Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

IMANI!

>> Tuesday, July 14, 2009

Imani sio DINI,...
... na ukitaka DINI unaweza mpaka KUKUMBUKA ulianza kuishangilia LINI.

Kwa IMANI,....
....ukinuniwa bado unaweza kuamini AKUNUNIAYE baadaye atakuchekea hata kama sasa hivi BADO unampa KWININI.


Imani ni UTAAHIRA na kama unatumia akili mpaka katika maswala ya IMANI,....
..... labda hicho ufanyacho ni SAYANSI na kumbuka ukitumia AKILI swala la DINI halieleweki kama tu IMANI.

Swali:
  • Hivi utaahira si unaoanishwa na mtindio wa kuelewa viletavyo maana kwa wengine KAMA VILE TU kuabudu Mbuyu, Mbuzi, Ng'ombe au tu Mungu Waupendo awezaye yote atakayewaachia binadamu kibao wafanye dhambi ili badaye awape kibano na kuwachoma moto?


NI WAZO tu KINGUNGE wala USITISHIKE!

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 6:20 pm  

kaaziii kwelikweli Imani:-(

Fadhy Mtanga 11:05 pm  

Sijatishika kingunge!

chib 11:32 am  

Imani ni utaahira! Kwa mtazamo wangu Sijakubaliana nawe!

Simon Kitururu 5:36 pm  

@Yasinta: :-)
@Fadhy: :-)
@Chib: Imani inaweza ikawa utaahira kama haieleweki kwa kutumia akili. Utaahira si ni mtindio wa akili unao sababisha binadamu ashindwe kuelewa waelewayo na yaletayo maana kwa wengine?

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP