Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Tuangalie tena SWALA ZIMA la kuhalalisha KUFANYA MATUSI ili iwe ni TENDO LA NDOA.

>> Thursday, July 30, 2009

[Tahadhari: stori hii haikufai kama mtoto au hujawahi kufanya matusi!]


NI binadamu na wala si tu BINAMU ambaye kwa binadamu ni nyama ya HAMU,...
....na hamu ni zilezile ingawa hutofautiana tu pale HAMU zinaposuuzwa kwa VITENDO.:-(


NA kufanya matusi ni kitendo KILEKILE kiletwacho na HAMU,...
...na inasemekana ni haramu na uhalalisho hutofautiana jamii MPAKA jamii kwa VITENDO.


NA wakati jamii ya leo NI kama ILEILE ya jana yenye HAMU,...
....kifikira uhalalisho wa leo wa kufanya matusi umezoeleka MPAKA jamii haina uhakika watofauti ya matusi na CHA NDOA KITENDO.


Na siku hizi kukutana na bikira ni nadra hata kama una hiyo HAMU,...
...na sasa katika jamii bikira ni yule ambaye hujafanya naye matusi kabla na sasa mfanyacho ni CHA NDOA KITENDO.

NA kumbuka siku hizi NI HATARI hata kama ni kweli UNAHAMU,...
...jamii imebadilika mpaka WENGI waliofunga ndoa wafanyacho bado ni MATUSI kwa kushindwa kutofautisha utamu wa MATUSI na THAWABU za CHA NDOA KITENDO.

Na kumbuka UTAPIGIWA makofi SIKU YA NDOA hata na boyfriend wa mke wako mwenye ya mke wako HAMU,...
....na wewe MWENYEWE na labda BADO waingia chumbani kufanya YALEYALE ila leo kwa kuwa ni ruksa ufanyacho chaitwa CHA NDOA KITENDO.


NA yasemekana KITANDA HAKIZAI HARAMU hata kama wakati unakula URODA kuzaa mtoto huna HAMU,...
..... na kumbuka hata kama mimba si yako mtoto asipofanana na wewe basi kafanana na MPWA WAKE Moshi MAJENGO au tu babu mzaa babu wa upande wauliyefanyanaye KITENDO.


DUH Nalikatiza wazo hili NUKSI na Shenzi Taipu!

Kumbuka ni wazo tu !

Swali:
  • Unafikiri ni ASILIMIA NGAPI katika jamii ya leo hualalisha MATUMIZI YA KITENGO kabla ya kuhalalishwa kitendo?
  • Hivi ni baraka na pete kweli ndio hugeuza kufanya matusi liwe tendo la ndoa?
  • Hivi si labda tendo la ndoa ni matusi tu katika jamii isiyojua ndoa?
  • Unafikiri ndoa sio AINA YA UBAHIRI WANGU wakutaka yangu iwe yangu PEKE YANGU na nyie wengine msinionjee?

Basi bwana nakupa siri nyingine kuwa sababu ya kuacha topiki hiii ni kwa sababu IMENISHINDA labda ndio maana unaweza ukakuta WAJANJA swala hili kwao Mtaalamu hata wa KONDOMU au tu NDOA eti ni Padre au PAPA wa ROMA ambao wote isemekanavyo hawajawahi kuonja MATUSI wala CHA NDOA KITENDO. HALAFU eti malaya mjuzi wa swala na aliyeshindwa ndoa kadhaa hasikilizwi akiongelea SOMO!:-(

Kwa mara nyingine NAACHA!
SIKU NJEMA MHESHIMIWA!
Na BWANA na BIBI WASIFIWE!

Au tuangalie hawa jamaa wanaopenda kufanya tendo la ndoa na WANYAMA katika-Two Women Describe Losing Their Virginity To a DOG!!


Au tu nimrudie Omar Kopa aongelee-UNYAGO




...

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 5:30 pm  

Somo la leo ni kali kaka Simon!!

Masangu Matondo Nzuzullima 7:40 pm  

Ni kweli somo la leo ni kali...kwa mbali sana limenikumbusha jinsi majina ya nywele yanavyobadilikabadilika kutegemeana na sehemu ya mwili zilipoota - ndevu, masharubu, nyusi,...lakini zote si ni nywele tu?

Simon Kitururu 1:57 pm  

@Dada Yasinta!Duh!
@Prof :Kazi kweli kweli!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP