Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Labda huu ni UKWELI kuhusu MTU YOYOTE yule!:-(

>> Thursday, July 16, 2009

Ukimtafuta MTU mapungufu,....
.... utamkuta na MAPUNGUFU.


Na kwa mapungufu,.....
.... anaweza kukunyoshea weye kidole....

.... huku haoni YAKE mwenyewe MAPUNGUFU.


Na jihadhari na ajulikanaye kwa kukosa mapungufu,....
.... na kama ni yeye mwenyewe ajishabikiaye wako ole.....
....na utakoma mwenyewe ukistukia afichalo lake PUNGUFU.


Lakini kwanini mtu atafute la mwingine pungufu,...
....wakati maishani muda hautoshi hata kujinyoshea mwenyewe kidole....
....katika jitihada za kusawazisha hata lako mwenyewe PUNGUFU?

Swali:
  • Hivi ni yako mangapi unafikiri hayana UPUNGUFU?
  • Hivi huwezi kutafsiri mahangaiko ya binadamu katika kusawazisha mapungufu kuwa ndio yajulikanayo kama MAISHA?

NI wazo tu KIJEBA usitishike!


Ngojea tubadili hali ya hewa kwa kutoka kwa binadamu na kuangalia ya MAJINI...




Au ngojea tu ALPHA Blondy amuongelee- Fanta Diallo

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Fadhy Mtanga 4:11 pm  

Imetulia.

Simon Kitururu 4:17 pm  

@Malenga Fadhy: :-)

Yasinta Ngonyani 6:45 pm  

:-(

Christian Bwaya 5:17 pm  

Ajabu kuna jamaa huwa wanaaamini hawakoseagi. Hawajapungua.

Kaka tuko wote. Darasa tamu

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP