Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kila mtu ni MWANASIASA!

>> Wednesday, July 22, 2009

Labda wengine katika mchezo wao wa siasa ,...
..... ni kunyoshea wengine kidole kuwa ni WANASIASA.


Labda wengine katika mchezo wa siasa,...
... utaustukia wakiucheza makazini ili wapandishwe cheo huku wakikana wao sio WANASIASA.

Na labda ni USHAHIDI unasiasa,......
.... kama uko chini ya mfumo wa kisiasa na una maoni kuhusu WANASIASA.

Na huwezi kuwa hujaathiriwa na siasa kiasi kwamba huna maoni ya kisiasa,....
.... kama mpaka jina la utaifa wako ujitambulishalo nalo ni tupu LABDA hata za Nyerere SIASA.


Na wanasiasa wengi hawajistukii ni WANASIASA,....
..... kwakuwa siasa zao ni za kufuata wahisiye ni kiongozi katika waaminicho katika SIASA.


Na ndio maana asilimia kubwa ya waitwao wanasiasa,....
..... hawakuhitaji kuiendea shule au labda BADO hawajui ni nini SIASA.


Na katika siasa mpaka za nyumbani nasikia bado BABA ni KICHWA CHA NYUMBA kisiasa,....
.... kama kweli huyo baba hata nyumbani anashinda katika mchezo wa kumchezea akili MAMA na WATOTO wake nyumbani wasistukie kuwa labda siku nyingine BABA ni MKIA wa nyumba KISIASA.

Na labda hata kutongoza ni tupu siasa,....
..... na ukikubaliwa labda ulikubaliwa na ALIYEKUBALI kabla hata hujatongoza na ni kwa KISIASA.:-(

Swali:
  • Unabisha wewe huchezi siasa ingawa hulipwi mshahara kama mwanasiasa?
  • Unauhakika unajua siasa ni nini kabla hujaendelea kukana eti kwa kuwa wewe sio mwizi basi wewe sio Mwanasiasa?
  • Kwani unafikiri ni wanasiasa wangapi wanajua siasa?
Samahani naachia hapa ngojea niende chooni kidogo kutekeleza ZA CHOOO siasa!
BAADAYE Mheshimiwa na kama sio mvivu ENDELEZA tu LIBENEKE kama UKO HAI Mheshimiwa!





Ngojea EN Vogue wawashawishi watu- DOn't let go


Au tu TLC wadai ya -Waterfalls

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Fadhy Mtanga 2:50 pm  

Na unaweza kukataa kuwa wewe si mwanasiasa hata wakati utumiapo propaganda ili kupata kile kinachowachanganya watu wakahonga hata magari.

Simon Kitururu 2:55 pm  

@Papaa Fadhy: Kweli kabisa usemacho!:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP