Tanzania Bwana! Kila kukicha kuna MKOA MPYA umeanzishwa!
>> Friday, March 09, 2012
Usije kushangaa kwenu sio kwenu KIJINA tena,...
... kwa spidi ya jinsi MIKOA inavyoongezeka TANZANIA!
SWALIZ za kizushi:
- Hivi wingi wa MIKOA ni dawa ya suluhisho la maendeleo BONGO?
- Wagawao MIKOA hawahisi labda Tugawe tu na NCHI tuwe na SERIKALi ya visiwa vya MAFIA , yavisiwa vya ZANZIBAR , Visiwa vya UKEREWE na Serikali ya TANGANYIKA Bara?
- Unauhakika unaweza kunitajia MIKOA YOTE ya TANZANIA sasa hivi bila KUJIUMAUMA?
Ndio,...
.... nahisi kuna WATANZANIA kibao,...
...... hawawezitena kunitajia TANZANIA ina mikoa MINGAPI na INAITWAJE.:-(
Ni wazo tu hili MKUU baada ya kustukia ,...
...... MIKOA MINGINE ya Geita, Katavi, Njombe na Simiyu imeongezeka TANZANIA!
4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Mimi ngoja niwe wa kwanza na nisema ukweli kwamba ni kweli mikoa inazaliwa kila asubuhi na wala siwezi kuitaja yote kama nilivyoweza miaka ileeeeeeeeeee
Nafikiri,kunafaida yake,kimaendeleo ukienda mbali zaidi kutaka kujuwa. mimi kwa uhakika nimekuwa mmoja wa waliokumbwa na mabadiriko haya ya kuongeza mikoa. kwanza kabisa nilikuwa mzaliwa katika wilaya iliyo kuwa zamani chini ya mkoa wa Tabora, baada ya serikali kuongeza mikoa nikajikuta tena kwenye mkoa wa Rukwa,mpaka hivi leo kuna mabadiliko te ya wilaya nilio zaliwa ina tenganishwa na kuwa mkoa kamili utakao itwa KATAVI. nikweli unavyosema mtakatifu kama si mfuatiliaji unanaweza kujikuta hujuwi nimkoa upi unatoka. kwamaana hiyo wilaya ya mpanda kuwa mkoa (katavi) kuna faida yake kimaendeleo nimekuwa nafuatilia mchakato mzima,nina uhakika kimaendeleo mkoa huo mpya utasonga mbele sana. namabadiriko yaweza yasiwe natija kwamikoa mingine!. kwa kutaja majina naweza kwa asilimia 90%. kaka s
Hatuwezi kujua nini kitatokea kesho hapa Tanzania...ha ha haiwezekani rais anashauriwa na Mkewe kitandani kesho asubuhi tunasikia jambo...JK Nyerere alipata kusema siku moja na watu wakacheeekaaa!
@ Wote: DUH! Ila Kaka S asante kwa mnyambulisho wako hasa kutokana na migao hii ilivyokugusa moja kwa moja.
Post a Comment