Katika KUOMBA,... .... unaweza kuomba mpaka TAKO!:-(
LAKINI tako LAKO linaweza lisiwe na manufaa KAMA ya TITI ingawa huo ndio UKWELI usio tako kwa ATAKAYE kubonyeza TITI!:-(
DUH!
Kuna sababu ,... .....na ni kawaida KUOMBA ingawa unaweza KUJISIKIA vizuri baada ya kuomba ,.....
....UKIPEWA.....
.... kwa kutumia VIGEZO a.k.a ZE vigezo VIHALALISHAVYO ni KWANINI uliomba MKEBE,.....
.... WAKATI,....
.... wakati ulitaka KIFUTIO TU kwenye MKEBE , na sasa una MKEBE wenye BIKARI na hakuna KIFUTIO kwenye mkebe.:-(
Swali:
Unakumbuka kuwa huhitaji kukumbushwa vigezo vya KUCHUCHUMAA KWA MZOEA CHOO CHA KUKAA kama swala ni KUNYA kwenye choo cha shimo ?
Unakumbuka kuwa pamoja na maringo yote ya kuchambia maji LABDA wewe ni shujaa wa KUTAWADHA kwa mchanga UKIPEWA nafasi?
Kinamna labda TUMEZALIWA na hatukuomba waliotuzaa WAJIFUNGUE sisi!:-(
Na,... .... Maisha si ukweli kuwa ni RAHISI ingawa usijinyonge lakini kwa kudhani NI RAHISI vile kuamua kuendelea KUISHI! Swali:
AU?
Katika kumuomba MUNGU yote hata yale ya kutaka kufuta makunyanzi ya CHUCHU, si ni KAWAIDA asilimia TISINI za tuombayo hata yasiyo na uhusiano na titi hata la kiume, si HATUJAPATA au MWENYEZI hatupi ndio maana tunaendelea KUOMBEA MPAKA chakula kilichopo mezani badala ya KUSHUKURU?
Hivi wanawake wanakumbuka wanaume wana CHUCHU ambazo sina uhakika wameumbwa nazo kwa sababu gani ingawa labda wewe unajua?
AU?
NIMEACHA! Kumbuka NAWAZA tu na LABDA ni UJINGA!
Ngojea twende CONGO Classical Symphony Orchestra walete - Carmina Burana
Au tu Youssou Ndourna Koffi Olomide walete - Festival
Kama unaamini huna WIVU,... ..... labda USIOMBEE kugundua GHAFLA una wivu USIJE ua MTU na BATA WAKE ghafla!
Na,.. ...kila siku TUNAFIKIRI na KUHISI..... Swali:
Unakumbuka kufikiria UNACHOFIKIRIA na kukumbuka ULICHOFIKIRIA jana na KUKIFIKIRIA tena leo?
Unakumbuka huwa HUKUMBUSHWI kuhisi?
Ukifikiria sana, LABDA unavyofikiri unavifikiria bado UNAVIHISI.
Na,... ....labda kama unafikiria HUNA wivu, basi wivu wako LABDA umelala na sina uhakika kama ni afya uuamshe udinde au tulia katika mkao huohuo wa sina WIVU ubakie umelala kwa utulivu!
Swali:
Au unahisije wewe baada ya kufikiria hili?
Labda kuna UKWELI kuwa ,.... ...kila mtu anastaili na mkao wake wakusikilizia WIVU.
Labda kuna UKWELI kuwa,... ...kuna mwenye wivu na MKE WAKE na mwenye wivu na SEHEMU ZA SIRI za mke wake.
Na labda,... ..... wakati SHOGA anakuonea wivu , HATAKI KULA vyako, bali anataka usiwenavyo ULAVYO ili apate nafasi ya KUKUTETA kwa kisauti kisikikacho kikisema; ''Sasa tulione litaringia nini sasa hivi wakati HALINA NANIHII, lione vile mwanya kama PENGO!'', halafu wala ASIMENDEE ulichokuwa una KULA kwa rahaaaa!:-(
Swali:
Si unakumbuka roho ya kwanini?
SINAUSHAHIDI!
Lakini,... ... naamini unaweza UKAHISI halafu UKAFIKIRI bado unafikiri wakati UNAHISI tu utakiwacho SASA HIVI KUJUA baada ya KUFIKIRI na KUHISI.:-( Swali:
AU?
NIMEACHA na WIVU SINA!
wiKIENdi njEMa!
Pumzika na Francky Vincent akizungumzia- Fruit de la passion
KUNA watumiao madawa ya KULEVYA,... .. na walao MAPARACHICHI.
KUNA walewao na DINI za KULEVYA,... ....na kwa michikichi wavimbiwa na CHIKICHI.
Katika ya BINADAMUUUU!
Mpaka ya MUNGU wafanya KIBINADAMU.
BIN-ADAMU mwenye DAMU!
Katika kuhakikisha ya MUNGU kibinadamu,... ......atetea miti akimwaga damu.
BINADAMUUU!
Hahitaji KUFUNZWA kupumua na AKIPUMUA astukia kuna damu.
BIN-ADAMU!
HUSAHAU anapumua na ana damu kama TATIZO si KUPUMUA au DAMU!
BINADAMUUU!
----------------------___________-------------------------------------- Nawaza tu Mkuu!.-(
Tutulie tena na DELINQUENT HABITS watukumbushe- Goodtimes
AU tu Delinquent HabitsFTHurricane G (bado ni enzi zile)... wazidi kutukumbusha katika -Underground Connection.[jihadhari na lugha za chooni kama msikiliza maneno]
Please do vote for my short story – Jasmine – and ask your friends to do the same. Please go to http://www.dailywritingtips.com and vote!!!!
Meanwhile, do visit my website - www.sandrasden.com –where you will find more short stories, waiting to be published. Do visit the forum please and post your thoughts please.
HutekenyekiNG'O kama hujakaa mkao wa kusikilizia MTEKENYO! Swali:
AU?
Na akupendaye... ...... ukimstukia anafurahia ukicheka AKIKUTEKENYA, unaweza kujifanya UNATEKENYEKA mpaka UKAJISTUKIA mwenyewe jinsi ulivyobarikiwa UIGIZAJI MZURI kwa kuangua kicheko mpaka UKABANJA KIDOOOGO , wakati umeguswa GOTI wakati UKWELI ni kwenye KIKWAPA , chini kidogo ya KITOVU na kwenye wigo wa KIUNO , karibu na mipaka ya shanga TU ndiko UNAKOTEKENYEKA mwanawani weye na GOTI lako linauma.
Na,... ...HAICHEKESHI kama hakuna KITU KINGINE ukijuacho kisababishacho HIKI kikuchekeshacho udhani KINACHEKESHA.
Na,... ......AKUTEKENYAYE ukacheka, kunauwezekano umemruhusu AKUGUSE MWILI na KITEKENYEO ndio maana KAKUTEKENYA ukacheka badala ya KUMPIGA NGUMI pana, KONZI la nguvu, au tu KUMPIGA NGWALA baada ya KURUKA KICHWA , na wakati UMEMPIGA ROBA ukawa unaachia MSONYO MREFU na TUSI LENYE UJAZO ambalo kama sio la nguoni lihusianalo na mama yake, basi ni lile lifananalo na ;'' Mende wee nenda katekenye kuku wenu hukohuko! Nyooo !Lione vile!''
Na,.. ...AKUCHEKESHAYE bila kukugusa , kuna uwezekano UNAMSIKILIZA au KUMUANGALIA kitu ambacho siku hizi kinasahaulika duniani, mpaka imefikia siku hizi BIN-ADAMU WENGI kufikia kupeana MPAKA mimba BILA KUANGALIANA na kabla ndoa haijafa, HAWASIKILIZANI.:-(
Swali:
Unakumbuka ulimi pia ni kitekenyeo?
Kumbuka tu kuwa,... ...UKIJIWEKA TAYARI , kumbukumbu hata za ulivyowahi KUTEKENYWA zinaweza KUKUCHEKESHA au KUKULIZA!:-(
Na kumbuka,... ... UKITEKENYWA sana UTALIA:-(
NIMEACHA! Kumbuka NAWAZA tu MKUU!
siKU Njema! Tutulie na Classic Rumba kutoka kwa KEKELE akidai -DELALI
Unaweza KUPANDISHIWA sketi wakati UNASUTWA kwa madoido wakati unashushiwa DALILI za tusi MURWAA na adaiye anakupa UKWELI !
Lakini,... ... ni MSAMIATI na mrindimo wa jinsi upewavyo MSUTO na MKWALA ndio hukamilisha FANI katika kuchojoa ugumu wako wa kuumizwa na MSUTO hata ndani ya MKWALA.
Sikubishii lakini kama unaridhika na MSUTO ukibaniwa pua wakati UNASUTWA au unapenda tu kukoromewa UKIPIGWA MKWALA katika kujali kwako USIKILIVU wa MKWALA kama MKWALA!
Chakusikitisha ni,.... .... sanaa ya jinsi ya KUSUTA au KUCHIMBA MKWALA inabidi ujifunze mwenyewe.
Na....
Hakuna TUISHENI ya kuchimba MKWALA!:-(
Hakuna twisheni ya KUSUTA!:-(
.....na darasani WALIMU hakuna!:-(
Uzuri wa KUSUTWA ni uwezo wake wa kukusaidia KUMFAHAMU zaidi AKUSUTAYE hasa kwa kuwa anakuambia mpaka asiyofikiri ANAKUAMBIA, na kukufaidisha kwa KUKUKUMBUSHA kitu kuhusu WEWE MWENYEWE katika DUNIA hii tuliyofikia KUTOJALIANA na kufikia kuendekeza VITA kutokana na kutojulia kumaliza ugomvi kwa MKWALA na KUSUTA wakati amani INABOA.:-(
Swali:
Hivi India na Pakistani si wamesaidiwa kwa KUPIGANA mkwala ndio maana bado vita haijaanza?
Unafikiri kwa mkwala unaUAhamu ya vita?
Unataka kusema hata kama si wewe uliyesutwa au kupigwa mkwala, hujawahi kustukia ULIBURUDIKA kushuhudia hizi SANAA?
Naacha! NAWAZA TU Mheshimiwa! Hebu twende Tanzania CNN wajadili miundo mbinu...
Au tu Mwanadada wa KichagaNAKAAYA alonge---
DUH tubadili hali ya hewa kwa kumuachia Mystikal awaamrishe watu fulanni...-Shake ya ASS[tahadhari lugha chafu kama wewe ni msikilizaji wa maneno kama yule]
Si lazima uombe,.... .... lakini wahitaji KUHITAJI ili uvumiliwe na UKUBALIWE.
Unaweza kujichukulia kwa nguvu lakini,... ..... na watu wakaelewa baadaye kwanini ulijichukulia na UKAKUBALIWA.
Daima,... ....KUKUBALIWA kwako kunauhusiano na mahusiano yako ya MATAKWA yako na watu wengine.
La sivyo huhitaji KUKUBALIWA!
Na hata,... .... katika taaluma ya kutongoza UNAHITAJi mtongozwa ili UKUBALIWE YAKO katika mtongozo. Ila katika ,.... .. taaluma ya MAHUBIRI, ili YAKUBALIWE unahitaji kubobea kwa YASIYO YAKO UHUBIRIYO utakayo KUKUBALIWA.
Kumbuka,....
NI YAKO ya kutongozea UKUBALIWE!
NI YA WENGINE utumiayo KUHUBIRIA ukubaliwe!
Swali:
Katika KUKUBALIWA unafikiri wewe ni MTONGOZAJI au MHUBIRI?
Cha muhimu ni,... .....kumbuka kukubali KUJIKUBALIA.
Wengi hata bila sababu za msingi hawata KUKUBALIA na kumbuka sababu yake kubwa ni kwamba HAWA JAMAA ni WATU bin BINADAMU.
Wasikilize lakini WAKIKUTONGOZA au KUKUHUBIRIA halafu kama unaroho nzuri WAKATALIE.
Swali:
AU?
AU unafikiri hujakubaliwa hata na MUNGU wa upendo?
NAACHA! Tulia na Percy Sledge azungumzie jinsi mwanamme akipenda katika - When a man loves a Woman.
KATIKA... ... IMAJINESHENI za NCHI NZURI, unaweza kumuona MPAKA MWANAMKE mzuri wa KIAFGANISTANI mwenye USHUNGI na kusahau utajiri wake wa TITI KUBWA lenye CHUCHU PANA.
Na,... .... kwa mpenda sana matako KUNA uwezekano asigundue UMEPAKA WANJA na unakucha ndefu kwenye vidole shujaa hata katika kushikilia NANIHII.:-(
Labda,... ....HESHIMA ni kwenda KINYUME au nyuma na utakavyo kwenda mbele AU vya MBELE.
Ingawa,... .... siongelei KIJAMBO cha mbele sasa hivi hapa ,...
...ILA....
kunauwezekano kuwa KWA heshima unajizuia kujamba kwa KUTUNZA heshima ya visivyo hitaji kuwa na UHUSIANO na NENO HESHIMA mbele KWA MBELE.
NI... ... aibu wakati VYA AIBU haionekani VINATIA aibu KWA sababu TU wenye HESHIMA NA AIBU wanavipa KIPAUMBELEvisivyo stahili heshima KWA HESHIMA na aibu.
Swali:
AU?
Unauhakika unamheshimu RAIS wakati yeye pia anajamba AU huna uhakika labda sasa hivi kajamba kiheshima na SI aibu?
Unauhakika kujamba ni KITENDO au labda kuona aibu kwa kujamba HADHARANI au kisiri ndio KITENDO cha AIBU?
KWA heshima naacha hii topiki AMBAYO LABDA NI YA KIJINGA KAMA UNAUHAKIKA, ingawa labda haijanishinda BILA AIBU!
JUMATISA njema!
Hivi leo kunauwezekano sio jumamosi au ngojea nirudie kukuuliza kwa kisauti....
Au nikukumbushe TENA kawimbo...
Au tu...
Kuna adaio aliye kwenye PICHA kuwa nilikuwaPOA ZAIDI miaka fulani ILIYOPITA wakati wa picha hizi BAADA ya hii sentensi ya KIJINGA, ingawa najaribu kujitetea sijabadilika bado ingawa siku hizi ni kweli nataka kumpa mimba mtu kama kuna mwenye huruma bila kumpiga PICHA :-(
Ngojea I-Wayne anikumbushe katika - Cant SATISFY her
Au turudi tu tena nyumbani kwa ALI KIBA azungumzie- NAKSH naksh MREMBO...
...... sababu za kuweka MLENDA kwenye mdomo ni kulenga TUMBO na labda NIA ni kuufikisha tumboni , ingawa labda mdomo ni tobo la tumbo kama hujaziba TOBO.
Kinyeo pia ni USHAHIDI wakuwa TUMBO limetoboka, INGAWA unaweza kuendelea kubabaishwa na SIMULIZI za UTUMBO ukasahau uhusiano wa kinyeo na tumbo wakati tunazungumzia UMARIDADI wa KOO kabla ya TUMBO.
SIKUBISHII ukinibishia lakini!
Pamoja na yote,... .....VITU karibu vyote vinauhusiano kama tu MIMI na WEWE ukiviangalia hata bila UMAKINI.
Swali:
Unakumbuka WEWE na MIMI tunahusiana?
Tatizo ni,... .... katika vilivyotoboka, ni mpaka uwe na mtazamo au TABIA ya kuliangalia tobo na kuanza kufikiria uwezekano wa labda tobo LIMETOBOKA , iliKUGUNDUA labda si kweli kinyeo na mdomo vyote VIMETOBOKA katika huu uhusiano wa haya MAHUSIANO.:-(
Tatizo ni,... ....wakati unaulengesha mlenda kwenye TOBO la tumbo ,ni tatizo kama HUKUMBUKI kilengwacho na yote MARINGO na madahiro ya mlenda si tumbo bali AFYA YA MWILI.
NAACHA! Kumbuka nawaza tu hapa na nakutakia kila la kheri chooni leo!
SikuNjema!
Swali:
Huwa unakumbuka kuangalia mahusiano ya UHUSIANO wa HIKI na KILE?
Unauhakika hujasoma ujinga PEKEE kama umefikia KUSOMA mpaka kwenye sentensi hii hasa kama HUWA huoni uhusiano wa ujinga na akili ?
Ngojea Manu Dibango abadilishe tena hali ya hewa katika-SOUL MAKOSSA
Tutulie na kazi za mwanamuziki nipendaye kazi zake tokea enzi za Tony Toni Tone, Lucy Pearl na hata akiwa solo kwa jina Raphael Saadiq. Hapa nimuache Raphael Saadiq,akiwa na Ali Shaheed Muhammad na Dawn Robinson. katika...kibao....-without U
Au tu niiache kazi yake nyingine akiwa katika Lucy Pearl , kibao cha akinadada kusutana- Don't Mess With My Man
WAKATI unaendelea KUVUMILIA wakati UMENYIMWA na MALAYA,....
.....bado....
AFRIKA inagawa kama malaya na kumnyima iliyomnyima liMTU kama ANYIMAVYO mtu MALAYA.
Labda,... ... AFRIKA ni BARA MALAYA ingawa kuna wanyimwao na MALAYA.
KATIKA..... ... KUVUMILIA ni bado unavumilia kwa kuwa ULITAKA na ukinyimwa ROHO INAUMA KWAKUWA ULITAKA ingawa uko katika uvumilivu na unafikiri imekuaje hunauhakika UTAPATA ya kawaida na unashangaa umenyimwa uliyofikiri ni YA UHAKIKA yake MALAYA.
Wakati UNAVUMILIA bado ni KWELI ulitaka kuifanya hata ambayo sio ya MALAYA ,na kunauwezekano unakumbuka au baada ya kunyimwa NDIO UMEKUMBUKA unaweza KUCHEUA mwenyewe na huhitaji MALAYA.
Swali:
Wakati unafikiria maendeleo umewahi kukumbuka kitu kiitwacho PUNYETO?
KAMA,... .... unavumilia LABDA unafanya na uvumilivu WAKO NI DALILI za kubobea katika KUFANYA.
FANYA BASI! Swali:
AU?
AU unanisubiri MIMI nifanye?
NA ni KWELI,... .... mambo ya MALAYA MTAMU anajua aliyeonja na kula MALAYA.
NA,... .... wengi waongeleao, KUPIGA KELELE au KUMZUNGUMZIA malaya,hawamjui MALAYA Swali:
AU?
Kama AFRIKA ni demu mwenye chunusi unafikiri unge mtoa chunusi kwa kubinya chunusi au kwa kumsifia anachunusi ujualo halidumu kwenye uso mzuri?
NAACHA!
Ngojea nimuache rafiki yanguPapaa Kweba ofisini!Kweba eeh, unanitenga lakini!Tuko pamoja na salamu lukuki!
Ngojea TONY HENRY alete tena muziki aina ya opera katika- NOW we are FREE.
Au ngojea TONY HENRY wa RNB alete za- Redemption Song
DUH!! Basi tupate tu ZUKE kutoka kwa Jacob Devariux na wenzake...
Labda,... ....unapenda rangi ya JIPU LIKIIVA au tu rangi ya NUNDU kesho yake baada ya kupewa NUNDU.
Na,... .... inawezekana WEWE ni MBAGUZI kama unauhakika wa MAANA YA UBAGUZI ni nini.:-(
Swali:
Kama unajua RANGI , kwa kawaida unazungumzia RANGI GANI nyeupe ya MTU kama katika SIMULIZI zako za karatasi JEUPE unazungumzia NYEUPE?
Ushawahi kuona mtu BILA rangi wakati unaangalia mavuzi au masharubu CHOMACHOMA ya MTU?[Samahani kama jina la nywelenywele nyingine inawezekana ni matusi.:-(]
Lakini,.. .....katika kuona KIBOGOYO unaweza kukumbuka MENO na ukajifanya ni kawaida yako kupiga MSWAKI wakati meno yako yameoza na yana rangi ya DHAHABU -MAVI.
Swali:
AU?
Na,.. ... wakati unaona RANGI YA BLUU BAHARINI,ni KWELI inawezekana ukasahau BAHARI HAINA RANGI BLUU na uonacho BAHARINI ni rangi ya anga la BLUU.:-(
Swali:
Kama wewe ni MTANZANIA unauhakika MZUNGU na ALBINO wanatofauti YA uweupe wa rangi wakati kwako MAALBINO ndio DILI?
Unauhakika unajua JINA la rangi yako?
NAACHA!
Ngojea tutulie kwa kwenda CHINA kushuhudia mwanamama AKILIA kwa kuchelewa ndege......
Au TYRA Banks anisaidie kwa kujishebedua katika-Shake YA body
Au tu Whitney Huston arudishe UMAHIRI ingawa ni UONGO katika - I will always LOVE U
Labda,... .... WAAFRIKA TUNAHESHIMA mpaka TUKATAWALIWA.:-(
HESHIMA ni kitu cha bure na labda ndio maana inasemekana WAAFRIKA wanaheshima sana kutokana na ukweli kuwa heshima ni BEI CHEE , kama hukiri kuwa ni BURE, mpaka kwa heshima tunategemea vya BURE na kwa heshima ni MASIKINI kwenye UTAJIRI.
Na,... .... ukisema WAFRIKA wanaheshima sana hasa KWA WENGINE kuliko WAJIHESHIMUVYO WAO, .....
.... naweza kushindwa KUKUBISHIA wakati NIMESHUHUDIA kuanzia WATU mpaka DINI ZA KIAFRIKA wasivyo na zisivyoheshimiwa na WAAFRIKA, na watafiti mpaka wa guenea worms wazinguao Waafrika wako au wanatoka UGHAIBUNI.
Labda ni kweli,... ....SIKU HIZI kuna wataalamu kutoka nje wa mambo ya AFRIKA wakati Waafrika tuko mstari wa mbele katika imani na tafiti za wengine kwa ajili ya WENGINE!:-(
Swali:
Hivi si HIP HOP ni bomba kuliko MDUMANGE, Mdundiko, CHAKACHA na TAARABU kwa pamoja?
Hivi unauhakika Taarabu na Mlimani park JAZZ BANDI ,ni miziki ya Kiafrika?
Hivi WAAFRIKA pamoja na kuuana unauhakika wana na wali-KUWA na HESHIMA?
Turudi katika hoja,.....
Wakati unataka KULETA ZA KULETA za kuwalaumu mafisadi wajanja MTOTO WEYE, kumbuka KIAFRIKA tokea enzi hizo TUNAHESHIMU WAKUBWA na tulitawaliwa salama SALIMINI kwa heshima.
HESHIMU wakubwa weye usije laanika bure wakati unajua kwa kuwa masikini ni rahisi zaidi kwenda mbinguni kuliko tajiri kupenya katika tundu la sindano, na ukikosa heshima UTALAANIKA.
Swali
AU?
Hivi unauhakika UKIHESHIMU utaheshimika hata na waheshimiwa wasiojua heshima ni nini?
Hivi unatofautisha kuogopwa na kuheshimiwa?
Nauhakika tu,... ... wakati WAAFRIKA kwa heshima TUNALALAMIKA, kwa kulala TUNATENDA na matunda yanaonekana katika mkao wa kuendelea kuujaza ulimwengu kwa KUJIFUNGUA akina totoz zenye majina kama MIKAELA na MIKA hata kwa Kihindu, Kiislamu na Kigagagigikoko .
MUNGU IBARIKI AFRIKA!
Au kama na nyie MIUNGU mpo na mna BARAKA kinamna , BARIKINI BASI AFRIKA na WAAFRIKA kama mbarikivyo wengine na acheni NOMA!
AAAGH!
NAACHA! Kumbuka nawaza tu hapa MKUU na labda sitendi!:-( wiKIENdi njEma!
UKIZALIWA unaweza kubahatika kuanza na NEPI au tu lichupi la kanga , shuka au kitenge, kama si linguo tu lililochanwa katika kaptura ya kaka,......
..... katika jitihada za WALEZI kukusitiri TOTO ZURI wakati unajinyea na kujikojole kwa utoto.
Kwa UJANJA na BAHATI unaweza kukwepa kuaga dunia MAPEMA mpaka ikafikia WALEZI kukusitiri kwa NEPI au tu chupi ya kanga, shuka,.... au kitenge , ZEE ZURI usitirike wakati unajinyea na kujikojolea kwa kusahau ya choo kwa uzee.
MAMBO YOTE ni NEPI kulia-nepi KUSHOTO katika dansi hili kama unabahati katika wimbo huu na sebene hili la MAISHA.
TUNAKUMBUSHANA TU na hatutishani!
Swali:
AU?
Bado unauhakika unataka kuishi sana ?
Au unamuogopa Mungu nini ndio maana hutaki kuanza mapema?
Tuendelee na ya CUBA kama CELIA CRUZ adaivyo katika - OYE COMO VA
MAMA tamutamu mwenye ASKARI,... .....najua ushapitia na unajua machungu, tufurahi kwa kuonja ACHALI.
NATAFUTA ya futari,... ... wajua kwa AFUNGAE tamu si pekee ASALI.
WENYE kelele wanatafuta GARI,.... .... mie nitaridhika na mzoefu wa kubinuka akinipa hata kwa kulala CHALI.
WADOGO wasio shuga mama kwenye sinia kubwa la KACHUMBARI,... ...wanajiamini kwa kisimi kikubwa MADHABAHUNI na kufikiri sala zitafika kwakua TUNASALI.
WAZEE walio shuga mama kwenye SAFARI,... ...kutoka Nairobi kwenda HUNGARY, naogopa twawezaishia MALI.
NA magugu ni kitanda cha NGIRI,... ....na kwa ajuaye ajua meno kama ngiri , kwa ngiri ni urembo kama BANGILI.
SHUGA mama mzoefu wa alichokula JUMA na alacho BAKARI,.... .... nimatumaini yangu utanilisha cha Serina , Asha , Rose kwa uzoefu wakati ukinijulia HALI.
SHUGA mama ukinifikisha usije shangaa nikitaka kutoa MAHARI,.... .... unajua safari zetu siku hizi hata kwa TREKTA bado matope mengi na hatufiki MBALI.
Ni kweli kama tamu nitataka yote KACHUMBARI,... ..... katika uadimu wa nyanya ndogo ZENYE MAKUBWA ,zikifikia mzani nisamehe kwa ULAFI katika hii HALI.
Unaweza kuogopa kuanguka hadharani kwa kuogopa STIGMA iambatanayo na KIFAFA ukianguka badala ya kuogopa MAUMIVU ya kuanguka , wakati kuanguka ni kawaida hasa kama umewahi kusimama au kutembea, ingawa kama WEWE ni mjanja , inawezekana ulishawahi kuanguka wakati umelala.
DOGMA zaweza kukusababishia usijiulize uwezekano wa uwepo wa MUNGU WENGI au SHETANI WENGI kutokana na kuaminishwa kuwa kuna ukweli mmoja na ukweli wenyewe ni kwamba kuna MUNGU MMOJA mzuri na SHETANI MMOJA mwenye sura mbaya.
Labda,...
kuna ambaye hafanyi kitu ingawa kinafanyika kwa kuogopa STIGMA.
HAKIPINGIKI kitu ingawa kinapingika kwa sababu ya DOGMA.
Labda,...
DOGMA ni kukana MACHALE yako!
STIGMA ni kuogopa yako TAFSIRI ya machale yako , kwa sababu jamii inatafsiri na kuoanisha tafsiri na kitu .Kitu uofiacho kinakuathiri!
Dosari za stigma ni pale wewe mwenyewe utakapofikia kuamini waaminiyo kuwa ni dosari hata visivyo na dosari kwa sababu kuna stigma iliyojengeka katika jamii hata kama ni ya kuoanisha kula sana na ulafi hata kama kazi yako ni mgonga kokoto na umbo lako ni kubwa kuliko, na sahani kubwa inakuja na hali halisi na si kwa ulafi kwako .
Dosari za DOGMA ni ukweli kuwa ni mtu mwingine yalimshinda kuelewa na kuelezea KWA NINI, na kaamua kuwa HIYO iwe ndio kweli tupu kwa wengine wote na USIBISHE.
Labda,... .... katika kulainisha mambo ya STIGMA unaweza kuunganisha na ya jamii ya KiTZ ya kama labda :
Ukibana matumizi na kama wewe ni MPARE kama mimi, watu wataendelea kufikiri wewe ni BAHIRI kwa sababu Wapare wana STIGMA ya ubahiri.
Hata kama wewe tajiri , ukiomba halafu ikajulikana wewe ni MGOGO, watu wataamini kuomba kwako kuko kwenye damu kwa sababu kuna waaminio ombaomba ni Wagogo.
Ukiiba kama wewe MCHAGA kama watani zangu, kuna watakaodhani unatunza na kudumisha MILA na DESTURI kutokana na STIGMA iwalengeshayo Wachaga na wizi.
Tukipenda ngono kama WEWE halafu ikawa sisi ni Wahaya , LABDA kuna....
Nakadhalika tatu katika stigma na....
Na maswala ya DOGMA yanaweza yakakuchanganya hasa katika mambo ya dini ambapo usipoangalia utashindwa kuelewa akusimuliaye kuna MUNGU MMOJA lakini hapo hapo kuna Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu roho Mtakatifu , wakati unamsikiliza adaiye yeye kapatia kwa kuamini kuna MUNGU MMOJA na SHETANI MMOJA katika ya Mungu mengi na ya Shetani lukuki.
Swali:
AU?
Kwani STIGMA ni mpaka iwe ya UKIMWI au UKOMA mtaani na DOGMA aamue PAPA wa Kiroma VATICAN?
Katika STIGMA labda kunamchango wako kama unasaidia kuamini kuwa kuna dosari ambazo zinamng'ang'ania mtu daima na kwa mahesabu yaleyale uliosimuliwa ni MAHESABU ambayo ukitekenya lazima yazae DOSARI.
Katika DOGMA , sema unataka tu kurahisisha ili kujisaidia usijishughulishe kuelewa tofauti.
Swali:
AU?
STIGMA na DOGMA DOGMA na STIGMA ......na labda vyote ni UJINGA.:-(
NAACHA! KUMBUKA NINAWAZA tu hapa! Nakutakia mafanikio MEMA NA MAKUBWA chooni leo!
Tutulie na Dave Chappelle alete busara za kukojoa katika- Piss On You
Au DAVE Chapelle aendelee katika- NIGGAR FAMILLY
AU tu Burning Spear a kumbuke katika -Days of Slavery
Kuna watakaodai ukila si lazima uonje kama ladha hakuna, kama tu watakaodai shughuli ya leo muhimu ya viumbe ni kubugia ili kuishi hata kama kiumbe KINA kionjea ladha.
SIKUBISHII!!
NA,.. ... wakati unajiandaa kujitetea kuwa huonjeki, WAULIZE minyoo na mafinyofinyo makaburini ni watu wangapi wameshawaONJA!:-(
Katika safari ya kumalizia safari ya umeumbwa kwa udongo na utarudi kwa udongoni , LABDA ni lazima uonjeke ili ugeuke udongo.:-(
Swali:
Hivi busara za majeneza ya chuma kama sio almasi kwenye kaburi la sementi si nikumuingilia Mungu na vipingamizi katika kuhakikisha alivyokuumba kwa udongo usirudi kuwa udongo?
Unakumbuka kama huna dhambi na ukafa bila kuwahi kufanya dhambi na kwenda mbinguni ,labda si utaanza kujiuliza utamu wa dhambi ulikuwa ni nini?
Wakati unadai huonjwi , usiende kwa daktari asije akahakikisha uogopacho kwa kusema kuna virusi na bakiteria vinavyokuonja sasa hivi hata kama hujisikii kuumwa leo kama jana!:-(
SAMAHANI KAMA ninakukwaza ingawa naamini kama unadini fulani kuna uwezekano ukatubu na kujisikia vizuri. Swali: AU? Si dini ni za kuwasikilizisha watu VIBAYA au VIZURI kutokana na mahitaji ya mfuata dini?
SIkunjeMA!
Namuachia Nusrat Fateh Ali Khan atupe muziki aina ya QAWWALI katika - Improvisation..
Au tu NIN na mshairi SAUL WILLIAMS wazungumzie- List of Demands
NAACHA! Kumbuka nawaza tu na usitishike usiponielewa ingawa labda kuna watakao nielewa naongea nini kinamna!:-(
Swali
Hivi mpenzi wako UBWABWA ni mzuri na anakaribia kufanana na yule umpendaye AKILINI-MUKICHWA au katika fantasi za WALI?
Hivi unauhakika ndoa ni zaidi ya neno ndoa wakati bado MWILI WAKO uko kwenye ndoa na MAWAZO YAKO yameacha MWILI na YANAJARIBU ndoa IENDELEE kufanana na uaminicho ni ndoa?
Mke mmoja Wanaume sita si ni NDOA kama ilivyo kwa Mume mmoja Wanawake ishirini na nusu?
Kuna WATU WEUSI wafikiriao na KUAMINI rangi nyeusi ni ishara ya kitu kibaya kama tu wabaguzi wa watu weusi wajaribuvyo kuwaaminisha watu kuwa MTU MWEUSI ana kasoro na ni MTU MBAYA. Swali:
Si umecheki walivyofanikiwa eeh?
Unaweza mpaka kuwasikitikia WATU WEUSI ambao wanadiriki mpaka kutamka kuwa RANGI NYEUSI nishai na ni rangi ya mavi kwa mapungufu yao ya kugundua kuwa mavi yana utajiri wa rangi nyingi.
RANGI na MAANA ZAKE hutofautiana karibu kila mahali.Kuna nchi rangi nyekundu ni mbaya na inaashiria maovu wakati katika jamii nyingine rangi hiyohiyo ina ashiria MAFANIKIO. Swali :
Samahani kwakukuuliza; lakini hivi unafikiri tokea uzaliwe mpaka leo umefanikisha vinyesi vya rangi aina ngapi?
Tukirudi kwenye hoja........,
Kuna watakao sifia suti NYEUSI kama tu Benzi JEUSI kuwa zina rangi ya heshima na mafanikio, wakati wakikataa kuitwa WEUSI kwa sababu za;
Weusi
Giza, Usiku, -Maana yake huoni vizuri.
Mtu mweusi ,-maana yake si mweupe.
Nguvu za giza, nyeusi ,- maana yake ni za shetani.
na..
...nakadhalika tatu na nusu, ya kitu kilichowatoa kujiamini kwa kuwa WEUSI .
Swali:
Umeshastukia KIDUME mpenda ngono hupenda kuiingiza kitu sehemu za giza asizoziona vizuri kwa furaha na hahitaji tochi?
Hujawahi kugundua nguvu waziitazo za GIZA hufanyika zaidi MCHANA kwenye mwanga?
Bado unaamini shetani ni mweusi na JINI ni mweupe?
Kumbuka SIRI ya DUA la KUKU kutompata MWEWE ni ukweli Mwewe hana imani na hajui kalaaniwa na KUKU.
WAKATI Mtu MWEUSI..... .... anaamini UWEUSI ni LAANA , labda kwa AAMINIYE inakuwa kweli LAANA.
Cha kufurahisha,... .... tupo ambao tunajua kuwa kuna ulaini pia uletwao na kuwa MWEUSI.
Cha kusikitisha ni,... .... WAPO waaminio kuwa kwa kuwa WEUSI wamelaaniwa na watakao tumia mpaka vitabu kama BIBLIA kuhalalisha.:-( Swali:
Kama hakuna aliyewahi kuona ROHO, WEWE kakuambia nani kuna WENYE roho NYEUPE au ya RANGI ya MAVI?
Kuna UWEZEKANO kabisa...... ...... ukitulia kisaikolojia UTASIKILIZIA vizuri.
UKITULIA utakuwa na uwezo zaidi wa kufuatilia hatua za utamu ZIKUSOGELEAVYO kabla ya KUSIKILIZIA ingawa unajua unaonja nini.
Kama hujui uonjacho,... ....UKIKUZA sana TEGEMEO la UKUBWA wa paja la utamu wakati hujui utamu wa bata na hukuona BATA aliyechinjwa, unaweza usiridhike na KAPAJA ka kuku utakakopata ingawa bado kuku ni MTAMU.
Labda Kisaikolojia,... ... ukiamini itauma au itaumiza kunauwezekano ikawa CHUNGU au usifaidi utamu wakati uonjacho ni kitamu kwa kuwa unahofia labda ni kona ya pili yenye UCHUNGU ingawa MASAJI upewayo ni FULU UTAMU kona hii. Swali:
Nashauri,... ..... tuendelee kupinga mkeketo wa NANIHII kutokana na madhara ya KIAFYA, Kisaikolojia na hata ya KIKUJINOMA.
Tukumbuke tu! ......Ukichomoa uwe na CHA kuingiza kama hutaki kishimo kibakie kitupu.
Kumbuka,... ...hata kama unataka kuacha POMBE, jiandae kuwa na KITU kingine kitakacho CHUCHUMAA pale ULEVI ulipokuwa unachuchumaa , la sivyo utarudia POMBE a.k.a KILAJI tu, kama umeacha tu na KIU ipo tu na haina tiba tofauti ijaziayo palipoachwa na KILAJI.
Kumbuka pia moja ya kiwafanyacho watu waende KISIMANI ni kwa sababu za kuishi katika mazingira yenye KISIMA la sivyo kama katika mazingira kungekua hakuna KISIMA , labda tungeweza kwenda NAO kuvizia mademu bombani. Swali:
AU?
Kwa hiyo wakati unaacha au kuachisha, jiandae au ANDAA vilevile MAZINGIRA yasaidiayo ari mpya na nguvu mpya ya MUACHO . Na kama nia yako ni KUOKOKA na KUACHA POMBE , labda kwepa walevi na jichanganye na WALOKOLE, ingawa labda kama unajiamini , unaweza kuwa Mlokole wa Kikristu ujichanganyaye na waislamu na kuzawadiwa KUJUA zaidi ulokole na UISLAMU. Swali:
AU?
Si sehemu watumiayo kisima , watu wanaweza kuridhika na bomba la maji kama tatizo ni MAJI?
Kuna waliofanikiwa kuondoa JANDO na UNYAGO bila kuwa na elimu nyingine imfunzayo KIGOLI shughuli na KIDUME aliye balehe KUSHUGHULIKA , matokeo yake SHUGHULI NA NDOA zinashindikana na tunalaumu TV na MAISHA MAGUMU , ingawa pia siku hizi KUNA wajanja wanafikiri somo litolewalo na SOMO linatosha kufunzwa kwa siku moja kwenye KICHENI PATI .
Somo lililohitaji MKUFUNZI ahakikishe MWANAWANI anapitia UCHUNGU na UTAMU, siku hizi lina WAKUFUNZI wasisitiziao UTAMU TU na ni kwa siku moja, kwa kuandaa LIMTU kwenye maisha yenye MACHUNGU labda zaidi ya utamu.
NI muhimu UKISHACHOMOA , ingiza kama unataka mchezo uendelee. Swali:
Unafikiri madhumuni ya maumivu ya Kidume kukatwa jando bila ganzi yanatimizwa na Kidume akikatwa maeneo na ganzi hospitalini?
Hivi madhumuni ya JKT ilikuwa nikuwatesa vijana Tanzania?
NA ,.. ..... ni muhimu kabla HUJATOA na unajua kuna madhara ya KISHIMO kubakia kitupu, UJUE utaingiza nini katika kujazia.
SI lazima kama ukitoa SEMENTI , ukijazia UDONGO utakuwa umedhoofisha UMADHUBUTI wa KISHIMO. Labda SEMENTI ilikuwa inaumiza tu KISHIMO na kujazia kishimo KWA unga wa ULEZI ndio ilikuwa na NI dawa ya NYUFA.
Swali:
AU?
Kumbuka,... .... wakeketaji walikuwa na sababu zao na jaribu kuzijua kabla ya KUTOA na kujikuta hauna cha KUINGIZA, au tu kujikuta kuwa kutokana na kutokujua PICHA NZIMA unashindwa kutetea hoja zako za KUCHOMOA hata kama una cha KUINGIZA. Swali:
Hivi ukijua ni lazima uchomoe na hujui cha kuingiza, uiachie MUMOMUMO nini?
Kwani ukiacha ya SHETANI ni lazima ufuate ya MUNGU?
Naacha! Topiki IMENISHINDA:-( Tuendelee kuwepo South Africa kwa Busi Mhlongo katika- Urbanzulu
Au tu twende PANAMA kukutana na KAFU BANTON enzi hizo kabla watu hawajastukia Reggaeton katika - EL MAD MAN
Ni kweli,... .....CHA AJABU ni kwamba jamiii imeamua kukataa mambo fulani yasiongelewe.
Lakini,..... ......MAMBO yanaendelea KUFANYIKA katika jamii ingawa hatutakiwi KUYAONGELEA.
Tatizo ni,.... .... jamii na JAMII hutofautiana na MIIKO ya jamii moja ni ruksa katika jamii nyingine.
Wakati jamii moja ni mwiko adhabu ya KIFO, nyingine kifo ni jambo la kawaida na KAMA WEWE MWANAFUNZI ukiandamana, hukawii kupigwa virungu na ukifa poa tu.
Na,... ....kuna JAMII ziaminizo ni mwiko kula kwa mkono kama tu waaminio kula kunahitaji KIJIKO, UMMA na KISU.
Swali:
Hivi JAMII ndio akina nani kama wewe hauhusiki?
Si labda KUTAWAZA msalani ni kuchezea mavi ingawa ni mwiko kuwa na huo MTAZAMO katika JAMII?
Miiko NI KIBOKO na inaweza kumfanya MUISLAMU ajifanye MLOKOLE kama jamii ni ya KILOKOLE.
Na,.... ..... MWANAKIJIJI anaweza kufikiri ni lazima ajifanye ni MTOTO wa MJINI kama anahisi kuna MIIKO inayomkumbusha kuwa hayuko KIJIJINI kama tu Msenge ajaribuvyo kujifanya basha maeneo mengine.
WAKATI katika jamii MIIKO inaweza kumfanya MKATOLIKI ASIKIRI kaokoka, MLOKOLE anaweza akamkana YESU katika kusawazisha ya KIDUNIA kama ya KUOPOA NGOMA.
Labda,... .... sababu za MENGI kutoongelewa ni fikra kuwa:
SI heshima KUNONG'ONEZA
SI busara KUONGELEA
NI aibu KUSEMA
NI matusi KUSIKIKA
AU
....LABDA hatuna uhakika na MAANA ya UYASEMAYO nayanachangiaje katika MUONEKANO WAO katika JAMII hata zaidi ya MUONEKANO WAKO.
Tatizo ni,.... ...... ukichukua muda kufikiria ni kwa nini jamii INAMTISHA mwanaJAMII , unaweza kugundua ni kwa sababu MWANAJAMII HUTISHIKA.
Swali:
Unakumbuka lakini kuwa hata ukianguka sokoni kwenye UMATI wa watu , ni asilimia ndogo sana tu ya watu inayoweza kushuhudia UMEANGUKA au hata kukumbuka ULIPIGA chini?
Ushawahi kusikia AIBU kwa afanyayo MTU mwingine wakati hakuhusu na afanyayo HAYAKUHUSU?
Kwanini?
Ushawahi KUJIPENDEKEZA kwenye sifa za MWINGINE hata kwa kudai unauhusiano naye au mnatoka kijiji kimoja wakati HAKUHUSU na yake HAYAKUHUSU?
NAJUA baadhi ya niandikayo hapa kijiweni KUNA waaminiyo hayafai kwa kubwa zima KUONGELEA.
Lakini narudia,.... .... JAMII zina TOFAUTIANA kutokana na wanajamii KUTOFAUTIANA. ......JAMIII zinaendelea KUTOFAUTIANA kutokana na WANAJAMII kuendelea kutofautiana.
Na,.... ......JAMII zilizotofauti ZINAENDELEA kuungana hasa kwa jinsi DUNIA inavyozidi kugeuka KIJIJI.
Usishangae kupigwa BUTWAA kila kukicha kwa kushuhudia MIIKO ikivunjwa kuanzia kwenye TV yako sebuleni mpaka kwenye uchochoro wa pembeni ya KANISA lako , MSIKITI wako , SINAGOGI lako au PALE uchochoroni, pale kati ya BAFU na CHOO chako.
Lakini,... .... MIIKO ni gundi ya jamii na kama unavunja MIIKO kaa katika mkao wakujua kuwa BINADAMU ni king'ang'anizi wa MIIKO aliyoizoea imfanyayo aamini ANAELEWA na KUJIELEWA.
UKIVUNJA miiko unaweza ukawa ni tishio katika JAMII na BINADAMU kama MBWA KOKO , si kila mara ukimtisha anakimbia.
Mara nyingine BINADAMU kama MBWAKOKO ukimtisha akajisikia unamuweka kwenye KONA , anaweza kukung'ata MAENEO kama MJUSI tu.
Swali:
LEO umekwepa KUONGELEA mangapi kwa kuhofia JAMII itakuelewaje?
SI unakumbuka JAMII inaweza kuwa MAMA, Baba, DADA, Kaka, Mchumba, Kimada, Rafiki wa Mpenzi wako utamaniye KUMKONYEZA,.....na WEWE?
Tukumbuke tu LABDA,... .....katika JAMII kuna wakwepao NYAMA YA NGURUWE na kula YA MBWA, kama tu ambavyo wapo wakwepao NYAMA YA MBWA na kula YA POPO . Na hata kama mambo yote ni MCHICHA , mwiko wako wa kula PEREGE labda haumuhusu mwenye mwiko wa kula SATO kwa CHUNGA.
SHIKILIA yako yenye MAANA kwako, YA wengine kama hayakuathiri wewe WAACHIE wenyewe WAHUSIKA hata kama yaletayo maana kwa WAHUSIKA ni KUCHEZEA mikojo.
Swali:
Miiko ya Mkatoliki Itali unafikiri inafanana na MIIKO ya Mkatoliki TANGA?
Miiko ya MUISLAMU Yemeni unafikiri inafanana na MIIKO ya Muislamu KAGERA?
HIVI miiko yako SEBULENI inafanana na ya CHUMBANI?
Hivi DINI yako sio KIONGEZO cha mkusanyiko wa MIIKO yako na labda SI lazima wengine IWAHUSU?
NAACHA MAHUBIRI! Topiki imenishinda!:-(
Twende South Africa kuangalia somo katika -Music and apartheid in South Africa
Au tu huko huko South Afrika , Black Mambazo & PJ Powers wazungumzie -Knocking on Heaven's Door