Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

MPAKA wa MTU!

>> Wednesday, July 08, 2009

Ukizidisha ,....
.... utaumiza MTU.

Ukipunguza,....
....waweza DHARAULIWA na MTU.


Ukizidishiwa,....
.... utaumia kama wewe ni MTU.

Kama unaweza na KINAFANYIKA,...
.... labda BADO hujavuka mpaka wako WEWE kama MTU.

Na kama kuna MPAKA,...
... kumbuka labda HUO umejengwa na MTU.

Kuhusu wewe ni MTU GANI,...
....inategemea na USTUKIAVYO mipaka ya WATU.

Kuhusu WEWE ni NANI,...
... chunguza mipaka YAKO wewe kama MTU.

Na kama kuna UTU,...
......kiutu kuna MIPAKA ya MTU.

KWAHIYO!
CHEZA, cheza kwa STEPU, usimkanyage MWENZIO!

CHEZA, cheza kwa STEPU,..
.. usijeparamia MTU.:-(

Swali:

  • AU?
  • Unakumbuka adui ya mtu pamoja na shetani kusingiziwa bado KWA KAWAIDA ni MTU?

NAACHA WAZO na kumbuka hili ni wazo tu MKUU WA KITENGO!


Ngojea Fela Kuti adai...-Water no get ENEMY


Au tu Stevie Wonder amuongelee- Mista know it all

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Fadhy Mtanga 8:14 am  

Imetulia kama shairi vile!
Sana tu mkuu!

Simon Kitururu 12:52 pm  

@Papaa Fadhy: Asante Mkuu!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP