Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Hata USIPOONA vyaelea LABDA vipo na ukweli ni TAYARI VILISHAUMBWA!

>> Wednesday, July 15, 2009

Usipoona KITU au kustukia moshi unafuka,....
.... SI LAZIMA ni kwamba kitu HAKIPO!:-(


Na ni kweli ni ASILIMIA CHACHE TU YA VITU ndio uistukiayo,....
... ingawa VITU unavipita hata NYUMBANI (Na hapa sizungumzii MABUIBUI!:-() na njiani ndio kabisaa huvioni wakati ukweli ni VIPO.


Hata sasa hivi sehemu ULIYOPO kuna machache tu unayastukia yaliyokuzunguka,....
.... NA kuna uwezekano mpaka jibu la MATATIZO yako hapo pembeni YAKO kidogo tu LIPO.:-(

UNARUHUSIWA KUNIBISHIA MHESHIMIWA!

Swali:
  • Unakumbuka labda leo siku nzima mpaka sasa hivi navyokutonya ulikuwa umesahau kuwa una hata KISOGO ingawa kipo tu nyuma ya kichwa chako?

  • AU?

NI HILO tu kwa leo KINGUNGE!


Hebu tupumzike kwa kuwashuhudia wastaarabu wakiendeleza USTAARABU...

Au ngojea tu MORY KANTE arudie kutuliza majeshi katika kibao - Yeke yeke

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Fadhy Mtanga 7:18 pm  

Mi sikubishii Kingunge Mtakatifu Simon. Halafu inawezekana kuna kitu unatembea nacho everyday lakini hujashtukia tu kuwa kinaharibu malengo ya wengine.
Ama niache mkuu.

Simon Kitururu 1:00 pm  

@Papaa Fadhy: Si utani!:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP