Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

INASEMEKANA kuna siri ya KUJUA kama UGALI UMEIVA kabla ya KUUTOMASATOMASA, kuubonyeza au KUUONJA!

>> Friday, February 20, 2009

LABDA,....
......binadamu ni MALIMBUKENI!:-(

Baada ya binadamu kugundua kuna uwezekano wa kupika, wamesahau kuwa MBICHI NYINGI hulika.:-(


Lakini,...
.. ....inasemekana UGALI hujisikia vizuri ukiliwa kwa mkono , na maswala ya kula kwa UMMA au KIJIKO yana uparura tu ugali na kuutia majeruhi ya dondoshayo njiaani utamu, katika safari ya utamu wa ugali kutoka kwenye sinia kwenda mdomoni.

Na....
.....wakati unajiandaa kufinyanga TONGE la UGALI ni muhimu ujue UNAUNYEMELEA ugali wa aina gani.

Kila aina ya ugali, kuanzia wa mahindi, muhogo, ulezi , BILA KUUSAHAU ugali wa unga wa magimbi, kumbuka UNAHITAJI mbinu tofauti ya mashambulizi hata katika KUUTOMASATOMASA, kuushikashika au tu katika KUUTUMBULIA MACHO ugali, hata KAMA safari hii ni katika kutaka kujua tu kama ugali umeiva au bado bila KUUONJA!

Swali:

  • AU?

Lakini,...
...... nisikudanganye kwa kukataa kuwa hakuna WAZOEFU wa ugali hata wa Mbatata ambao wanajua UGALI WA MBATATA umeiva bila KUUSHIKASHIKA, KUUTOMASA au hata KUUONJA. Na sina uhakika kama hawa WAZOEFU huwa wanatumia harufu au ni mbinu gani zaidi katika utaalamu ,na labda hiyo ndio siri ya UZOEFU katika taaluma.

NA TATIZO....
.... la wote wahangaikiao staili za kutaka kujua IMEIVA au BADO, mara nyingi WAMESAHAU tu kuwa WAHANGAIKIAVYO vinalika vikiwa VIBICHI.

Ni kweli kabisa nakwambia kuwa kuanzia;
  • Nyama
  • Nyanya mshumaa
  • Mchele
  • Wali
  • Unga wa mahindi
  • Ugali

AU
  • Nakadhalika kadhaaa,.....
......VYOTE huweza kulika vibichi hata kama huna ujazo wa njaa WAKUTOSHA.

Swali:
  • Si kuna uwezekano bikira mdogo yuko tayari ingawa mkubwa ndio inaaminika kaandaliwa na yuko tayari ingawa naye hayuko tayari ingawa yuko tayari?
  • Unakumbuka kuna mpaka wataalamu wajawazito walao mpaka UDONGO?


SIKUKATAZI!

Endelea tu KUTOMASATOMASA , kubonyeza au KUONJA kama ni kweli HUZIJUI MBIVU HIZI kuwa ni MBIVU hata ukiwa kona ya saba KULE katika mkao wa KUNYEMELEA huku ukiwa na wasiwasi labda ni MBICHI!

Kumbuka kijiweni kuna KIPINDUPINDU lakini, kabla hujafinyanga tonge !

Na nimesikia kuna wenye busara wadaio ukinawa mikono kabla, INASAIDIA hata kwa kuonyesha umejaribu kujiandaa angalau kwa kunawa kabla ya mashambulizi ya tonge.

Labda,...
..... tutumie tu kijiko!
Swali:
  • SI labda ni kweli ukila vibichi utaumwa tumbo?
  • Hivi sijui tutumie tu kijiko?
  • Si utaumwa tu tumbo au kuharisha kama vibichi vinakuumiza hata ukitumia kijiko?

Lakini,....
... Labda endelea kula vibichi kama vilivyoiva hujazoea, USIJEUMWA TUMBO buuure!

Mimi simo!

NAACHA!
Kumbuka NAWAZA tu hapa!



wiKIENdi njEMa!
Twende kidogo kwa Wakyuba kukutana na Orishas wakidai - 537 CUBA



Au tu tupitie tena Jamaica kwa Admiral Tibet, Shabba Ranks & Ninja man enzi hizo , watupunguzie spidi kwa kitu - Serious times

7 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Anonymous 9:10 am  

duh!

Vibichi vingi vimepuuzwa kwasabau ya hao wakoloni mambo leo.

rasta hapa.

kwao jani wanalikubali kwa sheria zao lakini hapa lilipo chimbuka wanalibana kwasababu ni bichi.

amani mkuu simon.

Simon Kitururu 9:27 am  

@Rasta: DUH!

Mzee wa Changamoto 1:20 am  

Kwani ni nani aliyesema kibichi hakiliki kama hakukila? Labda alikula na hakufurahia. Si unajua kuwa kama hujala huwezi kusema hakiliki? Ukibanwa ueleze kama una ushahidi utasemaje? Unadhani akataaye kutia nanga mtoni akiogopa itatua kwenye "tope" alijuaje kuwa kuna tope kama hakujaribu "kunangisha huko"?
Simo kwenye kutomasana na hasa kwa ugali. Natomasa maembe na mapapai kuona kama limeiva. Tatizo ni kwamba huna uhakika wa embe utomasalo limetomaswa mara ngapi na waliolitomasa kabla yako walikuwa wasafi kiasi gani. Papai nalo ndio kabisaaaa ukilitomasa zaidi linakosa "mjishiko" linapwayapwaya. Kisha linakosa mlaji na kushushwa bei kulazimisha mteja.
Hahahahahahahaaaaaaaaaa. Ama kweli wikiendi imeanza. Nami wacha niende sokoni ninunue embe ama papai.
Bless

Simon Kitururu 9:00 am  

@Mzee wa Changamoto: Nimestukia wewe Mhuni. Hahahaha!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa 11:34 am  

pweee. umenikumbusha mahakamani bukoba. polisi wamkamata mzee fulani na madumu ya gongo, wamshitaki mahakamani kwamba jamaa alikuwa na kinywaji haramu. mzee kauliza, mmejuaje kuwa ni haram? polisi kapayuka, eti tumeonja. mzee kwatukana, pumbafu; haramu inaonjwaga? mimi nilikuwa na dawa yangu ya kikohozi nyie mnaita haramu?

kesi ikawa noma!

Simon Kitururu 10:28 pm  

@Kamala: DUH!

Mzee wa Changamoto 5:13 pm  

Kamala we kiboko. Hiyo imetulia kinoma

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP