Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Twendeni KUMTUKANA RAIS!

>> Thursday, February 12, 2009

Wakati tunajiandaa kwenda kumtukana RAIS,.....
.......... tukumbuke tu kuwa SHAMBA BOY, mtumishi na pia aongozwaye na RAIS kasha tukanwa, anatukanwa kila siku na labda anatukanwa na RAIS.


Utamu na BURUDANI tofauti ya TUSI KWA RAIS ni jinsi ipewavyo UZITO TOFAUTI TU kwa sababu atukanwaye sasa hivi ni RAIS .


Kama RAIS ni mtu kama HAUSIGELI wa RAIS, usishangae kuwa labda ushamtukana Rais bila kufikiria umtukanaye ni RAIS kwa hiyo huhitaji sana kujiandaa sasa hivi kumtukana RAIS.

Au niibe msemo wa Obama katika lugha ya Kiswangliung'eng'e: ''YES WE CAN tukana'', na ukweli ni ''YES tume ZE tukanwa''!

Unaweza kubisha , lakini tusi ni jinsi tu utafsirivyo tusi.


NA...
.... katika KUJIPENDEKEZA KWA RAIS labda ndio aina moja ya tusi kwa Rais kwa KUMSIFIA KAMA ANAWEZA wakati unajua umahiri wa RAIS mpaka sasa hivi umebobea kwa alioshindwa na anayoshindwa kama Rais kiurahisi.


Swali:

  • Kwani sifa za uongo apewazo RAIS sio MATUSI rahisi katika jeduali la MATUSI?

MSIFIE tu RAIS kama HUFIKIRII hizo sifa si kipenyo kwenye TUSI mduara kwa RAIS.

Lakini wakati unamtukana Rais,....
......inawezekanaMWENZIO bado anaendelea kula KIURAHISI!:-(

Nakutakia KILA la kheri wakati unamtukana Rais tusi limfikialo Rais na linasawazisha afanyayo RAIS kwa kukuletea AHUENI sio katika kufaidi kutukana tusi TU kirahisi!

Matusi huhitaji SHABAHA na kulenga tusi kwenye kishimo katika matusi si rahisi!

Swali:
  • Hivi unajua kukokotoa kipenyo cha tusi katika kujua nguvu ya tusi kwa Rais ?

  • Si unauhakika kwa kutukana umeshatoa stimu na unasikia ahueni kwa hiyo Rais anaruhusiwa kuendeleza andelezacho mpaka utakapo mtukana tena baadaye kwa kuendelea kushindwa URAIS kirahisi?

  • Unauhakika simuongelei Rais wa shule ya vidudu hapa?


NAAACHA!

Nawaza tu hapa kumbuka!
Tutulie kwa kwenda Gabon kwa Oliver Ngoma katika nanihii ya- ICOLE...



Au ngojea nimuachie..JACKY RAPON aendelee kulainisha kwa Mi amor.....

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Anonymous 12:08 pm  

Loool bro Simon asante sana kwa Oliver Ngoma nilikua natafuta sana nyimbo zake maana zimetulia vizuri sana.

Simon Kitururu 12:19 pm  

@Mzee wa Taratibu:Hakuna noma Mkuu!Ila kuna tetesi kwenye redio za mabua kuwa Oliver N'goma hali yake si nzuri sana sasa hivi:-(

MTANZANIA. 4:35 pm  

Kama kawaida! Nimeona nyayo zako. Mmh! Kimsingi mjadala wa uraia huwa unakuwa mrefu. Ni vzr tuendelee kutumia makaratasi yetu na vyeti vya kuzaliwa kama utambulisho. Ila tukifuatilia kiuasilia mhh!! nachelea!

Simon Kitururu 2:03 am  

@Mtanzania:DUH!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP