu ana zake, ....

Mkuu nimeliona neno hapo,nami naomba nisahihishe kidogo inaitwa `WASWAHILINA'...yaani wanaopenda kuswali au kuabudu kwa Waislamu,AU?!

Simon Kitururu 8:52 pm  

@Mkuu GOODMAN: Nakubali kabisa usemalo!
@Ambiere M3:Asante kwa sahihisho. Na nimelifanyia kazi!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

There was an error in this gadget

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP