Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

LINI Tanzania kutakuwa na CHAMA CHA MAPINDUZI?

>> Wednesday, February 25, 2009

Inasemekana TANZANIA ina WANAMAPINDUZI!

Na,...
....TANZANIA kuna WANAMAPINDUZI.
Swali:

  • Unajua chama CHAO?
  • Unauhakika wanamapinduzi wanahitaji CHAMA?


NAACHA!
Tulia twende Brazil kutulia na Zé Renato na Milton Nascimento

Au ngojea BUGLE aseme- WHAT WE GONNA DO...

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Anonymous 5:25 am  

Naamini kwamba kuna wanamapinduzi Tanzania. Pengine ni wachache na au hawajui wapindue nini. Inawezekana pia kwamba wanaogopa kuonyesha uanamapinduzi wao wakichelea kunyofolewa kutoka katika "kiini". Naamini pia kwamba uanamapinduzi wa wanamapinduzi hujidhihirisha zaidi wanapokuwa peke yao na kwa hivyo hawahitaji chama. Kuwaweka pamoja wanamapinduzi kunawafanya wakerezane, kubutuishana na kufunikana; na kwa maoni yangu hakuwezi kuwa na chama cha wanamapinduzi. Ndiyo maana Che alizikimbia raha za uwaziri Havana kwani aliamini kwamba akiwa na Castro pengine uanamapinduzi wake ungetiwa kunguku. Kwa hivyo, na kwa kifupi, ndiyo kuna wanamapinduzi Tanzania - japo siwezi kuwataja kwa majina - kwani pengine inawezekana HAWAPO!

Simon Kitururu 1:28 pm  

@Profesa: Nakubaliana na kila kitu ingawa natofautiana na wewe katika mimi kuamini kuwa Tanzania wanamapinduzi hawako wachache ingawa nakubaliana nawe labda HAWAPO kwa sababu ; HIVI WAKO WAPI?

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP