Kwa MPENZI sura ya MALAIKA! Tupande KIBAJAJI mwenzio BENZI sina!:-(
>> Friday, February 06, 2009
Kwa mpenzi Midomo Mizuri!
 Dhumuni la barua hii  si kukujulia hali tu , bali na kutaka kuharakisha safari ya penzi letu  ifikie pale niaminipo nimelipata penzi lako kiuhakika  ili mwenzio niache KUKUDANGANYA.
Mpenzi Midomo Mizuri kama ya bata, ni kweli  nikikuona  moyo unapiga mdundiko na kwa jinsi macho yako malegevu yanavyoniwashia indiketa  kuwa ni zamu yangu  kupita, napata mshawasha wa ari mpya na nguvu  mpya   yakufika nawe faragha tukafanye ya faragha. Lakini pia indiketa ziniambiazo hii ni zamu yangu kupita zanikumbusha kuwa labda aliyetangulia  alizionja zabibu hizo kwa mitindo ambayo mimi siwezi kuchuma zabibu.:-(
 Mpenzi naombea ningezaliwa enzi zile wazazi na kijiji kizima wangekujua zaidi kuliko mimi na kazi yangu ingekuwa ni  kusikilizia ni lini wazazi wangu watakutana na wazazi wako katika kunirahisishia ujio wako maishani mwangu tule zabibu.
Mpenzi midomo mizuri, mwenzio na wasiwasi pia kuwa hupandi baiskeli, ingawa Phoneksi  yangu iko pimped  na nyuma imeandikwa maandishi kwa lugha ya kisasa ''NO SWEAT''! Tetesi hizo nimezipata baada ya kusikia hata VIBAJAJI hupandi na  ulishawahi kumtukana Kamanda aliyekuja kichwakichwa  kukuchukua na PICK UP  kwa kudai  kuwa kaja na gari la kubebea majani ya ng'ombe na sio kumpakia Kisura Midomo Mizuri.:-(
Mpenzi katika barua hii  naomba kukiri  kuwa  nahitaji huruma yako  ili niache kukudanganya. Nafikiri inabidi nikiri tu kuwa hii misuli sio ya gym bali ni ya kugonga kokoto. Na suti yangu ya Kaunda sio fasheni bali ni kweli ilikuwa ya Kaunda na nilipewa na  hausiboi wa Kaunda tuliyekutana na kuzoeana katika mikutano na semina za mahausiboi za kuboresha jinsi ya kumnyenyekea akupaye kazi kubwa kwa mshahara mdogo.
Na nimeshauriwa niendelee kukudanganya kwa kuwa inajulikana kuwa WEWE unafurahia sana mdanganyo kwa dhati, na wenye busara wanaendelea kudai kuwa nikikuambia ukweli hatua ya ndoa hatutafikia . Na unajua tena mwenyewe dunia tuishiyo kwa wastaarabu kama sisi wa dini za kupokea kutoka kwa wageni kistaarabu  , tendo  la ndoa linahitaji refa au  libarikiwe na Padre au Sheikh kabla hatuja likokotoa kistaarabu.
Mpenzi Midomo Mizuri, wakati najisikia kukuambia ukweli, ngojea nikiri pia kuwa ni kweli sio kila siku unapendeza na ukiniuliza kuhusu nguo zako nijuazo unazipenda kuwa zimekupendeza ,nalazimika kukudanganya kuwa ni kweli zimekupendeza. Ni kweli pia  unanuka sana mdomo nikigongana na wewe asubuhi na  tako lako halitingishiki ukitembea kama nikusifiavyo. Samahani kwa kukiri PIA kuwa hizo ni baadhi za vitu vinivutiavyo kwako sana tu ingawa nasikitika kujua unavikimbia kwa kupiga mswaki na kujaribu kwa nguvu na nusu ya ustadi kutingisha makalio.
Kabla sijamaliza barua hii ningependa kukuomba angalau leo nijitahidi kuja  kukuchukua kazini mwako na BAJAJI. Ni matumaini yangu utachukulia huu ni utani na utapanda bajaji  twende  kwenye nyumba husika  karibu na Shekhe alipo nikiwa na tumaini  labda tutafumaniwa kwenye mkeka na kufungishwa ndoa ya mkeka maana hela za kitchen pati , begi pati na hata Fweza za harusi ya kuhalalishia watu au  kujulisha umati tendo la ndoa RUKSA na labda tunalifanya KIMANDINGO sina !:-(
Nimatumaini yangu kabisa baada ya kusoma  barua hii utatabasamu  kwa kuzani si kweli ni kwenye BAJAJI na sio kwenye BENZI ndio matarajio yangu tutaanzisha ukurasa mpya wa PENZI. Hali halisi MPENZI ni kwamba bado niko kwenye hatua ya BAJAJI ya kukodi ingawa nina PENZI LA KWELI pamoja na kwamba  nilikudanganya ilikupata sikio lako lililozoea kusikia utamu wa asali kuliko wa ndimu. Nasita pia kukiri ukweli mwingine kuwa mwenzio hata  ndoto za Benzi sijafikia Mpenzi.
NAKUPENDA   Mpenzi Midomo Mizuri Cheusi Dawa Mwanambilimbi!
Nakupenda sana na naahidi kukupenda kwenye CHEUSI na  hata kwenye  MKOROGO!
Pata basi busu la kikohozi cha bata MPENZI na kwa mapenzi usiteme!
Nakuahidi nitakuwa mwenye juhudi za kujitolea kwenye shughuli za faragha mpaka kitengo kitapata ujauzito tu Mpenzi!
Nitunzie nafasi angalau ya kigoda kwenye moyo wako Mpenzi!
Tutaonana basi mbele ya ofisi yako ukitoka ofisini tukaendeleze ule mpango vipi!
Au vipi Mpenzi!
Swali:
- Unauhakika Mpenzi ni nini?
- Unauhakika husemi tu na ukweli ni kwamba huelewi penzi wala hujui kupenda ni nini ingawa unadai kwa juhudi mbele za UMATI unampenda hata Yesu au Mungu?
- Unauhakika ni kwanini umeisoma hadithi hii ambayo labda ni ya kijinga mpaka sentensi hii hapa Mkuu?
Au twende tu na Kibajaji maeneo...:-)
AU?


NIMEACHA!
NAWAZA tu Mkuu hapa !
WiKIenDI njeMA!
Tutulie na NANKO arudie kusema.....-.LUCKY U
AU tu Pepe Kalle aseme....-HIDAYA..
AU tu Pepe Kalle aendeleze kwa kusema- Milla....
 
  
 Posts
Posts
 
 




2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Kuhusu mpenzi Midomo Mizuri...hehe, nimesoma hadi mwisho lakini siwezi sema kwa nini...tuseme mie mdaku tu! Kisha kama kawaida mzik nao umenirudisha mbali tena sana,,,nikiwakumbuka wazazi wangu wakiusikiliza mziki wa kina Marehemu Franco, Pepe, Tabu Ley,na wengine wengi...kisha mwenyewe na marafiki angu tukisakata viuno kule Tents eneo la Buruburu Nairobi huko 90's...siku ambazo Lingala ilikuwa imevuma...tukiskiza Arlus Mabele...Koffi Olomide...weh...raha ile tukicheza kochokocho DUH! Nisije nikaema mengi hapa:)
@Serina: DUH!:-)
Post a Comment