Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Wakati tuna wasiwasi na HEKIMA za UJINGA wa MWENYE AKILI TIMAMU!:-(

>> Saturday, July 25, 2009

Kumbuka MWENYE akili timamu,...
.... maana yake LABDA TU ni yule atumiaye akili tusiujue ujinga wake ANAOUKWEPA.

Na labda WENYE akili SANA timamu,...
.... NDIO hutumia zaidi akili TUSISTUKIE ukubwa wa asilimia ya ujinga wao WALIOTUFICHA ndio maana hatuujui INGAWA labda bado HAWAJAUKWEPA.


Na katika KUUANGALIA wasiwasi wa KUOGOPA kuonekana wajinga wa wenye akili timamu,...
... mpaka MWENYE AKILI anaweza kusahau kuwa KAMA UNAAKILI huwa unajijua tu UNAAKILI hata wakati unafanya ujinga NA HILO huwezi KULIKWEPA.:-(

Na hakuna mwenye akili timamu,...
.... ambaye hana ujinga na ndio maana VITA YA KUFUTA UJINGA kama UNA AKILI huwezi kamwe KUIKWEPA.

Swali:
  • Unabisha?
  • Unakumbuka kuwa kama mwerevu anajisomea kinamna anakiri kuwa yeye bado MJINGA?
  • Halafu unakumbuka kuwa KUNAUWEZEKANO taahira ndiye hutumia akili sana kuhakikishia UMATI yeye sio MJINGA?
  • Unafikiri mwenye akili huhitaji kukumbushwa anaakili ili atumie akili?

NIMEACHA na NI WAZO tu MHESHIMIWA!

Ngojea Nina Simone abadilishe hali ya hewa kwa kitu- My baby just cares for Me




Au tu James Brown na Lenny Kravitz wakumbushe- Papa's got Brand new BAG


2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Fadhy Mtanga 2:33 pm  

Mi sibishi, ila nashangaa umejuwaje hayo?

Christian Bwaya 4:19 pm  

Mjinga anajua kusema ayajuayo. Mwenye akili, anafaham kusema hata asiyoyajua.

Wongo ni kazi. Mjinga hauwezi, itabainika!

Kudanganya vizuri, inabidi kujua unasema na nani, ulisema nini kabla, na kwa nini unadanganya, kazi ambayo ni ngumu kwa mjinga!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP