Kama HULII sasa hivi KUNAUWEZEKANO kuna kitu UMESAHAU!:-(
>> Tuesday, February 10, 2009
Kumbukumbu za utamu zinaweza kukusaidia KULILIA mpaka MTU.
Maumivu yanakuliza wakati unaumia lakini kumbukumbu za utamu zinaweza kukuliza wakati unakumbuka hata penzi lilivyowahi kuwa tamu.
Lakini.....
.....KUNAUWEZEKANO kabisa wakati unakumbuka kitu KUNA kitu unakisahau!
USIPOANGALIA unaweza kusahau KUKUMBUKA KWA MAKUSUDI kwa sababu kwa kisiri kuna KITU hutaki kukikumbuka sasa hivi.
Tatizo ni.....
..... hata usipotaka kukikumbuka kama kipo, KIPO TU na kinakusubiria chobisi!:-(
Na ni kweli hata masikini anaweza kupitisha siku bila kukumbuka kuwa yeye ni masikini ingawa ndani ya siku anapambana na kitu ambacho mtu mwingine atatafsiri ni mapambano ya umaskini wakati kwa mtazamo wa maskini anajaribu tu kupitisha siku kala chakula na labda pakulala papo.
Inawezekana kabisa masikini anajitahidi kuishi ndani ya siku na MUDA MWINGI ndani ya siku ya kimasikini MASIKINI hataki kukumbuka kuwa yeye MASIKINI.
Inawezekana kuwa si BUSARA kumkumbusha masikini kuwa yeye masikini kama vipimo vyenyewe vya utajiri haviaminiki.
Swali:
- Unafikiri tajiri sio masikini?
- Unafikiri kwa sababu LEO HULII hakuna kikuumizacho ?
- UNAuhakika sababu za kutokulia kwako sio tu UZOEFU wako wa kulea maumivu?
Wakati MAKALI ya yaliyowahi KUTULIZA hatuyasikii sana sasa hivi, kuna uwezekano kuwa yamezidi na TUMEZOEA TU MAUMIVU!:-(
NAACHA!
SIKU NJEMA!
Tulia tena na Russell Peters katika- SHOW ME THE FUNNY....
Au tu Curtis Mayfield arudie - Superfly Live
0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Post a Comment