Mr KIBEBERU ndani ya siku! (Hadithi ya KIJINGA -kisogo cha kwanza)
>> Tuesday, February 17, 2009
ILIKUWA jumamosi kama jumamosi nyingine kwa Mr Kibeberu na siku ilianza kwa CHAI na KIPORO cha wali na maharage cha juzi.
Pamoja na kwamba kiporo kilikuwa kimeanza kuchacha kwa mbali, hii haikuacha kumfanya Kibeberu ale huku akiachia tabasamu kwa mbaaaaali huku akisema kimoyomoyo hii ni siku ya kujirusha hasa kwa mtu kama mimi niaminiye katika DINI ya KAZI KWA SANA na baada ya kazi ni KUTOA STIMU KWA SANA tu.
Wakati anamalizia kufunga zipu ya suruali na wakati akijiuliza kuwa kwa nini suruali yake ina zipu badala ya vifungo, Kibeberu aliendelea kutabasamu kwa kukumbuka kuwa jioni hii BENDI aipendayo ya Ochestra MSULI PEKECHAPEKECHA ndio itamiliki mirindimo ya mioyo ya watu mjini katika KUPEKECHA.
...............Kama kawaida saa za kikubwa hazikawii kuwadia na jioni ikamkuta Kibeberu akitumia kujulikana katika mchezo aliozoea wa kutaka kuingia kwenye shoo bure ingawa leo hii bila mafanikio.
Lakini kwa uzoefu wa nyoka alijikuta akijinyonganyonga katika foleni na kwa uzoefu alifanikiwa kuwa miongoni mwa washabiki wa Ochestra MSULI PEKECHAPEKECHA waliokuwa ndani ya ukumbi mapeeema!
Kibeberu ndani ya nyumba alienda na miondoko ya kusalimia awajuao na kuchekea VIMWALI wazuri asiowajua katika kujaribu kuweka jeduali likae katika mtindo wa kurahisisha mtongozo hapo baadaye, yote ni katika KUANDAA matibabu ya kujihami na upweke ujao baada ya shoo ili Kidume asijejikuta yuko pekee ghetto.
Kibeberu kwa unyenyekevu aliisogelea BAA yenye kuonekana kuvutiwa na ushabiki wa wajao kula KILAJI na kuipunguzia bugudha ya kujaa pombe. Wakati Kibeberu anatafakari bei za pombe mawazo ya POMBE SI CHAI na uharamu wa pombe yalimkatiza akilini mara mbili na nusu ,kwa kukumbuka makaripio ya SHEKHE na hata Mchungaji wa kanisa la kijiweni kuhusu madhara ya ulevi.
Wakati anaanza kukumbuka pia maoni ya wazazi kuhusu mambo ya anasa , KIMWANA MWANANA aliyekaa kwenye stuli ndefu pembeni ya baa akifyonza KILAJI akafanikiwa kurudisha ari mpya ya KIMIMINIKA na kilaji kikaagiziwa huku akikumbuka lakini sasa hivi NI kwa mbaali kuwa ; POMBE si CHAI.
Dakika chache baada ya kuwa akijaribu kutatua swala la hivi KIGOLI aliyempita yuko NUSU-uchi au uchi-nusu , akasikia sauti ya PAPAA MSULI ambaye ni kiongozi wa bendi ya MSULI PEKECHAPEKECHA akifoka kwenye KIFOKEO kwa msemo wake uliopo kwenye wimbo wake maarufu mpya,- alisikika akisema; ''GRISI kiunoni weka, MBINUKO pakua!'' na umati ukasikika ukijibu; ''MSULI pekechapekecha na MAkalio BINUA!'''
Mr Kibeberu akatabasamu mtabasamu wa kujua sasa shughuli imeanza!
Mr Kibeberu alifumbua macho na kuiona silingibodi anayoitambua kitu ambacho kilimfanya akenue meno kwa tabasamu la kujua alifanikiwa kurudi nyumbani SHWARI baada ya kimiminika a.k.a KILAJI cha kutosha jana usiku. Wakati anajaribu kukumbuka jinsi alivyofurahia jana usiku akashtuliwa na sauti ya kijambo pembeni yake na ndipo alipo kumbuka hakuja nyumbani peke yake.
Kwa haraka alistukia mpaka yuko uchi na kwa kawaida huwa halali uchi. Kwa mbali akakumbuka jana alikuwa anadansi na kimwana mwenye mwanya wenye ujazo mwanana.Na tabasamu likarudi baada ya akili yake kurudi katika mkao wa tamaa za fisi.
Lakini alipofunua shuka kumshuhudia KIGOLI, alipigwa na butwaa kugundua aliyelala pembeni yake bila nguo ni bibi kizee na hana meno. Wakati anajaribu kutafakari imekuaje yuko uchi na bibi kizee, akastukia gauni jekundu lililoko sakafuni linafanana na la yule kigoli aliyekuwa naye kwenye taa dimu mwenye bonge la mwanya mwanana na denda lenye uzito wa FRESH mtindi.
Ghafla moyo ukaanza kumdunda kwa spidi za sungura wafanyao mapenzi kwa kukumbuka jana usiku hakuwa hata na condom, huku akishindwa kuelewa ilikuwaje mapengo yalikuwa yanaonekana kama mwanya mwanana jana usiku!:-(
HADITHI IMEISHA!
Swali:
- Unakumbuka pombe si chai?
- Unakumbuka kumlinda na kujilinda ingawa wote tumekusikia ukitangazia umati HUFANYI uasherati?
- Bado huongelei ngono na kondomu kwa sababu si utamaduni wetu ingawa uwapendao wanaendelea kufa kwa kutokujua?
- Unauhakika kama umesoma mpaka hapa, huu sio ujinga ulioandikwa hapa?
BAADAYE!.....
Hebu tutulie kwa kushuhudia mtazamo wa HARUSI ya dada na dada katika- SOAP'S FIRST LESBIAN WEDDING..
Au ngojea CYPRESS HILL wazungumzie wao mtazamo katika - Under Mi Sleng Teng
0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Post a Comment