Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

UTAAHIRA wa ALIYEPENDEZA!

>> Monday, July 27, 2009

Adhaniaye KAPENDEZA,...
...anaweza akakusumbua HALAFU labda jeuri yote HIYO ni kwakuwa ETI LEO kavaa KIBWAYA.:-(


Na mwenye kutaka KUONGEA kwa VAZI,....
.... kwako ANAWEZA akawa hakutishi KWA KUWA kwako alichovaa ni MIDABWADA hata kama WEWE kama MIMI hatuna uhakika chupi aliyo vaa HAIJAPWAYA.:-(


Na kama UNASIFIWA umependeza,....
.... jaribu KUKUMBUKA ufinyu wa SWALA ZIMA la KUPENDEZA katika DUNIA HII yenye ufinyu wa kujua ni NINI MUHIMU mpaka unaweza fikiri LABDA BINADAMU BICHWA KUBWA na ajazavyo dunia ni UJINGA na LABDA katika kitengo cha BICHWA KUBWA ni kweli ubongo UNAPWAYA.:-(



NI wazo tu MKUU WA KITENGO na wala USITISHIKE!


Swali:
  • Katika swala la BICHWA KUBWA ubongo unapwaya unafikiri najiongelea mimi, wewe au kama kawaida tudai ni YULE?

NARUDIA kuwa hili ni WAZO TU KISHTOBE au MUZEE wa KUPARAMIA !


Ngojea ni muachie mdau Fally IPUPA aongeleee-AssociƩ



Au tu Fally aongelee -Bakanja

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Fadhy Mtanga 4:11 pm  

Mkuu mi sijui bichwa la nani ubongo wake unapwaya. Ahaaa nimekumbuka, ni mabichwa ya mafataki.

Lakini mkuu wa kitengo aliyependeza ni noma, anaweza akakufanya ughairi kwenda bank kudeposit school fees ya mtoto wa ndugu yako, badala yake mguu ukakupeleka shopping mall kumwongezea mapendezo.
Ama mguu ukakupeleka hoteli fulani kwa kitengo cha operesheni maalum.
Aliyependeza usimkadirie pafupi, utauza hadi nyumba ya urithi.

chib 6:14 pm  

:-)

Yasinta Ngonyani 3:35 pm  

Mmmhhh :-(

Simon Kitururu 5:54 pm  

@Wote: :-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP