Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

MUNGU! Wakati bado simuelewi hata BINADAMU ULIYEMUUMBA avaae nguo SIKU HIZI!:-(

>> Friday, July 31, 2009

Nizidishie imani MUNGU,...
....ili nizidi kuelewa imani MUNGU.


Labda nitakuelewa MUNGU,...
.....kama utakavyo tukuelewe MUNGU.

Kwa kuwa wengi watuuziao zisemekanazo ni zako dini MUNGU,...
.....wamekuwa wengi kama zao watuuziazo dini MUNGU.

Na kwa upungufu wetu wa kibinadamu MUNGU,...
... twatoana mpaka DAMU katika kujazia mapungufu ya imani kibinadamu MUNGU.

NI hilo tu MUNGU!


NA ijumaa NA Wikiendi NJEMA kwenu wote WADAU wa BLOGU HII !


Ngojea kiumbe Phil Collins atusaidie kusubiria baadaye kwa kitu- Another day in Paradise


Au tu kijana aliyetutoka Michael Jackson atupe-Man in the Mirror

6 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Fadhy Mtanga 11:59 am  

Tatizo wamezigeuza dini biashara.

Simon Kitururu 2:01 pm  

@Papaa Fadhy: Labda biashara ni dini ndio maana si wote tuna maduka!:-(

Yasinta Ngonyani 5:37 pm  

Amina! Ijumaa na week end njema kwako pia ila usinywe ulanzi mwingi:-)

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) 6:12 am  

...na kila dini (na vizalia vyake) inadai kwamba yenyewe ndiyo inafundisha kikweli juu ya Mungu wa kweli...

Ni kweli "...Tuzidishie imani MUNGU, ili tuzidi kuelewa imani MUNGU..."

Wikendi njema Mwanafalsafa!

chib 11:30 am  

Nimegundua kwa nini wikend hii ilikuwa nzuri sana na yenye amani. Kumbe Kitururu alikuwa ameisha ibariki :-)

Simon Kitururu 4:35 pm  

@Yasinta: :-)

@Profesa: Si utani!:-( Na asante Mkuu!

@Mkuu Chib: :-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP