Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

labda ni WIZI MTUPU!:-(

>> Tuesday, July 28, 2009

Sadaka,...
.... kama ukifuatilia ziendako SADAKA.

Ukweli,...
.... ukifuatilia BAADHI YA NIA za aliyeamua KUKUAMBIA UKWELI.




Kupendeza,....
.... ukifikiria USAHAULISHWAVYO labda aliyependeza bado ananuka MAENEO kwa kuwa tu eti leo KAPENDEZA.


UONGO,...
.... ukifikiria labda umeepushwa kustukia USHALIZWA lakini watembea kifua mbele kwa kutostukia udhaniayo ni kweli karibu yote ni UONGO.


YA WEWE,...
.... kama yanakusahaulisha BINADAMU WOTE tunahusiana kwa kuwa unakazania YA WEWE.


YANGU,...
.... kama yamenisahaulisha twafa twayaacha na labda ukweli ni kwamba DUNIANI hakuna chochote kwa asilimia mia nawezasema si CHAKO na ni CHANGU.


Wizi,....
.....ukikumbuka VINGI VIIBWAVYO havina msaada kwa MWIZI!:-(

DUH!
Swali:
  • Unakumbuka aliyezoea kuiba husahau afanyacho ni WIZI?
NI wazo tu MHESHIMIWA na nakutakia kila lakheri katika SIKU YAKO Mkurugenzi!


Hebu sie wengine tuendelee na THE TRIBE CALLED QUEST katika-Can I kick it



Au tupate tu LAPDANCE kutoka kwa NERD

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 8:21 pm  

Simon:-(

Fadhy Mtanga 10:32 pm  

Ukishtukia unaibiwa na mwimba korasi kwenye operesheni maalum inakuwaje?

Koero Mkundi 8:28 am  

KITURURU, HUMPATI MTU HAPA.......LOL

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP