Friday, July 31, 2009

MUNGU! Wakati bado simuelewi hata BINADAMU ULIYEMUUMBA avaae nguo SIKU HIZI!:-(

Nizidishie imani MUNGU,...
....ili nizidi kuelewa imani MUNGU.


Labda nitakuelewa MUNGU,...
.....kama utakavyo tukuelewe MUNGU.

Kwa kuwa wengi watuuziao zisemekanazo ni zako dini MUNGU,...
.....wamekuwa wengi kama zao watuuziazo dini MUNGU.

Na kwa upungufu wetu wa kibinadamu MUNGU,...
... twatoana mpaka DAMU katika kujazia mapungufu ya imani kibinadamu MUNGU.

NI hilo tu MUNGU!


NA ijumaa NA Wikiendi NJEMA kwenu wote WADAU wa BLOGU HII !


Ngojea kiumbe Phil Collins atusaidie kusubiria baadaye kwa kitu- Another day in Paradise


Au tu kijana aliyetutoka Michael Jackson atupe-Man in the Mirror

Kwa waogopao MDUDU bila kuogopa LISILO na macho DUDU!:-(

Wapo wapendao kukwaa kwa kionjeo DUDU,...
.... na inasikitisha KWAKUWA inasemekana ndio wengi wapatao MDUDU!:-(


Eti hawaogopi DUDU,...
... kwa kuwa katika SHUGHULI walikubuhu tokea shule ya VIDUDU.:-(


Eti wengine ni MADUME WAZIMA ambao wana DUDU,...
... lakini eti ni kweli NAO wajisikia angalau kwa nyuma kupewa DUDU.:-)


Na siwajaji hawa madume WAPENDA DUDU wenye DUDU,...
.... kwa kuwa yao SIYAJUI VIZURI na jamii yenyewe imefanya wengi wao wajifiche ambao labda ni wetu tuwaheshimuo na si kwa kuogopa MDUDU.


Lakini kumbuka likimtemea mtu DUDU,...
...wapo wadaio hunyonya ENEO kama embe sindano,...
.... wakiamini huathiriki kwa KUNYWA togwa yake hata kama kokwa lina MDUDU.:-(

Wengine KIDUDE waringishia wenye DUDU,....
..... wasahau kuwa hata kama kuna vizuia MZALISHO labda bado HIVYO havizuii MDUDU.

Lakini ni chaguo lako mpenda DUDU,....
.... lakini JUA tu wakati unachekelea dudu, kuna MDUDU!:-(

TUNAKUMBUSHANA TU MHESHIMIWA na wala sileti za KULETA!:-(
Swali:
  • AU?
  • Hivi bado SI unakumbuka kuna UKIMWI a.k.a MDUDU mdau HATA wakati unacheza nayo?
NI HILO TU!:-(


Ngojea Cristofer a RANT kuhusu ambacho katika malezi sijui kama kinatokea bado Bongo katika-Purity Ball and Promise Ring..

Au tu KINGWENDU FAMILY warudie -Huyu DEMU MAPEPE..

Thursday, July 30, 2009

Tuangalie tena SWALA ZIMA la kuhalalisha KUFANYA MATUSI ili iwe ni TENDO LA NDOA.

[Tahadhari: stori hii haikufai kama mtoto au hujawahi kufanya matusi!]


NI binadamu na wala si tu BINAMU ambaye kwa binadamu ni nyama ya HAMU,...
....na hamu ni zilezile ingawa hutofautiana tu pale HAMU zinaposuuzwa kwa VITENDO.:-(


NA kufanya matusi ni kitendo KILEKILE kiletwacho na HAMU,...
...na inasemekana ni haramu na uhalalisho hutofautiana jamii MPAKA jamii kwa VITENDO.


NA wakati jamii ya leo NI kama ILEILE ya jana yenye HAMU,...
....kifikira uhalalisho wa leo wa kufanya matusi umezoeleka MPAKA jamii haina uhakika watofauti ya matusi na CHA NDOA KITENDO.


Na siku hizi kukutana na bikira ni nadra hata kama una hiyo HAMU,...
...na sasa katika jamii bikira ni yule ambaye hujafanya naye matusi kabla na sasa mfanyacho ni CHA NDOA KITENDO.

NA kumbuka siku hizi NI HATARI hata kama ni kweli UNAHAMU,...
...jamii imebadilika mpaka WENGI waliofunga ndoa wafanyacho bado ni MATUSI kwa kushindwa kutofautisha utamu wa MATUSI na THAWABU za CHA NDOA KITENDO.

Na kumbuka UTAPIGIWA makofi SIKU YA NDOA hata na boyfriend wa mke wako mwenye ya mke wako HAMU,...
....na wewe MWENYEWE na labda BADO waingia chumbani kufanya YALEYALE ila leo kwa kuwa ni ruksa ufanyacho chaitwa CHA NDOA KITENDO.


NA yasemekana KITANDA HAKIZAI HARAMU hata kama wakati unakula URODA kuzaa mtoto huna HAMU,...
..... na kumbuka hata kama mimba si yako mtoto asipofanana na wewe basi kafanana na MPWA WAKE Moshi MAJENGO au tu babu mzaa babu wa upande wauliyefanyanaye KITENDO.


DUH Nalikatiza wazo hili NUKSI na Shenzi Taipu!

Kumbuka ni wazo tu !

Swali:
  • Unafikiri ni ASILIMIA NGAPI katika jamii ya leo hualalisha MATUMIZI YA KITENGO kabla ya kuhalalishwa kitendo?
  • Hivi ni baraka na pete kweli ndio hugeuza kufanya matusi liwe tendo la ndoa?
  • Hivi si labda tendo la ndoa ni matusi tu katika jamii isiyojua ndoa?
  • Unafikiri ndoa sio AINA YA UBAHIRI WANGU wakutaka yangu iwe yangu PEKE YANGU na nyie wengine msinionjee?

Basi bwana nakupa siri nyingine kuwa sababu ya kuacha topiki hiii ni kwa sababu IMENISHINDA labda ndio maana unaweza ukakuta WAJANJA swala hili kwao Mtaalamu hata wa KONDOMU au tu NDOA eti ni Padre au PAPA wa ROMA ambao wote isemekanavyo hawajawahi kuonja MATUSI wala CHA NDOA KITENDO. HALAFU eti malaya mjuzi wa swala na aliyeshindwa ndoa kadhaa hasikilizwi akiongelea SOMO!:-(

Kwa mara nyingine NAACHA!
SIKU NJEMA MHESHIMIWA!
Na BWANA na BIBI WASIFIWE!

Au tuangalie hawa jamaa wanaopenda kufanya tendo la ndoa na WANYAMA katika-Two Women Describe Losing Their Virginity To a DOG!!


Au tu nimrudie Omar Kopa aongelee-UNYAGO




...

Nikome BABU WEE! Mie SILI KWAKO!:-(

Na labda ni vizuri huli KWANGU,...
.....labda unajitegemea.

Na labda kuwa na wasiwasi kwa kuwa sili KWAKO,...
....labda sikuhitaji!:-(


Na tuwe na wasiwasi wa afya ya jamii kama imefikia tunawaza kuwa NANI ala KWA NANI,...
....labda maana yake jamiii IMEZIDIWA MUDA WA MAJUNGU na KAZI inahitaji .

Na tuwe na wasi wasi kama sijali yako kwa kuwa si YANGU,...
...labda maana yake hujali pia YANGU kwa kuwa una YAKO na kama ni kweli kujifunza UTU tunahitaji!:-(

Swali:
  • Nani kakwambia usiwe na wasiwasi kwa kuwa sili kwako?
  • Huwa ni kawaida kwako kuoanisha WASIWASI na MLO a.k.a KUPIGA TONGE?

NIWAZO TU KIJEBA wala usiwashwe!

Hebu twende tena Cape Verde kukutana na Lura alete-Na ri NA


Au tubaki tu Afrika hapahapa Cape Verde Calu de Brava adai-Terra Love

Wednesday, July 29, 2009

Pamoja na yote HALI HALISI bado ni SIRI!

Na kama HALI HALISI,.....
.....isingekuwa ni SIRI labda watu wote wangeshastukia ni nini KITU HALISI!

Ndio!Pamoja na kuwa kufa na njaa NAKO ni HALI HALISI,....
.....na pia wengi WAWASAIDIAO WAFAO NJAA hufanya hivyo kwa kujisadia wenyewe labda KIMSHAHARA wa N.G.O au tu KIKUSUUZA ZAO ROHO wajisikie ni watu wazuri ,na hiyo pia NI HALI HALISI.:-(


Na wakati UNAKUA kihalisi,...
... labda hustukii ukweli kuwa si kweli wazazi wanataka unywe chai na kiporo cha ugali kwa mlenda wa jana kwakuwa labda MSHAHARA wa WAZAZI HAUTOSHI na hiyo ndio HALI HALISI.:-(


Na labda isingekuwa siri HALI HALISI,...
.... ungekuwa unajisikia kufakufa sasa hivi UNGEJUA HALIHALISI kama hali yako halisi sasa hivi haikusikilizishi kufakufa kwa kuwa kwetu sisi ukitukenulia meno tunahisi unafuraha HATA KAMA hiyo kwako si HALI HALISI.

Nalikatiza wazo HALISI,...
... usije mpaka ukaanza kuwastukia ni WATU wangapi hata ukiwaza unaweza kuwahukumu kuwa washadakwa na SHETANI na labda UKWELI NI KWAMBA wako karibu zaidi yako na MUNGU na hiyo ndio HALI HALISI.:-(

Swali:

  • Siriasli unafikiri ni watoto wangapi kwa hali halisi hustukia labda maisha waishiyo ni kwa sababu wazazi wao wamechacha na hiyo ndio hali halisi?

  • Kwa hali halisi unayoifahamu unafikiri ni MARAFIKI zako au ndugu zako wangapi wana UKIMWI au tuseme tu MINYOO na hiyo ndio hali halisi?

  • Unauhakika kuna mtu hata mmoja hapa duniani ajuaye yote kuhusu YAKO hali HALISI?


NAKATIZA WAZO MHESHIMIWA lakini TUKO PAMOJA MKUU!
Hebu twende kidogo UK tukacheki WACHAWI wakiomba kazi na hii ni hali HALISI...



Au tupitie tu Mozambique tukutane na MARIZA adai-Africa Calling[Meu FADO Meu]



Au tubaki tu Mozambique Djaaka adai-Djogoro

Swala zima la KUANZA UPYA!

Kwanza,...
.... ukiamka tu kuna uwezekano hakuna UJANJA zaidi ya kulazimika kuanza UPYA.:-(


Pili,...
....kama ulijaribu na kuumia KWA KUKATA TAMAA inaweza ikawa ni KUKATA TAMAA unako KUANZISHA UPYA:-(

Tatu,...
.... labda ni kweli safari iliyopita NANIHII ilikosewa kama hutaki kukiri uwezekano kuwa ULIKOSEA,.........................
....SASA kwa nini usijiunge nami Mtakatifu Simon Kitururu /Muzee wa Kukosea TUANZE UPYA?

Nne,...
..... kumbuka hata kama ulipatia jana hiyo ilikuwa JANA leo mchezo hata uleule ni MPYA.:-(

Swali:
  • AU unasemaje katika swala zima la katika maisha ,TUANZE UPYA au TUKATE TAMAA?


NIMEACHA wazo halafu SAMAHANI KIDOGO MHESHIMIWA naenda kukojoa KIDOGO!:-(


Unaweza kumsikiliza Peter Tosh akikumbusha katika - Pick Myself UP

STAREHE za watu za kuumiza roho MTU!:-(

Labda ni ubinadamu kwa binadamu kuwa na hamu ya kuumiza MTU!

Na kiubinadamu kuna mtu anahalalisha ni nani marafiki na nani maadui hata katika kuchagua wa kumuumiza MTU!

Cha ajabu hata undugu tukiachia mbali urafiki waweza ukawa ndio uletao nafasi ya mtu kuumiza MTU.


Ni vizuri kukumbuka tu,...
.....MKUKI kwa nguruwe unaumiza hata nguruwe ingawa kuna mtu hutaka kuhalalaisha ya mkuki kuwa mchungu tu kwa MTU.

Swali:
  • AU?
  • Hivi ukijisachi kumoyo hautakuta angalau chembechembe za nyege za kutaka kuumiza MTU roho?


Ni wazo tu MUZEE WA KUPEKECHA na wala USITISHIKE!

Hebu Fatboy SLim abadili hali ya hewa kwa kitu-Praise You


Au tu FAT man Scoop amalizie kwa-Put Ur Hands UP

Tuesday, July 28, 2009

Haloo mpenzi NATAKA SITAKI, sogea basi ili NISIJE anza mpaka FIKIRIA jinsi ya KUKUDANGANYA mpenzi!

[Tahadhari:sina uhakika na maudhui ya topiki hii leo mawazoni endelea kuisoma kwa uamuzi wako tu mi sikushiki KIBINDO uisome!:-(]

Kwa Mpenzi TAMUTAMU,....

Najua NIA yangu UNAIJUA,....
... ingawa NAHISI wadhani ni ustaarabu kwako nihahe kwanza kwa kuwa hutaki tupitie NJIA YA MKATO.


Sogea basi mpenzi kivulini ili tusiungue JUA,....
.... na unavyochukua muda nashindwa mwenzio kuacha KULIANDAA NENO ili angalau USINIJIBU KWA MKATO.


Kumbuka mpenzi INACHOSHA ukiringiwa sana na nahisi hilo UNAJUA,....
.... kumbuka hata samaki siwapendi na unanifanya katika kwako kujipendekeza nimeanza kumsifia mpaka SATO.

Na ukizidisha NATAKA SITAKI unajua,...
...siku hizi kuna wafanyao kisasi kwa kukupata wakati waliacha kukutaka na hapa siongelei KIDALI -PO.


Kama hunitaki Mpenzi unajua,...
.... si vizuri kunifanya nihahe wakati wangu udhaifu waujua naKIRI kama wajua hutaki kunigawia kitamutamu KIPATO.


Ushaniingiza DHAMBI unajua,...
....au wataka nianze kutubu wakati kitendo chenyewe ni penzi na ni penzi tu lifanyalo udhani nina MCHECHETO.

NTAKUDANGANYA unajua,...
.... lakini kwanini nikudanganye wakati nina uhakika ukijua ukweli UTAJUA nachokuandalia ni zaidi ya KITO?


DUH naacha WAZO halafu hapa NAKIRI simuongelei yoyote maalumu zaidi ya leo kuingiwa hili wazo baada ya KUSHUHUDIA jamaa likimwaga kauli!


Swali:
  • Hivi ukimpata mpenzi kwa njia za uongo maana yake penzi lenyewe ni la uongo?

  • Unauhakika hujadanganya katika kumlenga mtu hata kwa kujipodoa wakati chini ya kipodozi ngozi mbaaaaya?

DUH NAACHA na ni wazo tu MKUU WA MASWALA KUMBUKA!


Ngojea EDDY MURPHY naye aongelee wake mtazamo katika-CHEATING[Tahadhari : Lugha chafu na labda si stori ya watoto kuchungulia katika mila fulani!Hapa na maanisha kama mtoto au utakwazika sikushauri ucheki kideo hiki!:-(]



Au tu Simply Red wadai- If U don't know me by NOW..

labda ni WIZI MTUPU!:-(

Sadaka,...
.... kama ukifuatilia ziendako SADAKA.

Ukweli,...
.... ukifuatilia BAADHI YA NIA za aliyeamua KUKUAMBIA UKWELI.




Kupendeza,....
.... ukifikiria USAHAULISHWAVYO labda aliyependeza bado ananuka MAENEO kwa kuwa tu eti leo KAPENDEZA.


UONGO,...
.... ukifikiria labda umeepushwa kustukia USHALIZWA lakini watembea kifua mbele kwa kutostukia udhaniayo ni kweli karibu yote ni UONGO.


YA WEWE,...
.... kama yanakusahaulisha BINADAMU WOTE tunahusiana kwa kuwa unakazania YA WEWE.


YANGU,...
.... kama yamenisahaulisha twafa twayaacha na labda ukweli ni kwamba DUNIANI hakuna chochote kwa asilimia mia nawezasema si CHAKO na ni CHANGU.


Wizi,....
.....ukikumbuka VINGI VIIBWAVYO havina msaada kwa MWIZI!:-(

DUH!
Swali:
  • Unakumbuka aliyezoea kuiba husahau afanyacho ni WIZI?
NI wazo tu MHESHIMIWA na nakutakia kila lakheri katika SIKU YAKO Mkurugenzi!


Hebu sie wengine tuendelee na THE TRIBE CALLED QUEST katika-Can I kick it



Au tupate tu LAPDANCE kutoka kwa NERD

Monday, July 27, 2009

UTAAHIRA wa ALIYEPENDEZA!

Adhaniaye KAPENDEZA,...
...anaweza akakusumbua HALAFU labda jeuri yote HIYO ni kwakuwa ETI LEO kavaa KIBWAYA.:-(


Na mwenye kutaka KUONGEA kwa VAZI,....
.... kwako ANAWEZA akawa hakutishi KWA KUWA kwako alichovaa ni MIDABWADA hata kama WEWE kama MIMI hatuna uhakika chupi aliyo vaa HAIJAPWAYA.:-(


Na kama UNASIFIWA umependeza,....
.... jaribu KUKUMBUKA ufinyu wa SWALA ZIMA la KUPENDEZA katika DUNIA HII yenye ufinyu wa kujua ni NINI MUHIMU mpaka unaweza fikiri LABDA BINADAMU BICHWA KUBWA na ajazavyo dunia ni UJINGA na LABDA katika kitengo cha BICHWA KUBWA ni kweli ubongo UNAPWAYA.:-(



NI wazo tu MKUU WA KITENGO na wala USITISHIKE!


Swali:
  • Katika swala la BICHWA KUBWA ubongo unapwaya unafikiri najiongelea mimi, wewe au kama kawaida tudai ni YULE?

NARUDIA kuwa hili ni WAZO TU KISHTOBE au MUZEE wa KUPARAMIA !


Ngojea ni muachie mdau Fally IPUPA aongeleee-Associé



Au tu Fally aongelee -Bakanja

SABABU za KUMPENDA msichana MZURI halafu unajua ni MJINGA!{Samahani : NI katika KIUME point of VYUU!:-(]

Mwanamke MWEREVU labda anaweza kukukumbusha MAMA YAKO!:-(


Halafu MWANAMKE mwerevu na ana MIAKILI KEDEKEDE ukileta za kuleta anaweza KUKUNYIMA na akajazia shughuli kwa kukutukania mpaka MAMA YAKO!:-(


Swali:
  • Kwani ni kweli wakati unashughulikia YA UNYUMBA wewe mwenye akili ni kweli UNAFIKIRI huwa UNATUMIA AKILI SANA?

NIMEACHA wazo !


Hebu twende tena KAMERUNI kukutana tena na Richard Bona aninyanyase tena-



Au tu tubakie tu tena KAMERUNI Manu DIbango aendeleze kuninyanyasa katika kitu-NEW BELL

ASANTENI WADAU WOTE pamoja na hawa ambao HAWAKUNITENGA juzi ya jana!:-(



Photobucket



Photobucket



Photobucket



Photobucket


Photobucket



Photobucket




Photobucket








Photobucket



Photobucket


Photobucket




Photobucket




Photobucket









Photobucket




Photobucket



Photobucket







Photobucket



Photobucket



Photobucket








Photobucket





Photobucket




Photobucket




Photobucket



Photobucket



Photobucket



Photobucket









Photobucket



Photobucket



Photobucket



Photobucket




Photobucket




Photobucket




Photobucket






Photobucket




Photobucket





Photobucket



Photobucket




Photobucket




Photobucket



Photobucket






Photobucket














Photobucket







Photobucket



Photobucket



Photobucket




Photobucket

Saturday, July 25, 2009

Wakati tunaendelea kuangalia UWEZEKANO wa kuwa LABDA suruali ni CHUPI ndefu tu!:-(

Na kabla hatujaangalia hata UWEZEKANO wakuwa KANZU ni GAUNI,...
...labda tukumbuke tulizaliwa UCHI.

Na wakati tunajaribu kujadili wavaavyo WAHUNI,...
.... labda TUKUMBUKE tu achaguaye nguo kwa nia ya zaidi ya KUJISITIRI huyo kashatatua tatizo la KUJISITIRI na kwa staili zake za kuvaanguo usishangae akitembea UCHI.:-(


Na labda ni uhuni,....
....kama sio kujilimbikizia MAVAZI wakati tukifumba macho siye wengine kwa shahuku na IMAJINESHENI labda BADO twakuona uko UCHI.

Na katika madai ya kujitunzia heshima au tu kuonyesha UALIWATANI,...
...Padre mvaa JOHO na SHEKHE mvaa kanzu hata kama jichoni mwako yote ni aina tu ya magauni YA HESHIMA , waweza kosa kazi sehemu ukiwaiga vazi sehemu waungwana waombeazo kazi na suti au tu pale kwa WAUZA MWILI ambapo ujanja ni kutembea UCHI.


Na labda ujanja ni kila sehemu na vazi lake MUUMINI,...
.... lakini ukitimiza hilo la kujali MITINDO YA NGUO labda maana yake NGUO kwako umuhimu wake si TENA kuficha UCHI.

Swali:

  • AU?

NI wazo tu MKURUGENZI na WALA Usitishike!
SIKU NJEMA ALWATANI!


Hebu Talib Kweli anisaidie kidogo kibao-Niggas lie a lot

Au tu Notorious BIG azungumzie tena ya - Big Poppa

Wakati tuna wasiwasi na HEKIMA za UJINGA wa MWENYE AKILI TIMAMU!:-(

Kumbuka MWENYE akili timamu,...
.... maana yake LABDA TU ni yule atumiaye akili tusiujue ujinga wake ANAOUKWEPA.

Na labda WENYE akili SANA timamu,...
.... NDIO hutumia zaidi akili TUSISTUKIE ukubwa wa asilimia ya ujinga wao WALIOTUFICHA ndio maana hatuujui INGAWA labda bado HAWAJAUKWEPA.


Na katika KUUANGALIA wasiwasi wa KUOGOPA kuonekana wajinga wa wenye akili timamu,...
... mpaka MWENYE AKILI anaweza kusahau kuwa KAMA UNAAKILI huwa unajijua tu UNAAKILI hata wakati unafanya ujinga NA HILO huwezi KULIKWEPA.:-(

Na hakuna mwenye akili timamu,...
.... ambaye hana ujinga na ndio maana VITA YA KUFUTA UJINGA kama UNA AKILI huwezi kamwe KUIKWEPA.

Swali:
  • Unabisha?
  • Unakumbuka kuwa kama mwerevu anajisomea kinamna anakiri kuwa yeye bado MJINGA?
  • Halafu unakumbuka kuwa KUNAUWEZEKANO taahira ndiye hutumia akili sana kuhakikishia UMATI yeye sio MJINGA?
  • Unafikiri mwenye akili huhitaji kukumbushwa anaakili ili atumie akili?

NIMEACHA na NI WAZO tu MHESHIMIWA!

Ngojea Nina Simone abadilishe hali ya hewa kwa kitu- My baby just cares for Me




Au tu James Brown na Lenny Kravitz wakumbushe- Papa's got Brand new BAG


Hivi BLOGU ni NINI?

Swali:

  • Unakumbuka?



Au tu Gil Scot Heron akumbushe- The revolution will not be Televised


Au tu Grandmaster Flash & The furious Five walete-The Message

Friday, July 24, 2009

Udhaifu wa hotuba NZURI kama tu MAHUBIRI MAZURI!

Hotuba nzuri LABDA haina cha zaidi,....
.... kwa kuwa HAKUNA cha zaidi kikumbukwacho ZAIDI YA KUWA hotuba ilikuwa nzuri .

UNAWEZA kunibishia zaidi,....
...lakini YALIYOMO kwenye hotuba huwa hayakumbukwi hata kama mazuri.

NDIO!
Labda Hotuba ni maneno tu na hakuna cha zaidi,....
.....na kama kungekuwa na cha zaidi mbona HATUJIFUNZI hayo mazuri kutoka kwenye HIZO zidaiwazo NI hotuba NZURI?
Swali:
  • Pamoja na hotuba au mahubiri mabaya kudaiwa kuwa huwa hayakumbukwi, unafikiri ni nani anakumbuka hotuba nzuri?
  • Unafikiri huwa unakumbuka asilimia ngapi ya yaliyomo hata kwenye kitabu udaicho ni kizuri?
Kuna hawa WATU wako mawazoni mwangu leo na labda YALIYOMO katika waongeacho hakuna chochote cha zaidi ndio maana huwa hatukumbuki waliongea nini mara tu baada ya kudai tuliwasikia wakiongea!:-(

Hebu tuanze na Iddi Amini DADA....


Halafu huyu jamaa ajulikanaye kama Mwalimu Nyerere.....


Halafu kuna huyu MADIBA...


Halafu kuna huyu OBAMA....



IJUMAA na WIKIENDI njema MHESHIMIWA!

Tatizo la kudai MWALIMU ni MZURI kwakuwa ANARAHISISHA kuelewa!

Binadamu ni mvivu ndio maana asilimia kubwa ya yamzungukayo HAYAELEWI

Na ukimpa nafasi atakuelezea kwanini HAELEWI.

Utasikia eti kitabu ni kibaya kwa kuwa HATUKIELEWI.

AU tu Mwalimu ni MBAYA kwa kuwa HATUMUELEWI.


Labda tukumbuke tu LABDA ni MWANAFUNZI ndio MBOVU kama HAELEWI.


Na tukumbuke tu kuwa WENGI wajuao sana ndio ambao kirahisi HATUWAELEWI.


Na kama unampenda Mwalimu kwa kurahisisha SOMO usishangae kujikuta mengi magumu HUYAELEWI.

NI wazo tu KINGUNGE na wala HUU sio MSAAFU!


Hebu tuulizwe- NAni ni Mwalimu wa MAPENZI....


Au tupate wimbo wa Omar Kopa -UNYAGO

Kama BADO hujawahi kufikiria kula PANYA!

Kuna uwezekano Bado hujawahi kuumwa njaa VIZURI!:-(


Ni hilo tu nilitaka kukukumbusha Mheshimiwa!

Thursday, July 23, 2009

CHAKUKUMBUKA!

Ni muhimu KUSAHAU,...

.... hata kama ni ujanja UKIKUMBUKA.


Na kwa kuwa TUNASAHAU,....
... LABDA ndio maana tunarudia hata yaumizayo tusiyo vizuri KUMBUKA.


Na kama leo UTASAHAU,...
.... labda kuna utakayefikiri baadaye ni JINIASI kwakuwa eti ANAKUMBUKA.:-(


Na unaweza kwa kula njegere UKASAHAU,...
... lakini kumbuka mtupa maganda ATAKUMBUKA.:-(

Swali:
  • Unakumbuka LABDA kuna jambo ulikuwa unalikumbuka miaka yote na ni leo hii umelisahau?


NAACHA wazo au tu Ujinga kama kwako ni UJINGA niandikacho katika BLOGU hii Mheshimiwa!:-(

SIKU NJEMA lakini MHESHIMIWA!


DUH ngojea Ochestra Makassy waongelee- Mosese



ASANTENI SANA Wadau ambao hamnichoki kama PAPAA Martin Mtefu,TOMMY, Peter na Marwaan ambao ni hawa hapa ndani ya baadhi ya picha hizi zangu...:-(

Photobucket




Photobucket






Photobucket










Photobucket


Photobucket


Photobucket


Photobucket





Photobucket



Photobucket

Au tu Lord Kitchener amalizie kwa kuongelea MENDE katika- KAKA ROACH

Tako - Siriasli!:-([tahadhari :stori ya kijinga]

Mtu anapoZALIWA,...
.... tako ni moja ya KIUNGO ambacho hata MJANJA huchelewa kukiona ingawa KIPO!:-(

Na saizi ya TAKO unapoZALIWA,...
....ni VIGUMU kuheshimu umuhimu wake ingawa linasaidia kukuondolea uzito WAKINYESI bila kuliomba na LIPO.:-(


Na kunauwezekano TAKO huwa linafichwa tokea UNAPOZALIWA,....
.... na sababu zake za kufichwa ni kwa kuwa hata kabla haujaliona kuna walisafishao na wanacho safisha ni kinyesi kwa hiyo hata likivalishwa chupi safi wanakuwa tayari wanakuandaa kuficha hata tako safi UKILISTUKIA ingawa ukiwa hai LABDA bado linasaidi ya aibu na LIPO.:-(


Na tako hata kama linapendeza na linanukia poda KWAKUWA limenyunyuziwa PODA baada tu ya KUZALIWA,...
.... bado hata alizungushaye UKUBWANI kwakuwa ni KIGOLI na linampendeza au tu ni MSENGE na BASHA anatamani kipenyo, NI VIGUMU kulikosanisha na uhusiano wake na KINYESI hata kama alizungushaye kapigwa pasi na anawaringishia wasio wajanja kuwa tako LIPO:-(


Swali:
  • Hivi kuna uwezekano MHESHIMIWA umefuatilia stori ya tako mpaka sentensi hii? LIONE VILE!:-(

DUH naacha wazo hili ambalo labda ni la KIJINGA Mheshimiwa WANZABANGA!:-(


Ngojea nimuachie Erykah Badu anisaidie katika kitu-Annie HAVAI CHUPI au kwa KIKRISTO -ANNIE don't wear no Panties
Au nimuache katika picha kama alivyonisaidia Juzi ya Jana....


Photobucket


Photobucket




Photobucket








Photobucket




Photobucket





Photobucket




Photobucket




Photobucket

Photobucket



Photobucket



Photobucket



Photobucket



Photobucket




Photobucket




Photobucket




Photobucket




Photobucket


DUH NAACCHA na namuachia tena Erykah aendeleze kunitesa kama JUZI ya JANA...katika - On and On

Ngojea mie MTAKATIFU Simon Kitururu nijaribu kusimulia TAKO kwa picha!:-([Tahadhari: stori ya kijinga]

Photobucket Hapa najaribu kuongelea umuhimu wa Tako




PhotobucketHAPA najaribu kuongelea ujazo wa tako...

Samahani ngojea Mahotela Queens wanisaidie kuleta Ustaarabu katika....-Mbaqanga





Au niwaache MAHOTELA QUEENS kwenye Picha wakiwa na baadhi ya watu wengine walio nisaidia kuendeleza Juzi ya Jana





Photobucket




Photobucket









Photobucket




Photobucket






Photobucket




















Photobucket



Photobucket



Photobucket



Photobucket




Photobucket


Photobucket




Photobucket









Photobucket



Photobucket



Photobucket



Photobucket

Au Ngojea Mahotela Queens Wamalizie KITENGO kwa-Mbube

Wednesday, July 22, 2009

Kila mtu ni MWANASIASA!

Labda wengine katika mchezo wao wa siasa ,...
..... ni kunyoshea wengine kidole kuwa ni WANASIASA.


Labda wengine katika mchezo wa siasa,...
... utaustukia wakiucheza makazini ili wapandishwe cheo huku wakikana wao sio WANASIASA.

Na labda ni USHAHIDI unasiasa,......
.... kama uko chini ya mfumo wa kisiasa na una maoni kuhusu WANASIASA.

Na huwezi kuwa hujaathiriwa na siasa kiasi kwamba huna maoni ya kisiasa,....
.... kama mpaka jina la utaifa wako ujitambulishalo nalo ni tupu LABDA hata za Nyerere SIASA.


Na wanasiasa wengi hawajistukii ni WANASIASA,....
..... kwakuwa siasa zao ni za kufuata wahisiye ni kiongozi katika waaminicho katika SIASA.


Na ndio maana asilimia kubwa ya waitwao wanasiasa,....
..... hawakuhitaji kuiendea shule au labda BADO hawajui ni nini SIASA.


Na katika siasa mpaka za nyumbani nasikia bado BABA ni KICHWA CHA NYUMBA kisiasa,....
.... kama kweli huyo baba hata nyumbani anashinda katika mchezo wa kumchezea akili MAMA na WATOTO wake nyumbani wasistukie kuwa labda siku nyingine BABA ni MKIA wa nyumba KISIASA.

Na labda hata kutongoza ni tupu siasa,....
..... na ukikubaliwa labda ulikubaliwa na ALIYEKUBALI kabla hata hujatongoza na ni kwa KISIASA.:-(

Swali:
  • Unabisha wewe huchezi siasa ingawa hulipwi mshahara kama mwanasiasa?
  • Unauhakika unajua siasa ni nini kabla hujaendelea kukana eti kwa kuwa wewe sio mwizi basi wewe sio Mwanasiasa?
  • Kwani unafikiri ni wanasiasa wangapi wanajua siasa?
Samahani naachia hapa ngojea niende chooni kidogo kutekeleza ZA CHOOO siasa!
BAADAYE Mheshimiwa na kama sio mvivu ENDELEZA tu LIBENEKE kama UKO HAI Mheshimiwa!





Ngojea EN Vogue wawashawishi watu- DOn't let go


Au tu TLC wadai ya -Waterfalls

Tuesday, July 21, 2009

Kasheshe la MWENYE PUA kustukia kashaNUSA!:-(

Kumbuka hata kama profesheni yako ni KUNUSA,....
... harufu kibao hata uwe mjanja huzinusi MAKUSUDI.


Na mara nyingi HATA ukinuia kurudia KUNUSA,....
.... si lazima ulikuwa hujui INANUKA na hata ukunje uso huku unaibania pua kunauwezekano KWA MARA YA PILI weye umenusa MAKUSUDI.

Ndio kuna vyenye harufu nzuri UKINUSA,.....
..... lakini hata hivyo unavistukia kwa msaada wa VINUKAVYO ambavyo kama VINUKIAVYO labda hukuvinusa MAKUSUDI.

Na pia , amini usiamini ukiwa hai hata kama ni BINGWA WA UKWEPAJI waweza jikuta tu UMENUSA,....
..... ingawa ni kweli pia unaweza kuamua VYA HARUFU MBAYA kuvinusa MAKUSUDI.



Swali:
  • AU?
  • Hivi umenielewa nachojaribu kusema ni kwamba kama binadamu kuna mambo kutokana na udhaifu wa kibinadamu unaweza jistukia tu uko katikati yake kwa kunuia au kutokunuia?
  • Na hivi unakumbuka ukinusa hata kinyesi shukuru UNALIPUA na shukuru tena zaidi LIPUA lako bado linafanyakazi?
NI wazo tu BITOZI na nakutakia MAMBO KUKU kwa MRIJA kama kwako kuku anapanda!

Ngojea ALI KIBA abadili hali ya hewa kwa kibao- Karim..




Au tu Ali Kiba amrudia -Mac Muga

BINADAMU katika juhudi za kuhalalisha KITENDO!

Kuna watu katika juhudi za KUHALALISHA...
... watadai kitendo ni haramu mpaka ukifungie ndoa KITENDO.

Na ukichunguza mbinu za binadamu za KUHALALISHA....
..... sio tu unatakiwa ukichinjie kuku zeruzeru katika kuhalallisha KITENDO , bali labda itabidi uitwe hata DOKTA ili baadhi ya watu wasikilize wako ushauri katika KITENDO.


Na ukicheza waweza badili dini ili KUHALALISHA.....
..... kwa kuwa labda nyingine dini HATA UJINGA unatafsiri tofauti katika kuhalalisha KITENDO.


Na katika KUHALALISHA......
....waweza jihalalishia una busara katika kitendo na ukauawa na KITENDO.:-(


Swali:

  • Unafikiri hujajaribu leo kujihalalishia KITENDO?

NI HILO tu MHESHIMIWA!

Ngojea Mikey General aje na -Mr Walker.....



Au tu Jon B ft. Beenie Man waje na - Everytime

Monday, July 20, 2009

WAKATI tunasikiliza ya yule ISEMEKANAYO ni WAKUIGWA MFANO!

Labda ukiona utakaokuuiga MFANO,....
.... USIWACHUNGUZE kiundani utakao KUWAIGA MFANO.

Na LABDA ukiwachunguza sana wakupao MFANO,....
.... waweza KUGHAIRI kuiga hata ule mzuri wao MFANO.


Na wakati unaiga MFANO,...
.... kumbuka mifano mingine HADHARANI ni danganyatoto na wawezajikuta umekuwa hata MALAYA kama si KIRUKA NJIA na tutajua kwa UONYESHAVYO wako MFANO.

Swali:
  • Hivi unakumbuka mpaka hata akina Rais Nyerere kuna wenye uhakika MIFANO yao haiigiki kwakuwa kwa mtazamo fulani KIMFANO ilishindwa?

  • Hivi unakumbuka ukimuiga NELSON MANDELA kuna watakaodai maana yake NDOA kadhaa zitakushinda na unaweza kuitwa TERORISTI na WAJANJA kama alivyojulikana MADIBA kabla hatujaMJUA?

Ni wazo tu KINGUNGE na NIMEACHA!

Hebu tumsikilize Rais wa Rwanda Paul KAGAME kidogo aonyeshe maringo yake dingilidingili mpaka chini... katika- Africa's Greatest Success?





AU tu Bembeya Jazz National wabadilishe HALI YA HEWA katika kibao -Whisky Soda

Friday, July 17, 2009

Kama TUKIBOBEA katika kuangalia ALIYEFAULU MTIHANI bado hajui NINI!

Ukifeli MTIHANI,....
.. ..waweza kuwa maarufu kwa KUTOKUJUA...

.... ingawa labda uliyefeli ungemfundisha hata aliyetunga MTIHANI ya kuanzia nje ya chumba cha MTIHANI. Au vipi mshikaji!:-(


Ukifaulu MTIHANI,...
.... unaweza mpaka KUJITUTUMUA kwa KUJUA....
.... ingawa labda ungefundishwa KITU usingevimba BICHWA kwa kuwa tu umefaulu MTIHANI.Au vipi mshikaji!


Na TUKIBOBEA katika kumuangalia aliyefaulu MTIHANI,....
... tunaweza kusahau kujifunza KUJUA...
.... ALIYEFELI au kufaulu HIYO haina mpango baada ya MTIHANI kwa kuwa siye wenyewe bado maisha kila wakati yanatupa MTIHANI.Au sio mshikaji?:-(
Swali:
  • AU?
  • Wewe unauhakika umefaulu wa leo MTIHANI?
  • Unakumbuka pia aliyefaulu leo mtihani ukimpa muda anaweza akasahau majibu ya maswali ya huuhuu mtihani wa leo alioufaulu MTIHANI?

NIMEACHA wazo na nakutakia IJUMAA na WIKIENDI NJEMA !
Mola akipenda tutaonana JUMATATU MHESHIMIWA!

Ngojea WAHU adai- Mambo BADO....


AU tu Mwana FA arudie kuwa - BADO NIPONIPO..

Chochote KIKUCHEKESHACHO kuna mtu KINAMLIZA

Kumbuka ,...
..... MAZINGIRA yakiruhusu na UJUACHO maishani kwenye picha ukikioanisha...

.... kuna KIMCHEKESHAYE hata kama kinakuliza WEWE.


Kumbuka,...
...AKITEREZA mtu na KUANGUKA...
..... labda atakayecheka ni WEWE.


Na LABDA kumbuka,...
.... kuna WACHEKAO akifa mtu hata kwa kisingizio ni adui...
.... hata kama sio WEWE.


Na vilevile kumbuka,...
... VICHEKESHO visivyowachekesha wengine...
... labda ndivyo vikuchekeshavyo WEWE.


Nuna basi kidogo labda utastukia na kukumbuka,...
... kuna mtu atakayechekelea akishuhudia umenuna...
...kama ambavyo uchekavyo HATAVISIVYOCHEKESHA kwa mwingine vikuchekeshavyo WEWE.


Labda tu pia kumbuka,...
...KULIA, kucheka, HUZUNI, furaha , mpaka hata KUTEKENYWA labda vyote unavijua....
.... kwa kuwa vyote ni kweli kiunganishi ni WEWE.


Swali:
  • Hivi bado unakumbuka katika SAKATA hili la maisha ajuaye vizuri kikuchekeshacho au kukuliza ni WEWE?

  • Na unakumbuka kuna mtu upishananaye mtaani kwako ambaye HATA SIKU MOJA hakuoni wala kukustukia upo hata tukiachana na swala kuwa unalia au kucheka?

  • Unabisha?
NAACHA UNYAMBISI!

Hebu tubadilishe ustaarabu kwa kusimuliwa ya YESU katika -YESU hakusema yeye ni MUNGU..


Baada ya mahubiri hebu Simba wa yuda - kwaya ya uinjilisti kijitonyama luthern church wazungumzie- Hakuna Mungu kama WEWE...


Baada ya kumaliza mahubiri ngojea Ngwair asimulie siku ilivyoendelea kwa mtu fulani katika kiba-MIKASI

Thursday, July 16, 2009

Kumbuka tu KUWA karibu WATU WOTE uliokutananao leo UNGEWASACHI utumbo walikuwa wanatembea na MZIGO wa CHOO!:-(

Binadamu ni SAWA hata tukikubali kuwa WATU si sawasawa UKIKUMBUKA,...
....karibu yeyote umuonaye hata kama haelekei msalani saa HIYO kunauwezekano ana mzigo wa CHOO.


Ni moja tu ya kugundua BINADAMU ni sawa hasa UKIKUMBUKA,...
...hata UKIRINGIWA na YULE au YEYE, kumbuka NAYE hata kwa maringo bado kuna muda hutafuta mlango wa CHOO.


Na kama WEYE ni mnuka KIKWAPA utishwaye na anukiaye marashi ya karafuu KUMBUKA....
....pamoja na yote madairo katika uhusiano wake na tako moja wapo ni MZIGO wa CHOO.


Swali:
  • Hivi ushashuhudia jinsi wapiganiao USAWA wapendavyo kutambulika wasivyo SAWA na waliobanwa na shughuli nyingine za maisha ambazo kwa binadamu hazina USAWA?
  • Kwani wewe hujawahi kumringia mtu bila kufikiria umrishiacho sio spesho?
  • Unakumbuka karibu dini zote maarufu zina nafasi ya Mmiliki watumwa na Mtumwa na ukizubaa una weza ukatengwa kwa kigezo una UUME au UKE?
NAACHA WAZO!
Hebu tuangaliye ya dunia.....


Au tu Lord Kitchener arudie - Sugar BUM BUM

Maswala ya kujiandaa KUWASHWA!

Kama bado HUWASHWI,...
.... shukuru UBONGO kama bado unakumbuka .....

.... huwa unakuna NGOZI lakini ni ubongo ukustuao wapi unawashwa UKIWASHWA.


Na kama bado HUWASHWI,...
....tumia ubongo utakumbuka...
.... mara nyingine si busara kujikuna kipengele kinachowasha UKIWASHWA.


Ingawa kwa wengi hudai ghafla tu bila taarifa hujistukia WANAWASHWA,....
...ni kawaida pia kukumbushwa kukumbuka...
.... kuwa hata kama hutamani kuwashwa sasa hivi, utajikuna vizuri UKIJIANDAA au utastukia labda dawa ni utumbue KIPELE na sio ukikune kwa kuwa UNAWASHWA.

Labda siri ya kujikuna au kujitumbua kistaarabu ni kujiandaa KUWASHWA!:-(

Swali:
  • Wewe kama ni Mkristo si huwa unakumbushwa uwe tayari kila dakika kwa ujio wa Yesu kwa kuwa ukijiandaa unaweza ukapatia sekunde ya kwenda mbinguni kimwanana?

  • Hivi kama leo huwashwi unauhakika umejiandaa KUWASHWA?
  • SI unakumbuka ukijiandaa vizuri hata mtihani mgumu kwako utakuwa rahisi?
  • Hivi unauhakika na maanisha nini hapa?

NAACHA wazo MHESHIMIWA na nakutakia KILA LA KHERI katika SHUGHULI ZAKO au niseme nakutakia SIKU kuku kwa MRIJA kama wewe sio vejeteriani!


Ngojea nitumie tena sauti kurudia kukiri......

Labda huu ni UKWELI kuhusu MTU YOYOTE yule!:-(

Ukimtafuta MTU mapungufu,....
.... utamkuta na MAPUNGUFU.


Na kwa mapungufu,.....
.... anaweza kukunyoshea weye kidole....

.... huku haoni YAKE mwenyewe MAPUNGUFU.


Na jihadhari na ajulikanaye kwa kukosa mapungufu,....
.... na kama ni yeye mwenyewe ajishabikiaye wako ole.....
....na utakoma mwenyewe ukistukia afichalo lake PUNGUFU.


Lakini kwanini mtu atafute la mwingine pungufu,...
....wakati maishani muda hautoshi hata kujinyoshea mwenyewe kidole....
....katika jitihada za kusawazisha hata lako mwenyewe PUNGUFU?

Swali:
  • Hivi ni yako mangapi unafikiri hayana UPUNGUFU?
  • Hivi huwezi kutafsiri mahangaiko ya binadamu katika kusawazisha mapungufu kuwa ndio yajulikanayo kama MAISHA?

NI wazo tu KIJEBA usitishike!


Ngojea tubadili hali ya hewa kwa kutoka kwa binadamu na kuangalia ya MAJINI...




Au ngojea tu ALPHA Blondy amuongelee- Fanta Diallo

Wednesday, July 15, 2009

Hata USIPOONA vyaelea LABDA vipo na ukweli ni TAYARI VILISHAUMBWA!

Usipoona KITU au kustukia moshi unafuka,....
.... SI LAZIMA ni kwamba kitu HAKIPO!:-(


Na ni kweli ni ASILIMIA CHACHE TU YA VITU ndio uistukiayo,....
... ingawa VITU unavipita hata NYUMBANI (Na hapa sizungumzii MABUIBUI!:-() na njiani ndio kabisaa huvioni wakati ukweli ni VIPO.


Hata sasa hivi sehemu ULIYOPO kuna machache tu unayastukia yaliyokuzunguka,....
.... NA kuna uwezekano mpaka jibu la MATATIZO yako hapo pembeni YAKO kidogo tu LIPO.:-(

UNARUHUSIWA KUNIBISHIA MHESHIMIWA!

Swali:
  • Unakumbuka labda leo siku nzima mpaka sasa hivi navyokutonya ulikuwa umesahau kuwa una hata KISOGO ingawa kipo tu nyuma ya kichwa chako?

  • AU?

NI HILO tu kwa leo KINGUNGE!


Hebu tupumzike kwa kuwashuhudia wastaarabu wakiendeleza USTAARABU...

Au ngojea tu MORY KANTE arudie kutuliza majeshi katika kibao - Yeke yeke

Tuesday, July 14, 2009

IMANI!

Imani sio DINI,...
... na ukitaka DINI unaweza mpaka KUKUMBUKA ulianza kuishangilia LINI.

Kwa IMANI,....
....ukinuniwa bado unaweza kuamini AKUNUNIAYE baadaye atakuchekea hata kama sasa hivi BADO unampa KWININI.


Imani ni UTAAHIRA na kama unatumia akili mpaka katika maswala ya IMANI,....
..... labda hicho ufanyacho ni SAYANSI na kumbuka ukitumia AKILI swala la DINI halieleweki kama tu IMANI.

Swali:
  • Hivi utaahira si unaoanishwa na mtindio wa kuelewa viletavyo maana kwa wengine KAMA VILE TU kuabudu Mbuyu, Mbuzi, Ng'ombe au tu Mungu Waupendo awezaye yote atakayewaachia binadamu kibao wafanye dhambi ili badaye awape kibano na kuwachoma moto?


NI WAZO tu KINGUNGE wala USITISHIKE!

UJANJA au tu kama ni kweli SIO UJANJA kuwa ni kweli MHESHIMIWA HUHITAJI kukumbushwa JINSI ya kufua CHUPI![usisome STORI hii!:-(]

Ulazima wa JINSI ya kufua CHUPI hata kama haina DOA eneo KUMBUKA tunaweza kuwa tunaongelea hili SWALA kwa kuwa KUNA mwenye chupi na INADHANIWA hicho kitu ni KAWAIDA.

Na katika kusawazisha ya KAWAIDA,....
.... ya kawaida yanaweza KUFIKIRIWA ni kawaida kwakuwa tu SI KAWAIDA ikizoeleka hugeuka KAWAIDA.


Na labda SI LAZIMA kuvaa chupi ingawa KIFICHA NYETI matumizi yake yashakuwa KAWAIDA.


Na mtoto mzuri CHUPI CHAFU hata kama hutaki kukubali hata SIKU NYINGINE akivaa chupi safi BADO utamkumbuka alivyopendeza na chupi CHAFU na unaweza kufikiri ingawa ni KAWAIDA kumbukumbu zako HIZO si KAWAIDA:-(

Na UKIFIKIRIA tu kuhusu kuwa MTOTO MZURI anavalisha chupi eneo zuri ambalo lisipoogeshwa hutaki kulinusa,.....
.. ....Labda ni kweli TITI KUBWA hata kama chuchu hakuna halikusaidii kukwepa kuwa tayari unajua HARUFU na UNAHISI labda eneo lililofichwa na chupi LINANUKA kwa kawaida na wazo hilo LABDA bado ni KAWAIDA.:-(



Na ni KAWAIDA kama huna mashine ya kufulia CHUPI kuna eneo tu LABDA UNAJUA linachafuka zaidi katika CHUPI na kama kwa kufua unatumia MIKONO huwa unatumia muda zaidi kulisugua ENEO na ni KWELI labda staili yako hiyo ya kusugua maeneo kadhaa ya chupi na sio CHUPI YOTE ni KAWAIDA.


Swali:
  • AU?
  • Unakumbuka kuwa KAMA hukumbushwi kufua CHUPI au KULA inamaana kwako hata KUJITAIDI ni KAWAIDA?
  • UNajua kuna jambo UNALAZIMIKA TU kama kufua chupi kwakuwa si busara kuvaa chupi mpya kila siku LA SIVYO labda JAMBO usipotenda itakuwa si KAWAIDA?

NAACHA wazo na kama umenisoma mpaka hapa KATIKA STORI HII ambayo labda ni ya KIJINGA wakati nilikuomba usisome stori hii, NAHISI UNATABIA MBAYA kwa kuwa husikilizi ushaurivyo!:-)

USITISHIKE kama STORI HII HAIKUFUNDISHI kitu MHESHIMIWA!:-(


DUH!

Ngojea tupate tena KITU katika miondoko ya KUNESANESA...


U tu ELEPHANT MAN amalizie kwa -WILLIE BOUNCE


ASANTENI WOTE ambao bado MNANITEMBELEA na ASANTENI WADU ambao baadhi mpo kwenye picha zangu za JUZZI ya JANA zifuatazo..

Photobucket



Photobucket



Photobucket



Photobucket


Photobucket



Photobucket


Photobucket




Photobucket



Photobucket




Photobucket





Photobucket



Photobucket















Photobucket




Photobucket




Photobucket












Photobucket



Photobucket


Photobucket





Photobucket


Photobucket

Monday, July 13, 2009

NIPANULIE!:-(

Panua,...
.... kama UNACHAKUPANUA.

Nipanulie,...
.... na NI msaada kwetu tupendao KUPANULIWA.


Wakati unapanua,...
.... kumbuka UNAKIPANULIO la sivyo USINGE PANUA.:-(

Nipanulie,...
.... si kwa sababu unahuruma TU, ila kwanini NICHACHE wakati una SHILINGI kibao UKIPANUA?


Swali:

  • Hivi unakumbuka yeyote unayefikiri KAFANIKIWA kuna uwezekano kuwa mafanikio yake yalifanikiwa kwa kuwa kuna MTU ali PANUA?
  • Hivi unakumbuka kama unauwezo na unataka watu wafanikiwe inahitajika UPANUE angalau UWIGO?
  • Unauhakika hujawahi kupanua au ni kwamba hukumbuki ukipanuliwa?

Duh NAACHA wazo na JUMATATU NJEMA Kijeba!

Au tu Nuru the LIGHT amuongelee - MSELA



Au tu FUCKLY alonge ya -DUDU

Aisee CHOO, naomba KUKUKOJOLEA!:-(

Choo,...
... watu WASTAARABU labda kabla ya KUKUNYEA nao pia NI KWELI wana KUKOJOLEA!:-(

Chooo,...
....vitendo UFANYIWAVYO kwa ajili tu una TUNDU , kwakuwa NI KWELI hata KAMA ni kweli HAITAKIWI TUSEME, ila MARA karibu zote TUKINYA tuna ADABU SANA hata kama UNABISHA muulize nanihii ATAKIRI ni kweli hata leo wakati TUKIFANYA mambo HATUJAKUKODOLEA.


Choo,....
..... mjanja kama tu MCHOYO wa KUNYA kweli WANAWEZA KIRI we bingwa kwa kuwa wote NI KWELI wana KUCHOJOLEA.


Choo,...
....asante kwa kuleta USAWA kwakuwa kuanzia RAIS mpaka wapendao URAHISI wote pamoja na MTAKATIFU mimi, TUNAKUTEMBELEA.



DUH!

NAACHA WAZO Kingunge kabla hujakumbuka nyuma ya KIKOJOLEO kuna KINYEO chenye sura MBAYA!:-(

Swali:'
  • Hivi unakumbuka CHOO na MTU ukifananisha wanaweza KUFANANA kama NI KWELI wote wanaweza KUKOJOLEWA?


Ngojea Dave CHAPELLE atukumbushe R Kelly anapenda kukojolea watu katika- Piss on YOU



Au tu jamaa apige GITAA katika wimbo wa R Kelly aongelee- -Ignition

Friday, July 10, 2009

CHINI kidogo ya SURA ya MUUZA SURA!

Labda MUUZA SURA ana sura NZURI,....
..... ukikumbuka....

.....hata UBAYA wa SURA MBAYA ujichoni mwa aliyejifunza TU nini SURA MBAYA.:-(


Labda MUUZA SURA kweli ana sura NZURI,...
.....ukikumbuka.....
.....hata UZURI wa SURA NZURI haupo NG'O jichoni mwa ASIYEHUSUDU, ingawa jichoni mwa apendaye, MZURI hana UBAYA.

Labda MUUZA SURA anajiamini tu kuwa ana SURA NZURI,...
...ukikumbuka tu.....
....ukijiamini hata jicho lako litakuhakikishia pua lako kubwa wala si BAYA.

Labda MUUZA SURA kiuno kama N'GE chini kidogo ya sura bado MZURI,...
....ukikumbuka....
... labda kwa wamjuaye UNDANI kwa NDANI hata tamutamu yake ya ndani ina SURA MBAYA.


Na labda MUUZA SURA kwa ndani bado MZURI,...
.... kama UNAKUMBUKA....
... karibu mara zote UBAYA WA MTU utaupata TU kama YAKO NIA katika mtu NI kuutafuta UBAYA.



Swali:

  • AU?
  • Hivi unakumbuka siku hizi TANZANIA na labda AFRIKA kwa ujumla , wenye MATAKO MAKUBWA na BOMBA LA SURA huwa hawashindi hata U-MISS Kariakoo a.k.a MASHINDANO ya UUZA SURA kwa kuwa eti maendeleo yametugundulisha kuwa MISS U.S.A kwa kawaida hana TAKO?
  • Halafu si unakumbuka MUUZA SURA anaweza bado akawa ni KINUKA MKOJO kama hatumii vizuri maliwato?



NI hilo tu KISURA/ HENDISAMU au tu WEYE uaminiye una BOMBA la SURA MBAYA, ila kumbuka ni WAZO tu Banangenge!:-(


NIMEACHA na nakutakia ijuMAA NJema na WIKienDI Kibonge!

Hebu HOT CHOCOLATE watukumbushe kitu - Sexy thing


Au tu SAMBA MAPANGALA kwa mara nyingine atukumbushe uzuri wa- Kabibi

Thursday, July 09, 2009

LEO mie MTAKATIFU Simon Kitururu NAKIRI kuwa na HAMU kweli ya UTANDU na UKOKO kwa MBAAAAALI!:-(


Sijui nipandishe MZUKA wa UTANDU na UKOKO ?

Na hamu kweli ya UTANDU na UKOKO kwa mbaali halafu nilipo MAMA NTILIE HAKUNA!:-(

DUH!

Na hapa siongelei ukoko wa UGALI , MAHARAGE ya NAZI ya JANA au tu MAKANDE a.k.a PURE/ KIBULU.

Wapenzi wa hiki kitu nadhani MNAJUA na mnanielewa naongelea nini!:-)

DUH!:-(



NI HILO TU!


Ngojea nijisahaulishe kwa kufikiria -BATA kama wasimuliavyo -HABIB na RICHIE


Au tu SAMBA MAPANGALA aendelee kunitamanisha -NYAMA CHOMA

Hamu ya KUNOGEWA TENA kama mara ya kwanza ilikuwa TAMU!

Utamu ULEULE kujirudia ni BAHATI NASIBU,..
... ingawa kwa kuwa MLENDA ushauonja mara ya kwanza wadhani wajua wake UTAMU.

Kama mara ya kwanza ilinoga na ukamsimulia NASIBU,..
.... haimaanishi katika SIMULIZI ZAKO za pili na ZA kumi za UTAMU kwa NASIBU huwa unaongelea uleule UTAMU.

Na haujirudii UTAMU wanasaikolojia WATAJIBU,...
.... kwa kuwa kisaikolojia au hata kihamu onjo la pili na la tisa hata la PEPSI huwa linatofautiana UTAMU.


Na kama mara ya kwanza ni chungu ILIKUSIBU,....
...kumbuka YA KWANZA CHUNGU inaweza ikawa SI CHUNGU ukirudia na KUPATIA jinsi ya kuonja UTAMU.



Swali:
  • AU?
  • Si unajua inadaiwa walioonja na kudondosha BIKIRA na walionja BIA na kudai chungu inasemekana baadaye chungu iligeuka TAMU?
Ni hilo tu na NI WAZO tu usitishike KATIBU WA MASWALA!

Ngojea Rose ROYCE walalamike katika -Love don't live here anymore

Msichana mzuri a.k.a KIGOLI na Mvulana mwanana a.k.a KIJEBA katika MASHINDANO ya KUZEEKA!

Na ni kweli hata DOGODOGO saizi YAKO,...
.... mpe muda ATAZEEKA.

Lakini angalia SURA LAKO na sikilizia kiuno chako kihimilivyo shughuli ZAKO,...
....wakati umestukia DOGODOGO si SAIZI yako kwa kuwa huvutiwi na Wazee na DOGODOGO kwako KAZEEKA.

Kumbuka!
Wakati DOGODOGO mambo zake DUKINAA katika VIONJO vyako,...
...kuna MZEE awezaye MAMBO ADIMU yenye makali ya ASALI na ukileta ZA kuleta ANAKATIKA na kupakua HAJAZEEKA.

Na kama ni KIGOLI kwa haraka AZEEKA kama nyanya kwenye kachumbari YAKO,...
.... jiulize ni kwanini KIJEBA hufa kwanza kabla ya KIGOLI aleZEEKA.

Ni swala tu la MUDA hata WAKO,...
... aringaye kama tu ASIYERINGA wote WAZEEKA.

Ni swala la MUDA tu hata WAKO....
... umjuaye kwa UTOTO bila kujali UKE wala wake UUME, ataZEEKA.:-(


Ringa MWANAWANE onyesha maringo YAKO,...
... kwani punde si utani UTAZEEKA.

Kumbuka hakuna mbaya kwa KUZEEKA kama ULIVYO mtazamo WAKO,...
... ila hata kama UNACHAKURINGIA, waweza kukosa nguvu za kuringa UKIZEEKA.

Na mwenye HOFU YA KUZEEKA na kama huo ni uoga WAKO,...
... kumbuka INA maana unashughuli chache na umezidiwa na muda wa KUFIKIRI wakati huu UKIZEEKA.


Swali:
  • Unakumbuka SASA HIVI unaendelea KUZEEKA?
  • Ushawahi kusikia ni wanawake wazeekao haraka?
  • Na hivi unajua TAKWIMU zadai ni WANAUME wafao MAPEMA kwa uzee?


Ni wazo tu WAZIRI wa mambo ya GHAFLA na STAREHE NDOGONDOGO , na wala USITISHIKE!


Ngojea JERREMIAH abadili hali ya hewa kwa kibao- Birthday SEX

Wednesday, July 08, 2009

MSTARI mwembamba kati ya KUJIHESHIMU na UNAFIKI!

Ni kawaida kwa UNAFIKI kufanana na HESHIMA,...
.....kwa kuwa WANAFIKI wengi KWA UNAFIKI mpaka hudhaniwa WANAHESHIMA.

MNAFIKI hukuficha UKWELI,....
.... usijue iliumpende, umpe peremende au tu kwake uwe na HESHIMA.

AKUHESHIMUYE hukuficha KI -MILA na DESTURI yatiayo aibu ya UKWELI,...
.....au hata KUKUNYIMA kidude hata kama ANATAKA kwa kuwa eti ANAHESHIMA.


HESHIMA ni UNAFIKI kama ni ya KINAFIKI,...
.. na kuna UWAHESHIMUO kwa kuwa TU unauchanganya UNAFIKI na HESHIMA.


Swali:
  • AU?
  • Ushawahi kumpa SHIKAMOO MWALIMU ili kumuonyesha HESHIMA huku unamtukana kimoyo?
  • Kwani unaathirika kwa KUHESHIMIWA KINAFIKI kama AATHIRIKAVYO akuheshimuye KINAFIKI?
NIMEACHA wazo MKUU wa KITENGO!

Ngoje tu tena FELA KUTI amuongelee- Gentleman





Au tu namuacha Steve Wonder aongelee-Master Blaster

MPAKA wa MTU!

Ukizidisha ,....
.... utaumiza MTU.

Ukipunguza,....
....waweza DHARAULIWA na MTU.


Ukizidishiwa,....
.... utaumia kama wewe ni MTU.

Kama unaweza na KINAFANYIKA,...
.... labda BADO hujavuka mpaka wako WEWE kama MTU.

Na kama kuna MPAKA,...
... kumbuka labda HUO umejengwa na MTU.

Kuhusu wewe ni MTU GANI,...
....inategemea na USTUKIAVYO mipaka ya WATU.

Kuhusu WEWE ni NANI,...
... chunguza mipaka YAKO wewe kama MTU.

Na kama kuna UTU,...
......kiutu kuna MIPAKA ya MTU.

KWAHIYO!
CHEZA, cheza kwa STEPU, usimkanyage MWENZIO!

CHEZA, cheza kwa STEPU,..
.. usijeparamia MTU.:-(

Swali:

  • AU?
  • Unakumbuka adui ya mtu pamoja na shetani kusingiziwa bado KWA KAWAIDA ni MTU?

NAACHA WAZO na kumbuka hili ni wazo tu MKUU WA KITENGO!


Ngojea Fela Kuti adai...-Water no get ENEMY


Au tu Stevie Wonder amuongelee- Mista know it all

Tuesday, July 07, 2009

HAMU ya vitu ADIMU!

Ni ulafi KULA SANA ,....
...... kwakuwa TU chakula ni KINGI.:-(

Na mapenzi yako ya NONIHINO,...
.... kwa kuwa unadhani ni adimu ,mie SIYAPINGI.

Na ni kweli,....
..... WALI ni MKUSANYIKO tu wa PUNJE za MCHELE NYINGI.

Kwa hiyo labda penzi lako la WALI,...
..... labda NI mkusanyiko tu wa PENZI LAKO la punye za mchele zilizobanana kwa WINGI.

Na kunauwezekano UKIKUSANYA penzi lako la vitu ADIMU,...
... utakuja STUKIA ni kweli PENZI LAKO si ADIMU kwa kuwa ni kweli UNAPENDA MENGI.:-(


Na kwa kuwa wengi hukwepa MALAYA kwa kuhusudu ADIMU,...
..... ndio maana DUNIA hii ya wenye hamu ya ADIMU imejaa MENGI.

Swali:
  • Au?
  • Unauhakika na uadimu wa vitu udhaniavyo ni ADIMU?


NAACHA wazo na nakutakia JUMANNE sangara wamo!

Ngojea na NASIO FONTAINE aongelee JUMANNE fulani katika -Black Tuesday


Au tu Lil VICIOUS amzungumzie mtoto mzuri kwa jina- NIKA

AIBU kama JUKUMU la UKUBWA!

Kua ustukie MAJUKUMU!

Kua ubanwe na MAJUKUMU,....
.....ingawa MAJUKUMU yapo tokea UTOTONI,....

.... hata kama JUKUMU KUU la mtoto ni awe MTOTO utotoni.


Kua ulazimike KIMAJUKUMU!

Kua uhisi una JUKUMU,....
.... ingawa kama huwezi JUKUMU,...
.... usiloweza LABDA sio lako JUKUMU.


Kwakuwa UNADHANI jamii inahisi ni lako JUKUMU,....
.... waweza ona aibu kwa kushindwa JUKUMU.

Na kama unalionea aibu JUKUMU,...
..... kumbuka jamii si lazima inapatia wakumpa JUKUMU.

Na kama bado unalionea aibu JUKUMU,....
.....MWANIWANE labda hilo si lako KIMAJUKUMU!

Na tukiachana na uvivu wa watu katika kukabili JUKUMU,...
.... kama umejaribu , SI mwisho wa DUNIA likikushinda JUKUMU.

Swali:
  • Au?
  • Unauhakika unalijua JUKUMU mpaka unafikiri ni lako JUKUMU?
  • Unauhakika viongozi wetu Afrika wanalijua JUKUMU?


NI wazo tu KIJEBA usitishike!:-(


Ngojea MAD LION aonyeshe asivyostukia jukumu lake kwa kuimba kibao-Shoot to KILL...


DAKIKA na SEKUNDE ambazo KIBINADAMU hazikumbukwi!

Dakika azaliwayo MTU,....
......NA sekunde afayo Mtu kwa huyo mtu HAVIKUMBUKWI.

Akuapo mtu kwa udadisi kuna kitu ANAWEZA kukumbushwa,....
.......INGAWA kwa uzoefu wa KIBINADAMU kabla ya kwikwi hua KWIKWI haikumbukwi.


Ndio!

Binadamu uwakutao wanacheka ,....
...... hufanikisha KICHEKO kwakuwa ukali wa maumivu ya kilio HAUKUMBUKWI.

Ndio!

Binadamu msahaulifu HUFIKIRI ,....
......... ni sekunde za makubwa kama KUFA ndio hayajulikani wakati mambo elfu lelaulela hayakumbukwi walakujulikana kama tu KWIKWI?


Ndio!

Dakika azaliwayo MTU,....
......na sekunde afayo Mtu LABDA kwa huyo mtu HAVIKUMBUKWI.

Swali:
  • AU?
  • Unauhakika dakika afayo mtu huwa anajua ndio sekunde HIYO anakufa?
  • Unauhakika aliyefariki anajua kuwa kafa?


DUH!

Ngojea ni muachie marehemu Franco aje na kundi lake katika- MARIO...

Monday, July 06, 2009

jumatatu NJEMA!

Ni HILO tu!



Nipo lakini na nahisi kama unanisoma basi na wewe UPO.

Swali:
  • AU?


Photobucket



Photobucket





Photobucket






Photobucket









Photobucket



Photobucket




Photobucket

Saturday, July 04, 2009

KUMA a.k.a KIDUDE kitumikacho saa nyingine ZAIDI ya KUKOJOLEA!:-(








Katika PICHA HII, hiki ni kifanananisho KATIKA maswala ya KIELELEZO kama HUJUI kidude!
:-({Samahani kwa mambo ya faragha kama BINGWA umefanananisha!:-(]











Ngojea tufafanuliwe kwa UNG'ENG'E kiduchuu,...

......katika maswala HAYA ya kuwa KUMA ni VAGINA kwa kiluguru...au tupate maelezo tu KUWA hata WADUDU wana KIDUDE....

The vagina (from Latin, literally "sheath" or "scabbard") is a fibromuscular tubular tract leading from the uterus to the exterior of the body in female placental mammals and marsupials, or to the cloaca in female birds, monotremes, and some reptiles. Female insects and other invertebrates also have a vagina, which is the terminal part of the oviduct. The Latinate plural (rarely used in English) isvaginae.

In common speech, the term "vagina" is oft..en used to refer to the vulva or female genitals generally; strictly speaking, the vagina is a specific internal structure and the vulva is the exterior genitalia only.

Na..
....KWA aibu ngojea tufafanuliwe zaidi kuhusu HIKI KIFAA kifanyacho zaidi ya kukojoa hapa

NA ,...
...nisikufiche HIKI KIFAA matumizi yake yanapendwa sana na wanawake kama tu PIA wanaume INGAWA kwa wanaume MALIMBUKENI ni kawaida kukosea jinsi ya kutumia HIKI KIFAA katika kukuna MATUMIZI.:-(
Swali:
  • AU?
  • Unafikiri Ustadhi au Mlokole kama tu MHESHIMIWA anakumbuka kuwa KUMA ni JINA TU la ENEO kama tu KINYEO ambalo labda kuna walitumialo JINA kama tu la MDOMO kwa kumaanisha wanakula NYANYA mshumaa?
NAACHIA MAHUBIRI HAPA!
Na ni kweli naacha KUWAZA na UKIZIDISHA WAZO SHAURI ZAKO wazo likigeuka MATUSI!:-(


Unaweza kucheza Kuma games hapa lakini!:-(



AU Ngojea Mbilia BEl Adai...-Phenomene


Au aongelee tu- DUKU duku...

MBOO a.k.a KIKOJOLEO!:-(


Samahani hii ni PICHA YA KIELELEZO cha GOVI na LABDA hiki ni KIELELEZO chenye baadhi ya DONDOO za matumizi ya KIFAA ya zaidi yaKUKOJOA![Samahani kwa stori za MWANASESERE za faragha INGAWA unaweza kunitukania ukichukia lakini]:-(
















Ndio!

Kwa lugha ya kitakatifu KIKOJOLEO CHA KIUME huwa KWA wajanja kinaitwa Penis!
DUH!

Hebu tupate ushee kwa ung'eng'e kiduchu...

Mboo a.ka. The penis NI:.....

.....(plural penises, penes) is an external sexual organ of certain biologically male organisms, in both vertebrates and invertebrates.

The penis is a reproductive organ, tecAlign Lefthnically an intromittent organ, and for placental mammals, additionally serves as the external organ of urination. The penis is generally found on mammals and reptiles.
Swali:
  • Unadhani USTADHI au MLOKOLE kama tu MHESHIMIWA hawawezi kudhani kutaja KIKOJOLEO ni TUSI kwa kuwa kinaitwa MBOO na KUNA wadaio HIKI KIFAA ni sehemu za siri ingawa si siri KIFAA HIKI kisaidiavyo umati KUJAZA watoto wa MTAANI kabla au baada ya kusambaza tayari VIRUSI mtaani?
Na KUMBUKA nimeacha wazo BITOZI na ukizidisha wazo linaweza geuka TUSI SHAURI ZAKO !:-(
DUH endelea HAPA kama unataka kujua zaidi kuhusu KIRUNGU kama KIJULIKANAVYO kwa lugha ya kitaalamu wa nanihii:-(...
Swali:
  • Hivi unajua UTAFITI UNASEMA ni wanaume AMBAO hawajui vizuri kukitumia HIKI KIFAA katika kujipatia AU kumpatia nonihino FARAJA ?
Lakini siye wastaarabu ngojea tuTabu LEY atuongeleshe KUHUSU
-CHERIE SAMBA


Au tu ngojea Tabu Ley aongelee-- Sacramento