Nimecheki jana na UKWELI ni kwamba nina UKIMWI!
>> Sunday, February 15, 2009
Ukweli ni kwamba sijacheki jana ingawa nacheki mara kwa mara labda kwa kuhisi nipewavyo katika kupakua MARA NYINGINE labda NINAPAKUA zaidi kama WEWE katika staili ya KUJIJAZIA.:-(
Swali:
- Hivi kama KESHO nikicheki tena halafu ikawa ni KWELI kuwa NIna UKIMWI kama MHESHIMIWA naNIhii, UTAJIANDAA KUKATAA kunipa ingawa sitarajii KUKUOMBA unisaidie NANIHII?
- SI unakumbuka kuwa UKIMWI ni ugonjwa tu kama BERIBERI na kwa ujanja wako unaweza UKAWA umeishi SANA kwa kukwepa mpaka ugonjwa wa MDONDO halafu ukawa huoni NISHAI kujinyea ingawa NI KWELI kwa ujanja wako umeishi mpaka UKAzeeka SANA na hukumbuki choo wakati UNAJINYEA na si mjanja?
- Hivi ulikumbuka kucheki jana?
Cheki pia kama ulishakuwa hata katika ajali ya mkokoteni ambayo ulijeruiwa wakati uko na MAJERUHI.
Cheki pia kama katika uteja wako wa magonjwa unawasiwasi na sindano zilizotumiwa kukupa ugoro.
Wakati unacheki kumbuka mtoto wa mjini HIV ukimdaka leo kwa kawaida hata mwezi ujao na mbili haonekani, kwa hiyo rudia tena kabla hujajinoma bila viatu angalau baada ya miezi mitatu.
CHEKI TU ila jiandae kabla ya kucheki kwa sababu jamii imezoea hata kutisha watu kuhusu KIFO mpaka imetisha watu kucheki MDUDU, wakati ukijua mapema unaweza mpaka kupanga maisha yako vizuri na labda badala ya kuhangaika na maboksi ungeweza kurudi kijijini kwenu MVOMERO ukacheze mkulanga katika kufurahia maisha kivyako.
Inasemekana wengi wasambazao UKIMWI kwa makusudi ni kutokana na kwamba hawakujiandaa na baada ya kujua wanafanya yao ya udhaifu ambayo ni kufikiri inalipa kufa na watu.
Kumbuka aliyedaka UKIMWI sio lazima maana yake kafikia mwisho wa maisha na HAJINOMI.
Swali:
- Unafikiri kwanini kuna aogopaye kucheki mdudu kwa kudhani ATAJUA atakufa wakati kuna wajitoleao kufa kwa ajili ya dini ambazo cha maana zifanyazo ni kuahidi YASIYOJULIKANA?
- Unajua inawezekana unao kama ni kweli bado hujacheki ?
Baadaye basi kama SIJAFA au HUJAFA!
Au ngojea tena Tender Mavundla atusaidie tena...
10 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Kaka Kitururu Simon Mkodo, naomba ukajicheki, maana waswahili wanasema lisemwalo lipo na kama halipo basi laja.
Hebu nenda kajicheki kisha tuwekee majibu yako hapa, ili tuanze kukupa ushauri nasaha kama utakuwa umeukwaa..........
@Dada Koero:Lisilo semwa nalo bado lipo. Nimecheki mara ya mwisho mwezi wa kumi na mbili.Nacheki mara kwa mara na mpaka nilivyocheki mara ya mwisho sikuwa nimefanikiwa kuukwaa. Nikiukwaa lazima utajua Dada Koero.
Mimi sio msiri sana hasa katika mambo kama hayo.
Wewe umecheki?
Kwani ni mpaka KiJEBA ajikwae ndio nasaha na ushauri vimtoke anayejua?
Kaka Kitururu,
Mimi Sijacheki na wala sitacheki kwa sababu vifaa vyetu vya kupimia ngoma ni feki, ya nini kufa kwa presha kwa jambo ambalo kamwe sioti kuwa nalo?
Kwa mtazamo wangu Ukimwi unaambukizwa kwa asilimia kubwa kwa kufanya ngono, Je kama hufanyi uwezekano wa kupata utatoka wapi?
Wasi wasi wangu: Je kwa nini uwe unapima mara kwa mara, Kulikoooni....
@Dada Koero: Nakubaliana na wewe UKIMWI unaambukizwa kwa asilimia kubwa kwa kufanya ngono.
Hapo hapo mejibu kuwa kuna bahati nasibu za UKIMWI ambazo zinapatikana kwa nadra hata kwenye ajali ya baiskeli na mkokoteni zifanikishazo kuchanganya hata damu za wahusika kwenye ajali.
Mimi mwenzio NI KUBWA zima halafu sina mtoto wala sijatulia na Mamaa wa mtoto mtarajiwa. Kwa hiyo ata kama ikiwa wewe ndio mama mtarajiwa mpya kwa makubaliano. Cha kwanza mimi hufanyacho ni kutaka kujua status yako KINGOMA. Na siwezi kumwambia Kimwana akacheki yeye tu bila mimi kufanya hivyo.
Natarajia nimekujibu swali la kwanini imetokea ninacheki mara kwa mara. Natarajia kuendelea mpaka nitakapo tulia na mtu mmoja wa uhakika au mpaka nitakapo jua nimeshaukwaa na hakuna haja tena ya kutaka kujua nina UKIMWI lita ngapi.
@Koero: Samahani kama nimekujibu kwa mwandiko wa mcharazo.
Nikijaribu kukujibutena;
Kuna labda kuna asilimia ndogo isiyopata ukimwi bila ngono lakini ipo.
Nacheki mara kwa mara nikipata mtu ambaye nahisi anaweza kuwa mama mtoto na kwa hiyo kuna siku lazima tutacheza bila pipi kijiti kuvalishwa soksi.
Kwa bahati mbaya sijafanikiwa kuwa na mtu ambaye zoezi la mahusiano halikuleta mushkeli na mara zote ni mimi nisiye mvumilivu.:-(
Kacheki tu hata wewe kwani nini?Ukijiandaa vizuri na kama unaamini kuna mbinguni sidhani kama utakuwa na presha kama uhisivyo.
Mwenzio sina uhakika wa kwenda mbinguni na sina presha:-(
Labda nimekuelewa, lakini nahisi hujanielewa?
Hivi kama kama unafanya kwa kutumia kifanyio (Condoms) unadhani hiyo inatosha kukusalimisha dhidi ya huu msinambe?
Je, vipi kuhusu kula denda, kifanyio kitatumikaje ulimini?
Jamani mimi bado nina wasi wasi sana juu ya hili, hebu nitoe wasi wasi mzee wakupima kila mara, wewe una maoni gani.
Wasiwasi Wangu:
Umesema kuw2a hujatulia hivyo kila umpataye shrurti mkapime. Ninavyofahamu mimi mara nyingi inashauriwa ukipima kwa mara ya kwanza inatakiwa usubiri miezi mitatu kabla ya kupima tena ili kupata majibu sahihi. Je kaka yangu Simon Mkodo wa Kitururu, waweza subiri miezi yote hiyo bila kuonja?
Sio kama nakusimanga bali nataka kujua msimamo wako, kabla sijakunong'oneza kitu........
@Koero:
Ukweli ni kwamba mimi naamini naweza kusubiri ingawa sijawahi kusubiri.:-(
Naamini katika matumizi mazuri ya kondom kwa asilimia kubwa unaepuka sio UKIMWI tu bali na magonjwa mengine ya kunako.
Huwa ninacheki nikimpata mtu ambaye nafikiri tutafikia kucheza bila viatu.
Kumbuka nafikiria kumpa mimba mtu ndio moja ya madhumuni ya kutafuta anayefaa kumimbishwa na ambaye anaonyesha anaweza kuwa mama wa mtoto ambaye hatupingani katika fikira za mtoto aleleweje na hatupingani kimaadili ya maisha .Hili ni moja ya jambo ambalo limenifanya nisiwe na mtoto bado.Ingawa kuna ukweli katika wote niliokutana nao kuna ambao nafikiri wanafaa kuwa mama ya mtoto wangu lakini hawanifai mimi na mitazamo yangu ya maisha kitu ambacho naamini kitaathiri ukuaji wa mtoto kama nipendavyo.
Ila ukiniuliza nitakuambia kuwa mimi nimetulia na sio kama ulivyosema kuwa sijatulia ingawa natambua utulivu inatafsiri nyingi kwa watu pia.
Kuhusu denda, hapati mtu kabla sijamjua status yake KINGOMA.Na kwa ujumla mie sio minjoy denda sana.Mara kibao denda linatoka baada ya kujua nina mpenda denda.Kumbuka kuna mambo mengi yakufanya mkiwa wawili ambayo yanaweza kuwa keep busy na wala msimisi denda. AU? Naamini kama mbunifu unaweza kuyahisi.
Kumbuka lakini kuwa hata kwa kutumia kondom mtu anaweza kupata mimba .Lakini unamjua hata mtu mmoja anayetumia kondomu na akapata mimba?
Naamini kabisa kama unaogopa hata kutumia kondomu kwa kuogopa kuukwaa MDUDU basi wewe unaogopa tu kufa. Na kama kuogopa kifo ndio kunakufanya uwe na tabia nzuri, basi kuna mengi yanakupita .Kumbuka hata iweje maisha ya binadamu ni mafupi.Na hata ujichunge vipi kwa namna moja au nyingine utakufa.
Kumbuka unaweza kufa kwa kuvimbiwa na maharage au kugongwa na baiskeli pia.
Au kama unaogopa sana kifo, jaribu kufarijika na dini.
Kaka Kitururu:
Kaaazi kweli kweli.
Je unaonaje tukifunga mjadala?
Au niuendeleze?
Ukweli ni kwamba bado sijaridhika na majibu yako!
@Koero: Endelea!
Dhumuni la mimi kuandika topiki hii hapa iliibuka baada ya rafiki yangu kudai topiki kama hii haiandikiki( hasa kwa mtu mwenyewe kuchanganya mapungufu yake na udhaifu katika vita ya mdudu).
Inadaiwa kutokana na watu kuogopa kuwa wakiandika ndani ya sentensi moja ``MIMI'' na ''UKIMWI'' ni kujichulia na watu wanaweza kuamini daima kuwa wana NGOMA ndio maana huwezi kuandika kitu ukitumia sentensi ikulengayo kwenye kitu taboo kuwa nacho kama gonjwa hili. Nikaamua kuandika ili watu waongee na labda katika kuongea zaidi kuna watu watajisikia kuliongelea swala zaidi na katika kuliongelea swala zaidi kuna watakaopata majibu zaidi.
Kwa kifupi kama unachakuendelea kuongelea na kufunza, ndio lilikuwa dhumuni la mimi kuandika hii post ambayo kuna rafiki yangu kaniambia nitaijutia:-)
Post a Comment