Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

KAMA wewe huandiki historia yako kama uijuavyo wewe!

>> Tuesday, February 17, 2009

Labda...
.... hatujui hata USAHIHI wa historia ya juhudi za binadamu kugundua choo cha shimo ,hata baada ya miaka yote hii baada ya baadhi ya BIN-ADAMU kuchoshwa na safari za kwenda kichakani ambako ukikosea unaweza kujikuta kichaka kimoja na Mama Mkwe mnachimba DAWA.


Na historia yako kama si wewe uiandikayo, inaweza kusimuliwa na ajuaye CHEMBE kuhusu wewe akiwa katika mkao wa kudai anajua mwili wako mzima hata ile chunusi yako KUNAKO.

Tatizo pia ni kwamba chochote kisemwacho juu yako hukutana MPAKA na masikio yenye UDHAIFU wa kuvumilia UONGO uliopo kwa kutopenda kuhangaikia ukweli mpaka UJITOKEZE kuhusu hata ubikira wa Bikira Maria baada ya kujifungua Yesu.

NAACHA!
Kumbuka Nawaza tu hapa MKUU!

SIku Njema!

Tulia na moja ya bendi nizipendazo sana kwa jina NUTTIN but STRINGZ katika kibao -Thunder..

AU ngojea wamalizie na Broken Sorrow

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Christian Bwaya 2:03 pm  

Mzee tuko pamoja.

Nakusoma sana kaka. Maswali yako yanatafakarisha sana. Kila lililo jema.

Simon Kitururu 3:08 pm  

Tuko pamoja Kaka Bwaya!Asante sana kwa kutochoka kuja kunisabahi hapa kijiweni.

Anonymous 6:15 pm  

mkuu simon sijui nianzie wapi?

rasta hapa.

Simon Kitururu 10:58 pm  

@Rasta:Mbona usha anza?

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP