Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

CHEKA BASI! Usitukasirikie wakati ALIYEKUKASIRISHA hajui kuwa KAHUSIKA!

>> Tuesday, February 03, 2009

TATUZI la tatizo husika,
.....labda ni kumweleza aliyeHUSIKA.

N
a hata leo ni siku HUSIKA,
...... kama UMENUNISHWA na bado hujamwambia MHUSIKA.

NA bado ni masika,
......hata kama hakuna mvua za MASIKA.

NA usituonee kwa kutufulisha SHUKA,
........wakati shughuli za KULITIA MADOA shuka hukutualika na HATUKUHUSIKA.

ETI kuniona unakasirika,
... wakati hata mipaka ya salamu SIJAVUKA!

MJULISHE mhusika,
........au usituzingue na mkasirikie ALIYEHUSIKA.

LIONE vile lilivyonuna mpaka sura lataka PASUKA!:-(
-----------------------------------------------------------------------------------
NIMEACHA!
NAWAZA TU hapa MKUU na labda wewe si MHUSIKA!



Au tu Jamiroquai wadai- Love FOOLOSOPHY....

AU Beenie Man feat Ms thing and Shawnna waendeleze ridhim ya maisha katika - dude remix(Tahadhari lugha kama wewe ni mtoto au msikilizaji)

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

MTANZANIA. 4:21 pm  

Simon! Wakati mwingine hasa pale mambo yanapokuwa hayaeleweki eleweki wengi huwa inakuwa ngumu kujitambua. Ikifikia hapo basi huwa ni mwendo wa kununa. Cha msingi tusiangalie tunapoangukia. Mi nadhani focus iwe pale tulipojikwaa!!

Nashukuru nimeona umepitia pale nyumbani kwangu na nimeuona mti ulousimika. Simon ww ni mmasai lakini!!!

MARKUS MPANGALA 5:24 pm  

Duh! hii sasa naona kama vile unakuna kisogoni halafu unatamani kuona unapokuna. NI KWELI TWANUNA BILA KUFIKIRIA kituchekeshacho au kitufanyacho tunune

Simon Kitururu 2:46 am  

@MTANZANIA: Nakubaliana na yote uliyosema kasoro swala la kama mimi ni Mmasai:-)
@Markus:Umeniacha hoi kwa kusema ''Hii sasa naona kama vile unakuna kisogoni halafu unatamani kuona unapokuna.''

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP