Swala la WEWE ni MZURI SANA na NAKUPENDA WEWE TU!
>> Wednesday, February 04, 2009
HAMU ya aliyesifiwa kutaka KUMILIKI aina ya SIFA aliyopewa JANA kutoka kwa LIMTU alipendalo , asipoangalia ataendelea kudhani sifa ile YA JANA ipo hata LEO wakati MTAALAMU hana sifa za jana LEO.
Labda....
.... kweli wewe ni mzuri, LAKINI limtu lako kama ni LIBINADAMU , inawezekana halikupendi wewe TU ingawa ukiliuliza bado lina busara zakukuambia;
''NAKUPENDA WEWE TU!''.
STAREHE ya kusikilizia SIFA kutoka kwa MPENZI ambazo usingependa MPENZI awe anazigawa ZE SIFA kwa wengine, usipoangalia UNAWEZA KUZIAMINI NA KUZIDAI sifa za jana LEO!:-(
NA ingewezekana....
.....kuna ambao wangetaka kuzinunulia BIMA sifa au angalau kuzisajili wawe na HATI MILIKI ili hata -ukienda mbele sendema , rudi nyuma sendema ,- sifa za mtaalamu ni zake hata nyumba iungue MOTO.
Swali:
- Kwani wewe unampenda uliyemwambia tu unampenda?
- Kama kuna usiyempenda unauhakika MAZINGIRA YAKIRUHUSU huwezi kujifunza kumpenda?
- SI kuna watu wenye wapenzi maalumu kwa makutano ya gizani NA WANAPENDANA KWA YAGIZANI tu, na kwenye mwanga hatuwaoni?
LABDA ukweli ni....
.....unapendwa KAMA UNAPENDEKA ,lakini watu wengine wanapendeka tu kama wewe UMPENDAYE akiwapa NAFASI ya pendo waonyeshe maringo yao dingilidingili mpaka chini.
Swali:
- AU?
Swali:
- AU?
- SI ni kweli unafurahia kwa sababu unaamini na LABDA hata ingekuwa ni kweli INAAMINIKA lakini huamini, bado usingefurahia MTEKENYO?
NAACHA!
Ngojea turudi tena kwa Waziri wa Utamaduni wa Brazil a.k.a Gilberto Gil anisaidie kusema -'Aquele abraço' / ' Back in Bahia '
Au turudi tu BONGO kwa RAY C asimuliye binadamu wajaribucho kufanya katika...-Na wewe MILELE
2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
DUH! NAWASHWA
@Markus: DUH!
Post a Comment