Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

STAILI ya kuongea IMSAIDIAYO mhubiri wa dini , labda INA MSAADA pia kwa mtongozaji!

>> Wednesday, February 18, 2009

Katika kila fani wanafani wanastaili zao za kuongea au kushusha kauli KATIKA FANI.

Kama wewe Mkristu, Mkristo ,Mlokole, Muislamu,......., au unatumia tu Waganga wa kienyeji , nafikiri unajua staili ya WAHESHIMIWA WASIKILIZWA katika kumwagia wafuasi KAULI zao hasa za vitisho kabla ya KUAHIDI tamutamu katika FANI.

Mimi binafsi napenda staili ya uongeaji wa kitakatifu wa MAPAPA wa kikatoliki ndani ya fani , na nakiri kuwa huwa wananifanya nijaribu kusikiliza wasemacho ingawa sielewi Kilatini , Kiitali au hata lugha yoyote watumiayo katika kumwaga KAULI kutokana na staili za kumwaga neno kitakatifu zitumikazo katika fani .

Na,...
......katika staili ya kumfanya msichana ajikute anavuta majani au anajikanyaga katika mkao wa nataka-sitaki wa kusikilizia kauli TAMU anazopatiwa na Mtongozaji, inasemekana ukimrekodi anayetongoza utastukia haongei kwa sauti yake ya kawaida.Yuko katika fani.

Na katika fani, hata ukiwa mbali lazima utajua nini kinaendelea watu wawili wakiwa wanapeana kauli hata kama mara hii ni Kijeba anacheza mchezo wa nataka-sitaki wakati MWANADADA anamwaga kauli ya mtongozo ndani ya fani.

Lakini,...
....... binadamu tuko tofauti!:-(


Wengine tumezaliwa tunapenda MDUNDIKO wakati wengine wamezaliwa wanasikia kelele tu kwenye MDUNDIKO.

Nawasiwasi staili ya wahubiri wa kilokole, hata kabla ya KUSIKIA WANAONGELEA NINI kuna watu inawatuliza roho na hao kuna uwezekano wakaokoka kirahisi labda kwa kuogopeshwa zaidi kutokana na staili ya mzungumzaji iwaingiavyo au kwa kuelewa zaidi kutokana na mhubiri kuto waboa kwa staili na kabla ya kwa neno, na kwa hilo labda mhubiri anakuna kipele kwa KAULI kwenye fani.

Kuna wengine ni staili ya mashekhe ya kushusha neno a.k.a KAULI iongezayo uelewa wao wa Kitabu Kitakatifu na ya ALLAH.


Tukirudi kwa mganga wa kienyeji au hata mtongozaji , staili yake inaweza kumfanya mtu akubali jambo ingawa aliyepewa KAULI wakati amejilaza kwenye kitanda chake cha teremka tukaze BAADAYE, atakuwa bado haelewi ni kwanini mambo kama; ya mtongozaji ya;Aisee dada nakupenda sana na kila nikikuona nabanwa mkojo AU ya mganga ya;Lete kijambio cha njiwa jike msenge na mzizi wa jiwe, vilikuwa vinaleta maana sana wakati anapokea kauli.

Bado tatizo ni;...
....tunaamini STAILI ya ashushavyo kauli Mmarekani ni tofauti na ya ashushavyo Mfaransa, na labda ni KWELI ! Lakini ukweli ni kuwa kuna Mgogo wa DODOMA anayeweza akawa anakuna Mfaransa kwa STAILI na kauli za Kigogo kuliko Mfaransa akunavyo Mfaransa mwenzake, kama tu Mmarekani awezavyo kuvutia Mpare wa Mwanga kwa Msuya , kwa staili na UNG'ENG'E labda kuliko awezavyo kulainisha Mmarekani mwenzake mtaa wa jirani kwa kauli , kisa anaongea na ana STAILI za Mmarekani mweusi katika kumwaga KAULI ya fani.

Swali:

  • Ushastukia hata mjinga akiwa anaongea kwa sauti au staili uioanishayo na mwerevu, mjinga haonekani mjinga sana ingawa unajua pointi zake zote hazikuni pointi ingawa anamwaga KAULI?

  • Ushawahi kutofautisha staili na sauti yako ya kuombea msamaha ilivyotofauti na ya kutongozea ingawa zote ni za utulivu na zinamwaga kauli?
  • Si unajua kutongoza maana yake kuomba kwa kubembeleza na sio lazima uwe unaomba nanihii?
Labda ni kweli ,.....
.... staili ya kuongea imsaidiayo MGANGA WAKIENYEJI, ina msaada kwa mtongozaji!
Na labda,....
... Staili ya muhubiri huyu UAMINIYE anahubiri ya nabii wa UONGO haiwezi kutumika kukuokoa kwa kutumiwa na muhubiri mwingine kukuokoa WEWE hata kama inashusha ya NABII wa kweli yenye UKWELI katika staili ya kukugawia KAULI.

Lakini,....
......HATA kama hutaki , ukweli ni kwamba Mtongozaji na Mtongozwaji wapo na staili za kumwaga kauli ZIPO na zina afya kama MNYOO na binamu yake FINYOFINYO!:-(
NAACHA!
Kumbuka nawaza tu hapa!:-(
siKU Njema!


Tulia na Harry Belafonte katika -Man Smart, Woman Smarter....



Au ngojea turudi tena Guadeloupe kukutana na FUCKLY katika kibao -Doudou....

8 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Anonymous 5:16 pm  

Si kweli kwamba eti maneno matamu ndiyo humtoa nyoka pangoni bali ni utaalamu wa mtoa kauli...Lakini si lazima kwanza mtongozaji afahamu mtongozwaji anapenda utoaji upi wa kauli ndiyo utaalamu wa mtongozaji ujipambanue zaidi? Vinginevyo hata mtongozaji shujaa aweza kuonekana kama mlolomaji tu. Ati, ni yupi anayeamua kwamba mtongozaji huyu au yule anajua kutoa kauli kama siyo mtongozwaji mwenyewe? Kama hivi ndivyo, ni yupi mwenye mamlaka ya kuamua kuhusu ubaya na hata ubora wa utoaji kauli - mtongozaji au mtongozwaji? Na mimi nawaza tu!

Anonymous 6:13 pm  

Hivi mkuu simon baada ya kuwaza uandikayo wewe wapata jibu?


amani .rasta hapa.

Simon Kitururu 8:43 pm  

@Profesa: Ngojea tuendelee kuwaza:-(
@Rasta:Ningependa kweli kuwa na majibu yote lakini bahati mbaya au nzuri sipati majibu yote, na kuna wenye busara waniambiao mara nyingine si muhimu kujua jibu kama angalau umefikia kujiuliza swali.:-(

Anonymous 12:40 am  

Anony. hapo juu. Wapo wanaoamini kwamba hakuna majibu. Ati tunajuaje kwamba moja ongeza moja ni mbili - tena mbili timilifu? Inaaminika kwamba hakuna majibu kwani hakuna kitu kilicho timilifu kabisa hapa duniani. Cha muhimu ni kuwaza na jamii zilizoendelea ni zile zenye watu wenye kuwaza - watu waliohoji na kupindua mifumo hata kama hawakuwa na majibu TIMILIFU... Bwana Simoni, mimi niko siriazi. Kusanya posti zako zote utoe kijitabu. Kinaweza kuwa kijitabu kidogo tu au cha kimzahamzaha lakini naamini kwamba kitaanzisha mkondo mpya katika fasihi yetu. Ukiweza kupata na mtu akachora picha za kifalsafa kwa kila posti basi itakuwa safi sana. Na kama unaye mtu aliyeko kileleni, si ajabu ukakuta kijitabu hicho kikavutwa na kuwa cha lazima kwa vijana wetu wa high school. Elimu yetu ni mtambo wa kuzalisha vijana ambao ni makasuku tu - na ni wakati sasa wakatiwa moyo kufikiri. Kijitabu kizuri chenye michoro na mawazo chokozi kama hiki chako kitakuwa mwanzo mzuri wa kuzichokonoa fikra za vijana wetu.

Bennet 1:12 pm  

Staili ya kuongea ni kama utashi tu wa kukusaidia kile unachoongea kisadikike na kuaminika na yule anayekusikiliza

Kikubwa ni kuwa uwe unahubiriwa, unatongozwa au kutishwa lakini kuna vitu ambavyo tunapenda kuvisikia na mara tuvisikiapo ndipo inakuwa rahisi kuviamni na kuafuatisha

kwa mfano unapomtongoza mwanamke/msichana hali ya kukubali ilishaanza tangu aliposimama na kukupa nafasi ya kuongea utakacho, kwa hiyo akiyasikia yale anayoyapenda ndio imani juu yako inaongezeka

Simon Kitururu 1:54 pm  

@Profesa:Nimeanza kushughulikia nikifikia hatua nzuri nitakutumia nilicho ambatanisha unisaidie hatua fulani.

@Bennet:Nakubaliana nawe Mkuu katika mtazamo.Karibu sana Kijiweni hapa Mkuu!

Anonymous 3:40 pm  

"...inasemekana ukimrekodi anayetongoza utastukia haongei kwa sauti yake ya kawaida.Yuko katika fani..."

Umenimaliza mbavu leo Simon!

Simon Kitururu 9:25 am  

@Serina: :-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP