Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Msichana mzuri a.k.a KIGOLI na Mvulana mwanana a.k.a KIJEBA katika MASHINDANO ya KUZEEKA!

>> Thursday, July 09, 2009

Na ni kweli hata DOGODOGO saizi YAKO,...
.... mpe muda ATAZEEKA.

Lakini angalia SURA LAKO na sikilizia kiuno chako kihimilivyo shughuli ZAKO,...
....wakati umestukia DOGODOGO si SAIZI yako kwa kuwa huvutiwi na Wazee na DOGODOGO kwako KAZEEKA.

Kumbuka!
Wakati DOGODOGO mambo zake DUKINAA katika VIONJO vyako,...
...kuna MZEE awezaye MAMBO ADIMU yenye makali ya ASALI na ukileta ZA kuleta ANAKATIKA na kupakua HAJAZEEKA.

Na kama ni KIGOLI kwa haraka AZEEKA kama nyanya kwenye kachumbari YAKO,...
.... jiulize ni kwanini KIJEBA hufa kwanza kabla ya KIGOLI aleZEEKA.

Ni swala tu la MUDA hata WAKO,...
... aringaye kama tu ASIYERINGA wote WAZEEKA.

Ni swala la MUDA tu hata WAKO....
... umjuaye kwa UTOTO bila kujali UKE wala wake UUME, ataZEEKA.:-(


Ringa MWANAWANE onyesha maringo YAKO,...
... kwani punde si utani UTAZEEKA.

Kumbuka hakuna mbaya kwa KUZEEKA kama ULIVYO mtazamo WAKO,...
... ila hata kama UNACHAKURINGIA, waweza kukosa nguvu za kuringa UKIZEEKA.

Na mwenye HOFU YA KUZEEKA na kama huo ni uoga WAKO,...
... kumbuka INA maana unashughuli chache na umezidiwa na muda wa KUFIKIRI wakati huu UKIZEEKA.


Swali:
  • Unakumbuka SASA HIVI unaendelea KUZEEKA?
  • Ushawahi kusikia ni wanawake wazeekao haraka?
  • Na hivi unajua TAKWIMU zadai ni WANAUME wafao MAPEMA kwa uzee?


Ni wazo tu WAZIRI wa mambo ya GHAFLA na STAREHE NDOGONDOGO , na wala USITISHIKE!


Ngojea JERREMIAH abadili hali ya hewa kwa kibao- Birthday SEX

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP