Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kama TUKIBOBEA katika kuangalia ALIYEFAULU MTIHANI bado hajui NINI!

>> Friday, July 17, 2009

Ukifeli MTIHANI,....
.. ..waweza kuwa maarufu kwa KUTOKUJUA...

.... ingawa labda uliyefeli ungemfundisha hata aliyetunga MTIHANI ya kuanzia nje ya chumba cha MTIHANI. Au vipi mshikaji!:-(


Ukifaulu MTIHANI,...
.... unaweza mpaka KUJITUTUMUA kwa KUJUA....
.... ingawa labda ungefundishwa KITU usingevimba BICHWA kwa kuwa tu umefaulu MTIHANI.Au vipi mshikaji!


Na TUKIBOBEA katika kumuangalia aliyefaulu MTIHANI,....
... tunaweza kusahau kujifunza KUJUA...
.... ALIYEFELI au kufaulu HIYO haina mpango baada ya MTIHANI kwa kuwa siye wenyewe bado maisha kila wakati yanatupa MTIHANI.Au sio mshikaji?:-(
Swali:
  • AU?
  • Wewe unauhakika umefaulu wa leo MTIHANI?
  • Unakumbuka pia aliyefaulu leo mtihani ukimpa muda anaweza akasahau majibu ya maswali ya huuhuu mtihani wa leo alioufaulu MTIHANI?

NIMEACHA wazo na nakutakia IJUMAA na WIKIENDI NJEMA !
Mola akipenda tutaonana JUMATATU MHESHIMIWA!

Ngojea WAHU adai- Mambo BADO....


AU tu Mwana FA arudie kuwa - BADO NIPONIPO..

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

chib 10:57 am  

Mambo yanakuwa mazito pale hata aliyetunga mtihani huo ukimpa mwaka unaofuatia naye anafeli.

Yasinta Ngonyani 6:55 pm  

Mmmmhhh kazi kwelikweli. Ngoja nisema bado niponipo kwanza:-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP