Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Maswala ya kujiandaa KUWASHWA!

>> Thursday, July 16, 2009

Kama bado HUWASHWI,...
.... shukuru UBONGO kama bado unakumbuka .....

.... huwa unakuna NGOZI lakini ni ubongo ukustuao wapi unawashwa UKIWASHWA.


Na kama bado HUWASHWI,...
....tumia ubongo utakumbuka...
.... mara nyingine si busara kujikuna kipengele kinachowasha UKIWASHWA.


Ingawa kwa wengi hudai ghafla tu bila taarifa hujistukia WANAWASHWA,....
...ni kawaida pia kukumbushwa kukumbuka...
.... kuwa hata kama hutamani kuwashwa sasa hivi, utajikuna vizuri UKIJIANDAA au utastukia labda dawa ni utumbue KIPELE na sio ukikune kwa kuwa UNAWASHWA.

Labda siri ya kujikuna au kujitumbua kistaarabu ni kujiandaa KUWASHWA!:-(

Swali:
  • Wewe kama ni Mkristo si huwa unakumbushwa uwe tayari kila dakika kwa ujio wa Yesu kwa kuwa ukijiandaa unaweza ukapatia sekunde ya kwenda mbinguni kimwanana?

  • Hivi kama leo huwashwi unauhakika umejiandaa KUWASHWA?
  • SI unakumbuka ukijiandaa vizuri hata mtihani mgumu kwako utakuwa rahisi?
  • Hivi unauhakika na maanisha nini hapa?

NAACHA wazo MHESHIMIWA na nakutakia KILA LA KHERI katika SHUGHULI ZAKO au niseme nakutakia SIKU kuku kwa MRIJA kama wewe sio vejeteriani!


Ngojea nitumie tena sauti kurudia kukiri......

5 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 1:15 pm  

Aaa eeh bwana ee sasa basi:-(

chib 1:17 pm  

Fumbo la leo!! Haya mkuu....

Fadhy Mtanga 4:09 pm  

Raha ni kuwa ukiwashwa usijikune mwenyewe kwani huwezi jikuna uzuri. Raha ni kukunwa.

Simon Kitururu 4:15 pm  

@Dada Yasinta +Mkuu Chib: :-)
@Papaa Fadhy: Ukisubiri ukunwe huweziitwa Mvivu?

Au haya ndio mambo yakutosugua vizuri mgongo katika kuuogesha kwa TATIZO la kutofikia vizuri mgongo?:-)

Fadhy Mtanga 7:23 pm  

Hutoitwa mvivu ila utakuwa unaongeza utamu wa kuwashwa na zaidi utakubalika unajua pozi la awashwaye huku akisubiri kukunwa.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP