UDHAIFU wa utakatifu wa MTAKATIFU SIMON KITURURU kabla hujamdaka AKIFANYA dhambi!
>> Wednesday, February 11, 2009
Dhambi unaweza ukawa umeishikilia kiuno huku  unakataa HUIFANYI dhambi.
NI kweli....
....wakati unamtetea MTAKATIFU,  dhambi ya mtakatifu  huelezeka kwanini yenyewe sio dhambi.:-(
Kubwa zima bado linaweza kukwambia lina uhakika duniani kuna mtakatifu asiye na dhambi ingawa liko kwenye dini ziaminishazo UMATI kuwa  hata toto lililozaliwa sasa hivi limezaliwa na DHAMBI ya ASILI na lisipobatizwa halitaenda kucheza mdako mbinguni.
Bin-Adam katika utaalamu wakutenganisha dhambi na sio dhambi ni mpaka lifundishwe na limtu jingine nini ni dhambi na katika hamu za Binadamu kuwa hana dhambi likikuamini wewe basi dini yako inakuwa ya kweli  kwa sababu ndio itakuwa kirahisi imeshushwa na Mungu ingawa Mungu  pia anahitaji tafsiri  kabla hujakaririshwa ni yupi wa KWELI.
Mtakatifu Simon Kitururu labda  dakika hii hana  dhambi kama unaamini katika sayansi ya KUTUBU bila kutoa sadaka dakika chache baada ya kumalizia dhambi huondoa dhambi.
Swali:
- Tukiachana na mtakatifu Simon Kitururu sasa hivi , una uhakika wewe huna dhambi?
- Unauhakika tokea mara ya mwisho ukutane na Simon Kitururu bado hajapata utakatifu na hana dhambi mpaka baadaye kidogo?
- Unafikiri mtoto wa mjini SHETANI alikuwa ZOBA kiasi kwamba hakujua Kijeba Yesu alivyo karibu na ya Mungu mpaka akaendeleza kutaka kumjaribu Yesu afanye dhambi?
NAACHA mahubiri kwa sasa!
Kumbuka NAWAZA tu hapa na kama unadhambi ambayo ukitubu dini yako inakupeleka mbinguni TUBU tu kivyako !Kumbuka labda hatutapanda basi moja kwenda mbinguni!
Ngojea tukutane tena na Yesu wa KILATINO Jose Luis de Jesus Miranda akumbushe kitu
Au R.E.M waongelee- Losing my Religion...
 
  
 Posts
Posts
 
 




0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Post a Comment