Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Pamoja na yote HALI HALISI bado ni SIRI!

>> Wednesday, July 29, 2009

Na kama HALI HALISI,.....
.....isingekuwa ni SIRI labda watu wote wangeshastukia ni nini KITU HALISI!

Ndio!Pamoja na kuwa kufa na njaa NAKO ni HALI HALISI,....
.....na pia wengi WAWASAIDIAO WAFAO NJAA hufanya hivyo kwa kujisadia wenyewe labda KIMSHAHARA wa N.G.O au tu KIKUSUUZA ZAO ROHO wajisikie ni watu wazuri ,na hiyo pia NI HALI HALISI.:-(


Na wakati UNAKUA kihalisi,...
... labda hustukii ukweli kuwa si kweli wazazi wanataka unywe chai na kiporo cha ugali kwa mlenda wa jana kwakuwa labda MSHAHARA wa WAZAZI HAUTOSHI na hiyo ndio HALI HALISI.:-(


Na labda isingekuwa siri HALI HALISI,...
.... ungekuwa unajisikia kufakufa sasa hivi UNGEJUA HALIHALISI kama hali yako halisi sasa hivi haikusikilizishi kufakufa kwa kuwa kwetu sisi ukitukenulia meno tunahisi unafuraha HATA KAMA hiyo kwako si HALI HALISI.

Nalikatiza wazo HALISI,...
... usije mpaka ukaanza kuwastukia ni WATU wangapi hata ukiwaza unaweza kuwahukumu kuwa washadakwa na SHETANI na labda UKWELI NI KWAMBA wako karibu zaidi yako na MUNGU na hiyo ndio HALI HALISI.:-(

Swali:

  • Siriasli unafikiri ni watoto wangapi kwa hali halisi hustukia labda maisha waishiyo ni kwa sababu wazazi wao wamechacha na hiyo ndio hali halisi?

  • Kwa hali halisi unayoifahamu unafikiri ni MARAFIKI zako au ndugu zako wangapi wana UKIMWI au tuseme tu MINYOO na hiyo ndio hali halisi?

  • Unauhakika kuna mtu hata mmoja hapa duniani ajuaye yote kuhusu YAKO hali HALISI?


NAKATIZA WAZO MHESHIMIWA lakini TUKO PAMOJA MKUU!
Hebu twende kidogo UK tukacheki WACHAWI wakiomba kazi na hii ni hali HALISI...



Au tupitie tu Mozambique tukutane na MARIZA adai-Africa Calling[Meu FADO Meu]



Au tubaki tu Mozambique Djaaka adai-Djogoro

5 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 2:18 pm  

Hali halisi:-(

Fadhy Mtanga 7:18 pm  

Ni hali halisi kuwa nimetoka kupika mishemishe mbili tatu, najishtukia hadi kiuno kinauma.

Simon Kitururu 3:33 pm  

@Yasinta: :-)
@Mkuu Fadhy: Duh mpaka umeumiza kiuno?:-)

Mzee wa Changamoto 7:08 pm  

Mmmhhhhhhhhhh! Hali halisi

Simon Kitururu 10:50 pm  

@Papaa Mubelwa: :-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP