Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

DAKIKA na SEKUNDE ambazo KIBINADAMU hazikumbukwi!

>> Tuesday, July 07, 2009

Dakika azaliwayo MTU,....
......NA sekunde afayo Mtu kwa huyo mtu HAVIKUMBUKWI.

Akuapo mtu kwa udadisi kuna kitu ANAWEZA kukumbushwa,....
.......INGAWA kwa uzoefu wa KIBINADAMU kabla ya kwikwi hua KWIKWI haikumbukwi.


Ndio!

Binadamu uwakutao wanacheka ,....
...... hufanikisha KICHEKO kwakuwa ukali wa maumivu ya kilio HAUKUMBUKWI.

Ndio!

Binadamu msahaulifu HUFIKIRI ,....
......... ni sekunde za makubwa kama KUFA ndio hayajulikani wakati mambo elfu lelaulela hayakumbukwi walakujulikana kama tu KWIKWI?


Ndio!

Dakika azaliwayo MTU,....
......na sekunde afayo Mtu LABDA kwa huyo mtu HAVIKUMBUKWI.

Swali:
  • AU?
  • Unauhakika dakika afayo mtu huwa anajua ndio sekunde HIYO anakufa?
  • Unauhakika aliyefariki anajua kuwa kafa?


DUH!

Ngojea ni muachie marehemu Franco aje na kundi lake katika- MARIO...

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP