Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Wakati tunaendelea kuangalia UWEZEKANO wa kuwa LABDA suruali ni CHUPI ndefu tu!:-(

>> Saturday, July 25, 2009

Na kabla hatujaangalia hata UWEZEKANO wakuwa KANZU ni GAUNI,...
...labda tukumbuke tulizaliwa UCHI.

Na wakati tunajaribu kujadili wavaavyo WAHUNI,...
.... labda TUKUMBUKE tu achaguaye nguo kwa nia ya zaidi ya KUJISITIRI huyo kashatatua tatizo la KUJISITIRI na kwa staili zake za kuvaanguo usishangae akitembea UCHI.:-(


Na labda ni uhuni,....
....kama sio kujilimbikizia MAVAZI wakati tukifumba macho siye wengine kwa shahuku na IMAJINESHENI labda BADO twakuona uko UCHI.

Na katika madai ya kujitunzia heshima au tu kuonyesha UALIWATANI,...
...Padre mvaa JOHO na SHEKHE mvaa kanzu hata kama jichoni mwako yote ni aina tu ya magauni YA HESHIMA , waweza kosa kazi sehemu ukiwaiga vazi sehemu waungwana waombeazo kazi na suti au tu pale kwa WAUZA MWILI ambapo ujanja ni kutembea UCHI.


Na labda ujanja ni kila sehemu na vazi lake MUUMINI,...
.... lakini ukitimiza hilo la kujali MITINDO YA NGUO labda maana yake NGUO kwako umuhimu wake si TENA kuficha UCHI.

Swali:

  • AU?

NI wazo tu MKURUGENZI na WALA Usitishike!
SIKU NJEMA ALWATANI!


Hebu Talib Kweli anisaidie kidogo kibao-Niggas lie a lot

Au tu Notorious BIG azungumzie tena ya - Big Poppa

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Fadhy Mtanga 2:36 pm  

Kuna wengine hata wavae jeans lakini ukiwatazama lazima imajinesheni ikutume wawapo nekedi.

chib 3:09 pm  

Mada yako imenikumbusha mabadiliko ya asilia (evolution) ya ch*pi za kina dada, zimekuwa zinaenda zikipungua saizi ukilinganisha za enzi za akina Darwin, ufike za enzi za Hitler uendelee mpaka za Mwinyi na sasa aina ya G-stri#g :-(

Yasinta Ngonyani 4:46 pm  

Leo sina cha kusema ila tupo pamoja na tutafika tu!!!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP